Wasanii wa filamu Tanzania na uchanganyaji wa lugha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wasanii wa filamu Tanzania na uchanganyaji wa lugha

Discussion in 'Sports' started by mamsindo, Oct 4, 2010.

 1. mamsindo

  mamsindo Member

  #1
  Oct 4, 2010
  Joined: Jan 8, 2010
  Messages: 28
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 5
  Kuna swala ambalo linakera sana kutoka kwa wasanii wetu wa filamu Tanzania.Hivi ili filamu ionekane nzuri ni lazima kutumia kingereza?Mbona wenzetu wahindi hutumia lugha yao tu na sinema zao zinapendwa?Mimi nadhani wasanii wabadilike,na watumie ama kingereza kitupu au kiswahili katika sinema nzima.Kingereza si lugha yetu na wengi wa wasanii wetu huonekana kuwa lugha hiyo inawapa shida hasa ila huenda hulazimika tu kuitumia LABDA (kama wanavyodhani wenyewe) kwa ajili ya kuapata soko la filamu zao_Ongeeni kiswahili fasaha na muweke tafsiri ya kiingereza kama mnataka kuuza kwa wanaoongea kingereza.

  Jukumu la kukuza kiswahili ni letu wenyewe sasa tukikimbilia kingereza tusichokielewa vizuri,lugha yetu (kiswahili) itakuzwa na nani.Tuache ulimbukeni kwani ni AIBU MNO.Nimeangalia sinema nyingi za lugha mbalimbali na zote nilizoangalia wasanii wametumia lugha zao asilia mfano kierumani,Kidenish,Kiswidi n.k bila kuchanganya na kingereza.Sinema zote hizi zina tafsiriwa kwa kingereza au lugha nyingine mbali na lugha zilizotumika katika filamu hizo.
   
Loading...