Wasemaji Jeshi La Polisi

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
214
Mara nyingi huwa najiuliza kama hawa makamanda wa jeshi la polisi ni wasemaji wa jeshi la polisi pia yaani katika mafunzo yao wamefundishwa kuwa wasemaji na watoa taarifa za jeshi lao kwa vyombo vya habari na vyombo vingine vinapotaka taarifa hizo au inakuwaje ?

Juzi niliangalia taarifa ya habari kutoka mkoani mbeya katika tukio lililotokea kyela , mkuu wa jeshi hilo mkoani mbeya ndio alijitokeza kuongelea suala hili badala ya mkuu wa jeshi katika wilaya husika au msemaji wa jeshi hilo mkoani mbeya au wilaya hiyo

Wakati huo huo katika tukio lingine lililiotokea mbeya mjini kamanda kova alitoa taarifa kwa vyombo vya habari , na kumbuka taarifa hizi sio kwa njia ya maandishi ni yeye kuhojiwa na kuelezea hali ya mambo ilivyo na ndio maana baadaye anaweza kugeuka na mambo kama hayo

Ni wakati sasa umefika jeshi la polisi liwe na wasemaji wao ambao watahusika katika kutoa taarifa na habari zingine kutoka jeshi hilo kwa raia na jeshi lingine ambao hiyo ndio fani yao na wamekomaa katika fani hiyo ya usemaji na utoaji wa taarifa .

Taarifa hizi zinazotolewa na wasemaji wa jeshi la polisi pia waziweke katika tovuti ya jeshi la polisi ili mtu wowote aweze kusoma na kufanyia kazi hapo baadaye hata kama mtu huyo hayuko Tanzania ili mradi aweze kupata huduma ya mtandao wa kimataifa .

Kukiwa na wasemaji wa jeshi la polisi naamini hakuta kuwa na taarifa za uwongo au polisi wenyewe kuteleza ulimi , sasa watakuwa wanafanya kazi kitekinoligia na kimaadili zaidi kuliko siku zingine zote za maisha yao .

Huwa inafurahisha sana kumwona mheshimiwa kama Suleiman kova yuko pale anasoma au kutoka habari ambazo hazimhusu , inauzi pia anapotembelea kila sehemu wakati yeye kuzunguka mitaani sio kazi yake .
 
Kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni yake kama katiba ya nchi inavyoeleza,sasa wewe mpaka kutoa hizi critism kwa kamanda kova, unajua taratibu wa upashaji habari ndani ya jeshi la polisi upo je?.Labda ni kusaidie kigodo,inspector general wa polisi amewapa mamlaka wakuu wa polisi miakoni kuwa wasemaji wa maeneo yao.miaka ya nyuma kulikuwa hata ma-OCD walikuwa wanatoa taarifa za maeneo yao hivyo sijaona nini kova amekosea.Mbeya yote ni area of his jursidiction.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom