Wasanii wa filamu ni muhimu wapewe elimu ya utambuzi na udadavuzi wa sanaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wasanii wa filamu ni muhimu wapewe elimu ya utambuzi na udadavuzi wa sanaa

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by maliki marupu, Dec 30, 2011.

 1. m

  maliki marupu Member

  #1
  Dec 30, 2011
  Joined: Nov 5, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nawashukuru sana wachangiaji wa mada tofauti mlizochangia. Ninamatumaini makubwa na imani kubwa na nyinyi, kutokana na uwezo mkubwa wa utambuzi wa mambo.leo katika jamvi letu la jukwaa la taaluma tunaona ni muhimu kujadili suala zima la elimu ya sanaa kwa wasanii wa tanzania.tumeona matukio mbalimbali yakiwakabiri wasanii wa filamu .miongoni mwa matatizo yanayowakabiri ni upatikanaji wa hati miliki ya kazi zao.pia ni kuibiwa kwa kazi zao.hii ni kutokana na wasanii kushindwa kudhibiti waharamia wanaotoa kazi zao bila kuwashirikisha kwa kuchoma cd zenye michezo yao na kuuza.pia tumeona migogoro katika makundi ya sanaa ya uigizaji migogoro isiokuwa na mwisho.vilevile tumeona namna utamaduni wa kitanzania unavyokiukwa katika baadhi ya filamu zinazotolewa na wasanii.kunabaadhi ya filamu huwezi hata kuziona na familia.pia wasanii wanaonekana kutokuwa na jumuiya au chama madhubuti kwa ajili ya kutetea haki zao za msingi.kutokana na matatizo kama haya naona kuna umuhimu wa kuwepo kwa elimu mahususi katika sanaa ili kuwafanya wasanii kutambua haki na wajibu wa kazi zao.pia wasanii wanapaswa kuelimishwa vya kutosha juu ya sheria mbalimbali zilizowekwa ili kulinda haki zao za msingi.vilevile wanapaswa kufahamishwa namna ya kuandika mikataba ya kazi zao ili kuwapa tija kiuchumi.hii ni kutokana na ukweri kuwa sanaa hii imekuwa ni mahali pa ajira kwa vijana.na si mahali pa kutumia sanaa kama sehemu ya kupata umaarufu usio na tija nini kifanyike kuimalisha fani hiiiii?
   
Loading...