Wasemaji kuhusu corona: Tumsikilize nani?

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,642
2,000
Awali tulibiambiwa maelekezo yote tutayapata kutoka kwa ama waziri wa Afya, Waziri Mkuu au Rais mwenyewe.

Pia, tuliambiwa tusikilize maelekezo ya wataalamu wa wizara ya Afya. Kauli hizi zilitolewa na viongozi wetu wakuu akiwemo mheshimiwa Rais.

Sasa naomba kuuliza swali hili,ni nani kwa sasa tumsikilize?
Baadhi ya wakuu wa mikoa wametangaza hatua za ziada zinazotakiwa kuchukuliwa.Mfano kuvaa barakoa kila unapotoka.

Awali msemaji wa wizara ya afya alisisitiza uvaaji wa barakoa sio muhimu kwa watu ambao hawajaambukizwa. Nakumbuka watu walishaanza kuvaa hizi barakoa bila hata amri kama zinazotolewa sasa. Na baada ya maelezo hayo tena ni daktari, waliovaa mitaani wakaonekana washamba tu. Leo wakuu wa mikoa (sio wasemaji wa huu ugonjwa) wanatoa maelekezo hayo.Tumsikilize nani?

Bado zinavaliwa masaa 4 zinatupwa? Na zikitupwa zinatupwaje? Au kuna sehemu zimeandaliwa za kutupa barakoa?
Vipi zilizotupwa zikizagaa mitaani, haziwezi kuwa chanzo cha kuenea kwa ugonjwa huu tena? Mamlaka zinajua uzito wa Ku-dispose barakoa zinazovaliwa kila baada ya masaa manne? Au watu wavae bila kujali masaa? Wasipozingatia masaa, nini kitatokea?

Kumbuka pia ukitoka masaa 8 kwa Siku ni barakoa 2 hizo ambazo ni sh. 2000@. Kwahiyo bajeti ya barakoa pekee ni sh. 4000@ siku. Kama ni mtumishi wa umma na unalipwa mshahara wa Shilingi laki nne, ujue kuna zaidi ya laki moja ya kununua barakoa pekee.

Tunaomba mwongozo tafadhali kutoka kwa wasemaji walioidhinishwa. Au hata kama kuna mabadiliko yamefanyika kuhusu wasemaji wa Covid-19


Sent using Jamii Forums mobile app
 

opondo

JF-Expert Member
Dec 28, 2017
280
1,000
Ninachokumbuka brother walisema hivi taarifa za wagonjwa wapya wa COVID 19 zitasemwa na waziri ummy mwalimu au waziri mkuu kassim majaliwa. Ila tuendelee kuchukua tahadhari tutakazopewa na wataalamu wa afya. (Sio taarifa zote pia tahadhari za kuchukua mpaka tupewe na waziri mkuu).

Ndugu kuvaa barakoa mpka upewe maelekezo na mtu? Kujiepusha kwenye misongamano mpaka uambiwe na mtu?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom