Luteni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 2,274
- 301
Akihojiwa na Bongo Radio msemaji wa Joseph Mbilinyi a.ka Mr. Sugu(MB elect) ndugu G. Solo amesema kuna baadhi ya wasanii waliokuwa wakimpiga vita Sugu kwenye majukwaa ya CCM wameanza kujipendekeza, amesema wengine walikuwa wanakwenda Mbeya kufanya Shoo makusudi ili kumchafulia Sugu bila hata kumsalimia leo wameanza kumpigia simu. Lakini anawapa live kuwa wao waendelee kutumiwa tu na CCM kama mipira na baadaye kutupwa na yeye anaenda bungeni kuwatumikia wananchi ikiwa ni pamoja na masilahi yao(wasanii).