Wasanii wa Bongo wamtelekeza Idris, hakuna aliyeenda kumwangalia wala kumpost

Chifyono

JF-Expert Member
Oct 16, 2017
921
1,658
Habari wakuu,

Waswahili waliosema kufaaye kwa dhiki ndiye rafiki hakika waliona mbali na hawakukosea.

Msanii Idris Sultan (comedian) kwa sasa anashikiliwa na jeshi la polisi kwa makosa ya kimtandao. Kama msanii ilivyo kawaida kwa wasanii wote wanapokuwa na matatizo mbalimbali, huungana pamoja kuweza kumsaidia mwenzao hata kwa kumfariji tu.

Hali imekuwa tofauti awamu hii kwa msanii huyu aliyewahi kushinda BBA 2014, kwa sasa hakuna msanii yeyote yule mwenye kuonesha kushirikiana nae, kumfariji, kumsaidia kutatua tatizo wala hata kumpost tu katika social network.

Watanzania hususani watu wake wa karibu wote wamemgeuka, hili ni funzo kwetu si kila anaekuchekea anakutakia mema wengine ndio hivyo wanafurahia unapokuwa unapitia mabovu katika maisha.
 
Huwa nasema kila siku Idris analazimisha kipaji.. kitu anachofanya sio chake halafu watu wengi hawamuelewi. Wakati umefika ajitathmini na kuacha kabisa inshu ya ukomediani
Hayo uliyoandika yanahusiana vipi na hii mada? na unaanzaje kusema Idris sio comedian ikiwa wewe tu ndio hucheki?

Tafuta kazi ya kufanya mtoto wa kiume chuki haikusaidii!
 
Back
Top Bottom