Wasanii wa kiume kujichubua inakuwaje hii? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wasanii wa kiume kujichubua inakuwaje hii?

Discussion in 'Celebrities Forum' started by UPOPO, Jan 14, 2011.

 1. UPOPO

  UPOPO JF-Expert Member

  #1
  Jan 14, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 1,371
  Likes Received: 718
  Trophy Points: 280
  KUNA mdau mmoja ambaye ni mwanamke anajaribu kuongea na Fc huku akiomba jambo analotaka kushiriki na sisi tusimpuuze kwani yeye ana uhakika nalo jambo hilo, ndio maana anataka liwafikie jamii na kujadiliwa, lakini hapo awali alianza kwa kulalamika kuwa mara nyingi kasoro au matatizo ya wasanii wa kike yamekuwa yakiwekwa hadharani lakini akina kaka hayaongelewi.

  Mwanadada huyu ambaye hataki jina lake litajwe katika mtandao huu anasema kuwa yeye ana uhusiano na msanii muigizaji mahiri katika tasnia ya filamu, boy friend wake huyu anapenda kujipiga deki katika uso wake, unajua kupiga deki uso?

  Yaani mchizi anajichubua kwa kutumia madawa wanayotumia akina dada katika mambo yao ya urembo, binafsi sina hakika wala ushahidi lakini lisemwalo lipo kama halipo laja Fc ilijaribu kumdadisi mwanadada kuhusu jambo hili na kutaka kujua labda aliwahi kumuuliza mtu wake kwanini anaharibu ngozi yake?

  “Yeye aliniambia kuwa kamera inapenda watu weupe kwa hiyo kwa sababu hiyo ndiyo kazi yake ili auze sura vizuri anaamua kutumia Cream ili awe mweupe, maana akiwa mweupe hawezi kukosa casting, akiwa mweusi hawezi kupewa casting hiyo ndiyo sababu kubwa ya wasanii wa kiume kujichubua kaka yangu”

  Lakini siku za nyuma kuna muigizaji mwingine wa siku nyingi ambaye kwa sasa haigizi aliwahi kuwalaumu baadhi ya wasanii wa kiume kutia dawa katika nywele pamoja na kupaka wanja katika nyusi zao jambo ambalo aliona kama lilikuwa halina maana, pengine tusiwalaumu kwa sababu wanaweza kuwa na sababu za msingi kuweza kutetea urembo huo ambao kuna wakati uleta utata kwa wanajamii.

  Lakini iwapo utakuwa na filamu maalum kama ambavyo msanii Hisani Muya (Tino) ambaye kwa sasa alikuwa akirekodi filamu ya Ushoga nafikiri hakuna shida katika kugombea poda, Cream na wanja na mpenzi wako, kwa sababu yupo katika filamu ambayo inaendana na mambo hayo ya kishoga kwani mashoga wengi upenda kujinasibu kama wanawake.

  Haya wasanii wetu jirembeni ili muuze sura lakini kama ikitokea watu wakihoji kuhusu matumizi ya vifaa vya kinadada waelimisheni kuhusu jambo hilo kuwa ni mambo ya kikazi tu lakini tukiwa kitaa haiwi hivyo.Zaidi kuhusu mambo ya filamu na wasanii ingia http://www.filamucentral.co.tz/

  *

  SOurce: MICHUZI JR Tarehe: Thursday, January 13, 2011 | ? | Perm
   
 2. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #2
  Jan 14, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  machoko tu hao,na wavivu wa ubunifu, mbona black america kama Denzel Washngton, will smith hawajichubui?
   
 3. O

  Okdabwai New Member

  #3
  Jan 21, 2011
  Joined: Jan 21, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sure kabisa yaani hii inaonesha wa2 wengi wabongo walimbukia mambo.cjui nnani kawaambia kujichubua ndio dili manake dah!
   
 4. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #4
  Jan 21, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Watoto si ridhiki hao :frusty:
   
Loading...