decomm
JF-Expert Member
- Dec 10, 2013
- 726
- 661
Habari wakuu!
Nawakumbusha waendeaha pikipiki kuwasha taa muda wote waendeshapo pikipiki...
Ukiwasha taa utawezesha wewe (pikipiki yako) kuonekana kwa urahisi kwenye 'driving mirror' au 'side mirrors' za magari yaliyo mbele yako...
Hata iwe mcha kweupee we washa taa tu! Ni utaratibu mzuri.
Baadhi yenu mnavaa viatu bya wazi mfano kanda mbili huku mkiendesha, haifai kufanya hivyo, vaeni viatu vya kufunika mguu vizuri...
Msiyapite (overtaking) magari upande wa kushoto... Wala msipenye penye kati ya gari na gari ni hatari sana kwenu...
Vaeni kofia ngumu (helmet)...
Fuateni Sheria mnapokuwa kwenye mataa ya kuongozea magari, fuateni sheria muda wote sehemu yoyote...
Madereva wenzangu na wapenda usalama barabarani mtakubaliana nami kuwa waendesha pikipiki sasa wamezidi kuvunja sheria na kujisahau kana kwamba wanayoyafanya ni sahihi.
Nawasilisha.