Wasanii wengi wa Bongo kuimba Amapiano ni wazi Wabongo tunapenda vya kutafuniwa (kitonga)

BabaMorgan

JF-Expert Member
Dec 18, 2017
4,040
10,460
Amapiano ni muziki mzuri na hivi karibuni umekwenda Sana kwa kiwango kizuri (umu Jf tunasema umekwenda kwa kiwango Cha dreamliner) pongezi kwa wa SA yote hii ni matokeo ya uzalendo na kuamini Cha kwao kwa kukipigania bila ya kuchoka (Persistence).

Ukitazama Singeli na Amapiano ni miziki yenye tofauti kwa maana ya midundo na hata asili ya inapotokea lakini Ina sifa moja inayofanana nayo ni amsha amsha Kama Ni mpenzi wa kuyarudi Kama Mimi Baba Morgan ni wazi hutosimama DJ akiwa anafanya yake kwenye pioneer mashine.

Kitendo Cha wasanii wengi wa bongo kuimba Amapiano badala ya Singeli kwangu Mimi naweza kufananisha kitendo hicho na uhaini tumekisaliti Chetu mapema kisa ni mafanikio ya Amapiano Leo hii dunia nzima inajua Amapiano Ni muziki wa South Africa inapotokea wasanii wetu wa bongo wanaofanya vizuri kuimba Amapiano inatufanya kukosa uwakilishi katika burudani wa Nchi yetu pendwa Tanzania huko ulimwenguni.

Wapo watakaohoji kuwa tumeiga aina nyingi za miziki kwa nini kuiga Amapiano iwe makosa? Muendelezo wa makosa hauwezi kuhalalisha kosa.

Hakuna kitu kinakuja kwa urahisi haswa katika mafanikio(no pain no gain) tupambanie Chetu na kukifikisha pale tunapohitaji hapo ndipo uwezo wetu utaonekana.

Singeli hizi zikuburudishe jioni ya Leo.

1. Hamisa mobeto - Ex wangu
2. Easy man - Fatuma na juma
3. Rayvany - Miss Buza
4. Harmonize - Hujanikomoa
5. Mzee wa bwax - kisimu changu

From northern part of Tanzania.
 
Broo siyo huko kwenye muziki tu inshort ukifuatilia asilimia kubwa wabongo sie huwa hatuna consistence kwenye mambo yetu plus ujanja ujanja mwingi ili mradi tu mambo yaende but kiuhalisia hatuna vya kwetu vya kujivunia
 
Sure kwenye Amapiano wa Tz wanaupiga mwingi utadhani joburg imehamia bongo.
 
Jana tu kuna dogo nimemwambia kuwa hawa wasanii wa bongolala flavor kama wangekua na akili timamu wangeheshimu mziki wa asili yao ili ifike hatua Burnaboi or mafikizilo watoe nyimbo zao kwenye mdundo wa singeli.
 
Punguzeni ushamba kidogo hao walioimba izo bongo flavor asili walifika wapi?

Mziki ni biashara unaaangalia kwa sasa soko linataka nn unachangamkia fulsa.

Ukijifanya wewe ni m bongo flavor kindaki ndaki utaishia kuwa na jina kubwa hapa bongo na huna kitu mfukoni, hapa sina haja ya kutoa mfano wa wasanii ambao walikuwa na uwezo wa kibadilika kisanaa na wakapiga pesa, ila walijifanya wabongo flavor mwisho wasiku wamebaki majina tu.
 
Mbona uwezekano wa kuifanya bongo flava au singeli kibiashara upo solution ni Kufanya mziki kiubunifu zaidi mbona watu watapenda kuliko kukopi na kupaste kunakofanyika saa hivi.
 
Jana tu kuna dogo nimemwambia kuwa hawa wasanii wa bongolala flavor kama wangekua na akili timamu wangeheshimu mziki wa asili yao ili ifike hatua Burnaboi or mafikizilo watoe nyimbo zao kwenye mdundo wa singeli.
Wagumu kukubali vya kwetu tunapenda vitu vya nje hata kama sio Bora kuzidi Cha nyumbani
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom