Wasanii Wa Ngoma Za Asili Watakiwa Kujisajili Kupata Fedha Za Mfuko Wa Sanaa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,001
9,866
Serikali imesema kuwa wasanii wa ngoma za asili wanatakiwa kujisajili kwa maafisa Utamaduni wa Wilaya ili waweze kupata fedha za Mfuko wa Utamaduni na Sanaa ambapo kwa mwaka wa fedha 2021/2022 mfuko huo umetengewa bilioni 1.5.

Kauli hiyo imesemwa Julai 24, 2021 na Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Sanaa wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi Leah Kihimbi katika Tamasha la Cigogo linalofanyika Chamwino mkoani Dodoma.

“Pesa hizo zinatolewa kwa vikundi vilivyofanya usajili na siyo sandakalawe nendeni kwa maafisa utamaduni wa wilaya ili muwe na sifa ya kupata pesa hizo vinginevyo pesa hizo zitapangiwa matumizi mengine.” Amesema Bi Kihimbi.

“Utamaduni wetu lazima tuulinde kama Mheshimiwa Rais Samia Suluhu anavyosisitiza ili uwepo katika jamii yetu milele na milele.” Ameongeza Mkurugenzi huyo Msaidizi.

Naye Mkurugenzi wa Maendeleo ua Utamaduni wa Wizara hiyo Dkt Emmanuel Temu amesema kuwa matamasha ya utamaduni yanapofanyika ni vizuri kuwashirikisha watu kutoka kila rika ili kuhakikisha mila na tamaduni za kitanzania zinarithiwa kwa haraka kutoka kizazi kimoja kwenda kingine.

Pia katika tamasha hilo tahadhari dhidi ya ugonjwa Uviko 19 umesisitizwa kwani ugonjwa huo ni hatari sana kwa afya ya binadamu na washiriki wote wameomba kufuata kanuni za afya.

Tamasha hilo la kitamaduni linafanyika kwa siku mbili tarehe 24 na 25, 2021

MICHUZI BLOG
 
Back
Top Bottom