Wasanii wa bongo ni kweli kioo cha jamii? Wapi nyimbo za maombolezo ya mauaji arusha? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wasanii wa bongo ni kweli kioo cha jamii? Wapi nyimbo za maombolezo ya mauaji arusha?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by George Maige Nhigula Jr., Jan 11, 2011.

 1. George Maige Nhigula Jr.

  George Maige Nhigula Jr. Verified User

  #1
  Jan 11, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 470
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Napigwa butwaa na wasanii wetu wa Tanzania wanavyojiita kuwa ni kioo cha jamii wakati huwa wanaendekeza njaa zao na kufumbia macho masuala muhimu jamii wanayoishi kwasababu ya kufunga fungate na CCM na kutumiwa kama toillete paper wakati wa kampeni.

  Huwa nategemea wasanii kuwa mstari wa mbele kutunga nyimbo za kuomboleza na kulaani kitendo cha jeshi la polisi kuwanyamazisha milele watanzania kwa kuwauwa na kuwashambulia kwa risasasi na mabomu bula huruma.

  Je hawa wasanii wetu wanajua nafasi yao kwenye jamii yao kwani hawaonekani kwenye harakati za ukombozi au ndo njaa imewafanya wawe vipofu na kutokuwa na moyo wa huruma kwa jamii inayoangamia kwa utawala wa mabavu na ukandamizaji wa haki za binadamu?
   
 2. Eng. Smasher

  Eng. Smasher JF-Expert Member

  #2
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 13, 2010
  Messages: 746
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nilikuwa nawakubali sana WAGOSI wa kaya!!
  Sijui wapo wapi hawa jamaa???!!!
   
 3. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #3
  Jan 11, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  Kwani mauaji ya Arusha ni 'mapenzi'?
  Au watalipwa na nani?
   
 4. George Maige Nhigula Jr.

  George Maige Nhigula Jr. Verified User

  #4
  Jan 11, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 470
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Sometimes you do things for your country as public service sio mpaka ulipwe, hata ukiwa na wimbo wako wa maombolezo na kulaani mauji ya arusha, wazalendo na wanaharakati wengi watadhamini kurekodi wimbo huo, wasanii wetu wamekosa uzalendo na ubunifu period!
   
 5. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #5
  Jan 11, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Wagosi bado ni wapiganaji makini walimpa support sana sugu kule mbeya wakati wa kampeni
   
 6. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #6
  Jan 11, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Wako bize kuandaa za uchaguzi ujao!
   
Loading...