Wasanii wa movie bongo na kampuni zao

warumi

R I P
May 6, 2013
16,273
18,380
Wasanii wa movie apa bongo hususani wa kike wengi, wameonyesha juhudi za kutaka kumiliki kampuni zao binafsi za kutengeneza filamu.hili wazo ni zuri sana kwani inaonyesha jinsi walivyo improve sanaa zao hadi kuamua kumiliki kampuni zao ilo kujiongezea kipato zaidi.Sasa hili suala kwa sasa ivi linaonekana kama fashion au mashindano, na wasanii wengi hufungua kampuni ili tu kuonekana na yeye anazo au kwa sababu zao wenyew binafsi.kwa mfano AUNT EZEKIEL alianza kufungua kampuni yake ya cream entertainment ambapo alitoa movie nne tu ambazo hata hivyo hazikufanya vizuri sokoni,ikaenda baadae akaamua kuacha kabisa kutengeneza filamu zake,akaja JACKLINE WOLPER naye akafungua kampuni yake ambayo kutokana na ubovu wa movie anazotoa kampuni yake haikuweza kufika mbali ikafa,akafuata ROSE NDAUKA naye katoa movie kutokana na kuvamia fani na yeye hakuna hata movie yake moja iliyoweza kufanya vizuri sokoni,akapotea japokuwa nasikia kuna film anaandaa,mwingine ni LUCY KOMBA huyu mwanadada alikuwa anafanya vizuri apo awali alitoa film yake ya DIVERSION OF LOVE ambayo ndiyo iliyomtoa uwoya na wasanii wengine wengi,big up lucy ila na yeye akakimbia game,mwingine ni NISHA huyu ni mgeni tu kweny film industry nasikia na yeye ana kampuno yake tayari japokuwa sina uhakika kama atafika mbali,ivi sasa tena WEMA SEPETU na yeye kafungua kampuni yake ambyo imepata umaarufu mkubwa apa jijini bila kutoa movie hata moja,hongera sana kwa mwanadada JENNIFER KYAKA au ODAMA,huyu ni zao la mussa banzi alianzisha kampuni yake miaka mitatu iliyopita hadi sasa bado anafanya vizuri kwenye game,hongera sana dada,swali ni je kwa hizi kampuni ambazo kila msanii akiigiza leo kesho ana kampuni yake kwel tutaendelea??,ebu waangalieni wenzenu apo nigeria akina MERCY JOHNSON,INI EDO,OGE OKOYE,RITAH DOMINIC,GENEVIVE NA OMOTOLA,hawa wadada ni waigizaji wakali sana nigeria,hata siku moja sijawahi sikia inni edo au genevive ana kampuni yake ya filamu japokuwa najua uwezo wa kufanya hivyo wanao.hii ni kutokana na kuwa wanaheshimu sana kazi zao,hata siku moja sijawahi kuta movie ka direct ini edo au yvonne nelson,apa hamjiulizi ni kwa nini hawafanyi hvyo??,wabongo ni wazuri sana kwa kuiga jaribuni na kuiga na hili kwa wenzenu.for the love of the game
 
mkuu umenena kweli ingawaje femnist watakushtaki make auja consider gender ila nimefurai ulipomtaja mercy johnson viva.
 
Mkuu kweli hilo la kila mmoja wao kumiliki kampuni nakubaliana na wewe.
Ila kwenye kudirect yvone Nelsson na van vicker wana direct.
Hata hivyo safari ya bongo movie bado ni ndefu.
Sijaona kitu bado.
 
Nikiangalia movie ya Warner bros, Fox, Lions Gate au Paramount halaf uje uniwekee sijui movie ya RJ mara Kanumba ze Great naweza nisiongee na ww mwaka mzima.. Quality matters!
 
kufungua kampuni ya film bongo unahitaji kitu kimoja tu Computer.......camera,light,boom mic na zana zingine utakodisha kwa wenye nazo au kuazima,editor laki na nusu mpk movie inakwisha na camera crew utawapata kibao kwa sh 30,000 per day tena wengine malipo mpk movie ikitoka,sasa kwanini kila mtu asiwe na kampuni.......
 
Pamoja mwana,mie siangalii huo uchafu uitwao bongomovie kamwe,its rubbish
Nikiangalia movie ya Warner bros, Fox, Lions Gate au Paramount halaf uje uniwekee sijui movie ya RJ mara Kanumba ze Great naweza nisiongee na ww mwaka mzima.. Quality matters!
 
Samahani hivi hizi kampuni zimesajiliwa na brella? Na je zinatambuliwa na TRA?
 
Mimi naonaga mauzauza 2 movie ina title ya kiingereza ndani wanaongea kiswahili. Ukienda kwenye subtitles ndo balaa.
Hii nchi kila kitu maajabu

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom