Wasanii wa Bongo Movie wametuaminisha Watanzania kuwa Walilipwa kuturubuni

Zero Hours

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
12,943
18,665
Siku zote mimi nilikuwa naimani kuwa hawa wasanii waliokuwa kwenye kambi ya mama ongea na mwanao walikuwa wakiisaidia CCM kwa mapenzi ya chama chao.

Sasa nimekuja shangaa kuwa hivi sasa wao wenyewe wanaeleza kuwa ile kazi ilikuwa ya mapatano ya malipo flani. Kwa kifupi ni kuwa hawakufanya kwa mapenzi ya CCM walifanya kwa mapenzi ya pesa.

Hii inamaanisha kuwa, Wanasiasa hasa Wa CCM walitumia Wasanii wa bongo movie kuwarubuni watanzania kuwa wapo upande flani wa chama kumbe walikuwa wakilipwa.

Hivi yale malipo yanatofauti gani ni Hongo?
 
Ulaya na Marekani vyombo vya habari vinanunuliwa kufanya propaganda! Lobbying companies nazo zinakuwaga kazini kipindi hicho. Zote hulipwa. Sembuse Tanzania kulipa wasanii!!!
 
Siwalituonyesha mikoko ya nguvu, wema alituonyesha rangerover sport car, shilole alituonyesha mercedez benz, stive nyerere yeye alikuwa anakula bata na jimama ufukweni, mh sasa hata hela ya vocha hawana! Lazima walipewa za chumaulete.
 
Unataka kusema aliye chaguliwa hakuwa anafahamu matumizi ya fedha za chama kwa kikundi hicho? Au alikuwa ana dhani wakina Nyerere walikuwa wana zunguka bure tu? 2020 nadhani itakuwa ni kampeni ya Baba ongea na Bashite.
 
Siku zote mimi nilikuwa naimani kuwa hawa wasanii waliokuwa kwenye kambi ya mama ongea na mwanao walikuwa wakiisaidia CCM kwa mapenzi ya chama chao.

Sasa nimekuja shangaa kuwa hivi sasa wao wenyewe wanaeleza kuwa ile kazi ilikuwa ya mapatano ya malipo flani. Kwa kifupi ni kuwa hawakufanya kwa mapenzi ya CCM walifanya kwa mapenzi ya pesa.

Hii inamaanisha kuwa, Wanasiasa hasa Wa CCM walitumia Wasanii wa bongo movie kuwarubuni watanzania kuwa wapo upande flani wa chama kumbe walikuwa wakilipwa.

Hivi yale malipo yanatofauti gani ni Hongo?
Yule aliyetunga nyimbo ya kumsifu Mzee Lowassa alifanya kazi ile bure tu?. Wale wote walioweka mabango makubwa ya Mzee ENL na wao walikuwa wanajitolea tu?.

Mleta mada, dunia ya hisani ni ile unayoiota usiku ukiwa umelala. Maisha ya sasa hayana bure.

Na ndio maana ya kampeni za kisiasa, kila sehemu unapoona kampeni basi tambua kwamba kuna fedha imetumika.
 
Ulaya na Marekani vyombo vya habari vinanunuliwa kufanya propaganda! Lobbying companies nazo zinakuwaga kazini kipindi hicho. Zote hulipwa. Sembuse Tanzania kulipa wasanii!!!

Unataka kusema kwa sababu Ulaya na Marekani Ushoga ni kitu cha kawaida na Tanzania nao tuone ni kitu cha kawaida?
 
Wakati wa kampeni tulishuhudia wasanii wakifanyia ccm kampeni kwa mbwembwe kubwa tukajua mna mapenzi na ccm kumbe pale mlikuwa mnalipwa, na mmekubali wenyewe kuwa mlilipwa hii maana yake nini?

Hii maana yake ni kwamba nyie ni wanachama Wanafiki sana hamna mapenzi na hicho chama maana mngelikuwa na mapenzi na hicho chama mngelifanya kampeni bure, ni aibu vilevile kwa chama chama cha mapinduzi kununua wasanii kwa ajili ya kuwafanyia kampeni.
 
Ni matatizo ya Malezi. Wakati wa uchaguzi ni muda wa watu kutengeneza mitaji
 
Wakati wa kampeni tulishuhudia wasanii wakifanyia ccm kampeni kwa mbwembwe kubwa tukajua mna mapenzi na ccm kumbe pale mlikuwa mnalipwa, na mmekubali wenyewe kuwa mlilipwa hii maana yake nini?

Hii maana yake ni kwamba nyie ni wanachama Wanafiki sana hamna mapenzi na hicho chama maana mngelikuwa na mapenzi na hicho chama mngelifanya kampeni bure, ni aibu vilevile kwa chama chama cha mapinduzi kununua wasanii kwa ajili ya kuwafanyia kampeni.
Nauhakika hata chadema wakisafiri kikazi, wanadai risiti ili waje warudishiwe hela.
 
Sasa hivi hawana chao hata 2020 watamshawishi nani!
Tunajua ni njaa tu inawasumbua!!
 
wale ni wasanii walidzain jambo lao wakapeleka bac wakaingia mkataba...sidhan kama kuna haja ya kujadili mbona sio ajabu
 
Nimekumbuka mbali sana kipindi mbunge wangu wa kilombero peter lijualikali mwanzoni aligombea udiwani ifakara mjini basi ccm wilaya walimleta diamond nampenda sana ila nikasema kura yangu kwa peter lijualikali na alishinda udiwani
 
Wasiwasi wangu hata huyo aliyekuwa anajiita kada ambaye kakimbilia chadema kwa skendo ya bangi kumbe naye alilipwa..inavyoonekana hawa si wanasiasa ni wafanyabiashara na ndio maana ccm ikimaliza uchaguzi inawatosa..maana walishamalizana kibiashara..
Swali la msingi ni je wema ataweza kuvumilia ukata wa chadema au itabidi chadema waandae posho ya wema kutoka kwenye ruzuku??
Je itakuwepo nafasi ya viti maalum kwa wema au ataingizwa mkenge kama wolper?? Maana bora ulipwe walau utajua ulilipwa..sasa pesa ukose na ubunge ukose..hiyo hasira yake ni balaa.
Wema ni mtu ambaye hawezi kukaa na watu muda mrefu..je wataweza kum maintain aweze kaa muda mrefu na bavicha bila kunyenyekewa kama anavyopenda??
 
Wakati wa kampeni tulishuhudia wasanii wakifanyia ccm kampeni kwa mbwembwe kubwa tukajua mna mapenzi na ccm kumbe pale mlikuwa mnalipwa, na mmekubali wenyewe kuwa mlilipwa hii maana yake nini?

Hii maana yake ni kwamba nyie ni wanachama Wanafiki sana hamna mapenzi na hicho chama maana mngelikuwa na mapenzi na hicho chama mngelifanya kampeni bure, ni aibu vilevile kwa chama chama cha mapinduzi kununua wasanii kwa ajili ya kuwafanyia kampeni.
That was a business..wao walikuwa washereheshaji ndio maana walilipwa..kisiasa inaruhusiwa na ndio maana hawakuwa watoa sera wakuu.
 
Back
Top Bottom