Wasaudia wakiri uwanja wao wa ndege umeshambuliwa kwa kombora la Yemen

kimsboy

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Messages
4,384
Points
2,000
kimsboy

kimsboy

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2016
4,384 2,000
Wasaudia wakiri uwanja wao wa ndege umeshambuliwa kwa kombora la Yemen
Jun 12, 2019 15:45 UTC

Msemaji wa muungano vamizi wa Yemen amekiri leo kwamba jeshi na vikosi vya kujitolea vya wananchi wa Yemen wamejibu mashambulizi kwa kuupiga kwa kombora Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abha, mkoani Asir huko kusini magharibi mwa Saudi Arabia.

Katika taarifa aliyoisoma leo, Turki al Maliki amesema kuwa, kombora hilo la Yemen limepiga kwenye eneo la kufikia wasafiri la uwanja huo na kusababisha hasara za mali. Vile vile amesema kuwa, watu 26 raia wa nchi mbalimbali wamejeruhiwa kwenye shambulizi hilo.

Mapema leo Jumatano, Msemaji wa Jeshi na Vikosi vya Kujitolea vya Wananchi wa Yemen amesema kuwa vikosi vya nchi hiyo vimejibu jinai za Saudi Arabia na kundi la nchi zilizoivamia kidhulma Yemen, kwa kuushambulia uwanja wa ndege wa Abha wa Saudi Arabia kama ambavyo muungano huo vamizi nao umeharibu viwanja karibu vyote vya ndege vya Yemen.

Yahya Sarii, Msemaji wa Jeshi na Vikosi vya Kujitolea vya Wananchi wa Yemen ameongeza kuwa, shambulizi hilo ni majibu ya kawaida kabisa ya taifa la Yemen kutokana na jinai kubwa inayofanywa na muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati).

Kabla ya hapo pia jeshi la Yemen kwa kushirikiana na vikosi vya kujitolea vya wananchi lilizionya Saudia na Imarati kwamba viwanja vyao vya ndege havitobaki salama na vitalazimika kufungwa kama ambavyo wavamizi hao wamevifunga viwanja vya ndege vya Yemen kwa mashambulizi yao ya kiholela.

Msemaji wa jeshi la yemen
4bsic4d51549ff1fsln_800c450-jpeg.1125972
 

Forum statistics

Threads 1,307,080
Members 502,332
Posts 31,601,025
Top