Washa Taa Mchana

Nyakarungu

JF-Expert Member
May 1, 2011
472
375
Nimefanikiwa kupata usajiri wa NGO, ya kijamii inayoitwa Home Of Diginity (HODi), hii itahusika na utetezi haki za binadamu kuhusu masuala ya afya mkoa wa Mara.
Mimi nikiwa mwenyekiti wa board napenda kutoa taarifa hii na ifahamike kuwa harakati hizi ni za kuhakikisha wanajamii wanapata haki yao
Walengwa
Walengwa ni wananchi wote wa mkoa wa mara,...
TUTAHUSIKA ZAIDI KUWATETEA NA KUPIGANIA HAKI ZA BINADAMU KAMA IFUATAVYO;-
1. Wafanyakazi wlioumia wakiwa kazini
2. watoto wa kike wanaokeketwa
3. wanawake wanaopigwa na kuumizwa na waume zao
4. wasiotendewa haki hosp..
5. wakulima wanaharibiwa mazao na wanyama pori,
Nikiwa mtu sahihi wa afya nina lengo la kuhakikisha afya ya binadamu inalindwa na kuheshimiwa, pia tutatumia fursa hii kutoa elimu ya uelewa wa mambo mbalimbali ya kijamii.........mengine tutajuzana as time go.........
 
Hongera sana mkuu, kwa pamoja tutaifikisha Tanzania pale inapostahili iwe.
 
Amen Ezan, naamini jamii inanidai niitumikie......hivyo nina wajibu wa kutokaa kimya nikiona mdororo wa maadili ya viongozi na wanajamii.
 
Safi sana kamanda, ila nakutahadharisha, kupitia asasi usiwe fisadi, tutakumulika tu, jitendee haki kwa kupigania haki za walio wengi, tamaa ya kujilimbikizia mali kamwe isikuingie.
 
Swala la Watoto na Wanawake ni la muhimu katika kuboresha matatizo yake,hongera katika kutmikia wananchi
 
washa taa vipi mpango wa mkiti bavicha?hongera kwa hili ila kwa kuanzia iwe mkoa wa mara baada ya taasisi kukomaawatu wote waruhusiwe kujiunga na kupata huduma hiyo muhimu.
 
Kazi nzuri mkuu. Nakutakia kila la heri. Nakuomba mkimaliza awamu ya huko Mara mje huku Arusha maana matatizo mnayoyashughulikia yapo kwa kiwango kikibwa sana. God bless you!
 
Hii ni kwa kuanza tu,ila tukipata uwezeshwaji,tutafika sehemu nyingi,kwani jamii haina wa kuisemea, hivyo tutapeleka elimu hii kwao.
Suala la ufisadi halina nafasi kwa mtu aliyejitoa bila kutumwa wala kuombwa afanye harakati,pia historia za nyuma za watu zaweza kuwa msaada mkubwa kwa wao kuushinda ufisi huo.
Mungu anisaidie niwaambukize wengine ari na moyo huu.

Pamoja na mm kuwa mwanaharakati wa kisiasa,ila hii haitahusika na siasa kabisa ili tutende kazi yetu bila kuingiliwa.
 
Nimefanikiwa kupata usajiri wa NGO, ya kijamii inayoitwa Home Of Diginity (HODi), hii itahusika na utetezi haki za binadamu kuhusu masuala ya afya mkoa wa Mara.
Mimi nikiwa mwenyekiti wa board napenda kutoa taarifa hii na ifahamike kuwa harakati hizi ni za kuhakikisha wanajamii wanapata haki yao
Walengwa
Walengwa ni wananchi wote wa mkoa wa mara,...
TUTAHUSIKA ZAIDI KUWATETEA NA KUPIGANIA HAKI ZA BINADAMU KAMA IFUATAVYO;-
1. Wafanyakazi wlioumia wakiwa kazini
2. watoto wa kike wanaokeketwa
3. wanawake wanaopigwa na kuumizwa na waume zao
4. wasiotendewa haki hosp..
5. wakulima wanaharibiwa mazao na wanyama pori,
Nikiwa mtu sahihi wa afya nina lengo la kuhakikisha afya ya binadamu inalindwa na kuheshimiwa, pia tutatumia fursa hii kutoa elimu ya uelewa wa mambo mbalimbali ya kijamii.........mengine tutajuzana as time go.........

Karibu.
Hongera mkuu
kuwa mwangalifu na fedha za ufadhili
hakikisha unafanya yale uliyoainisha hapo juu
maana NGO nyingi zimekuwa kwa ajili ya kujinufaisha na sio walengwa
 
Nakuaminia toka siku ile uliwasha taa mchana kweupe uwanja wa mbuzi kitaa kwetu bg up
 
Back
Top Bottom