Wasanii vijana matajiri bongo

TANZANIA ina vijana waliojaliwa vipaji vikubwa mno na laiti kama wangepata sapoti zaidi ya hapa walipo, basi wangekuwa mbali mno kwenye sayari hii ya dunia. Kwa sasa vijana wetu wanapenyeza na kulishika soko hasa la muziki Afrika Mashariki na Afrika kwa jumla. Lakini ukweli ni kwamba vipaji vinalipa na ndicho hasa kinachojitokeza kwa baadhi ya vijana ambao ni wasanii wa Bongo. Kupitia vipaji wana maisha mazuri. Wanakula, kunywa na kuvaa vizuri. Wanaishi kwenye majumba mazuri na kuendesha magari ya kifahari. Ifuatayo ni listi ya mastaa 10 ambao uchunguzi wa Ijumaa Wikienda umebaini wanaongoza kwa utajiri Bongo;View attachment 963368

NASIBU ABDUL ‘DIAMOND PLATNUMZ’
Ukiacha muziki wake unaouza sehemu mbalimbali duniani, malipo ya YouTube yanayotokana na video zake kutazamwa na mamilioni ya watu, staa huyu namba moja wa Bongo Fleva, kwa sasa anatajwa kuwa ndiye msanii tajiri zaidi Afrika Mashariki.
Uchunguzi wa Ijumaa Wikienda ulibaini kwamba, utajiri wa Diamond unatokana na biashara zake mbali na muziki ambapo amekuwa akiingiza mkwanja mrefu kupitia bidhaa za Diamond Karanga, Chibu Pafyum, ubalozi kwenye kampuni kubwa kama ilivyokuwa kwa Cocacola, na Vodacom na sasa Belaire na Pepsi. Pia mkwanja mwingine mrefu anauingiza kupitia usimamizi wa wasanii walio chini ya lebo yake ya Wasafi kama Harmonize, Rayvanny, Mbosso, Queen Darleen na Lavalava.
Diamond anaongoza kwa kupiga shoo nyingi zenye malipo makubwa ndani na nje ya nchi likiwemo tamasha lake linaloendelea la Wasafi Festival. Hadi mwaka jana, Diamond alitajwa kuwa na utajiri uliofikia Dola za Kimarekani milioni 4 (zaidi ya shilingi bilioni 8 za Kibongo), lakini mwaka huu utajiri wake unatajwa kuongezeka maradufu.
Kwa utajiri huo, Diamond anamiliki nyumba kadhaa jijini Dar ikiwemo ile ya kifahari anayoishi iliyopo Madale-Tegeta. Mbali na kumiliki majumba Dar na ile aliyomnunulia mzazi mwenzake aliyezaa naye watoto wawili, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ iliyopo nchini Afrika Kusini, pia anamiliki magari makali kama BMW X6, Toyota Land Cruiser V8, Toyota Prado na mengine ya kawaida.

EMMANUEL MGAYA ‘MASANJA MKAND-AMIZAJI’
Kijana huyu ambaye ni msanii wa vichekesho, nyimbo za Injili na ni mchungaji, naye anatajwa kwenye listi ya vijana wenye mkwanja mrefu. Masanja alianza kuingiza mkwanja kitambo kupitia Kundi la Ze Comedy kisha Orijino Komedi kabla ya kuwa msanii wa kujitegemea. Anaingiza pesa kupitia semina, shoo zake za Injili na vichekesho vya majukwaani na vile anavyovirusha mitandaoni. Pia anajihusisha na kilimo kikubwa cha mpunga mkoani Iringa.
Kwa kufanya kazi kwa bidii, Masanja anamiliki nyumba za maana, moja ni ghorofa ipo Tabata, nyingine Kigamboni na nyumbani kwao, Mbarali, Mbeya. Kwa upande wa magari, Masanja anamiliki ndinga kali kama BMW X6, Toyota Land Cruiser V8, Nissan Hardboard, Toyota Verossa na mengine ya kawaida.

JOSEPH MBILINYI ‘SUGU’
Sugu ni mmoja wa waasisi wa Bongo Fleva. Amefanya muziki huu kwa takriban miongo miwili na kujipatia mafanikio makubwa. Kabla ya kuwa Mbunge wa Mbeya Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Sugu alijiingizia mkwanja mrefu kupitia kuuza muziki na shoo mbalimbali. Baada ya kukwaa ubunge mwaka 2010, Sugu aliendelea na muziki ambapo amekuwa akipiga shoo mojamoja kwa ajili ya kuchangia elimu kwa watoto wa maskini jimboni kwake.
Kwa mkwanja alionao, Sugu anamiliki mjengo wa kifahari jijini Mbeya alioupa jina la Khaki House. Pia kuna taarifa kuwa anamiliki mjengo mwingine jijini Dar. Mbali na mijengo hiyo, Sugu anamiliki hoteli ya kitalii ya nyota tatu iitwayo Desderia iliyopo jijini Mbeya. Kuhusu usafiri anaomiliki, baada ya kuwa mbunge anatembelea ndinga kali aina ya Toyota Land Cruiser V8 na magari mengine ya kawaida.

JOSEPH HAULE ‘PROFESA JAY’
Kama ilivyo kwa Sugu, Jay ni miongoni mwa wasanii wakubwa walioupa ‘platform’ muziki wa Bongo Fleva.Katika kipindi chote alichofanya muziki huo kabla ya kuwa Mbunge wa Mikumi kupitia Chadema mwaka 2015, Jay aliuza muziki na kufanya shoo nyingi kubwa ndani na nje ya nchi zilizomuingizia mkwanja mrefu.
Ukiachia mbali umiliki wa studio yake ya Mwanalizombe, Jay amewekeza kwenye biashara mbalimbali ikiwemo saluni ya kisasa iliyopo Msasani na shule ya watoto iliyopo jijini Dar. Pamoja na ubunge, Jay ameendelea kufanya muziki kwa kutoa ngoma kali zinazomuingizia mkwanja kupitia YouTube na shoo mbalimbali.
Kwa utajiri alionao, ukiacha ule mjengo wake uliobomolewa ili kupisha upanuzi wa Barabara ya Morogoro pale Kimara- Temboni jijini Dar, jamaa huyu anamiliki mjengo mwingine na viwanja jijini Dar na jimboni kwake, Mikumi mkoani Morogoro. Baada ya ubunge, sasa Jay anasukuma ndinga kali aina ya Toyota Land Cruiser V8 na magari mengine ya kawaida.

ALI SALEH KIBA ‘KING KIBA’
Kiba ni mmoja wa wasanii wenye mkwanja mrefu Bongo na mafanikio yake yalianza kuonekana kuanzia mwaka 2014 alipoamka rasmi kwa mara nyingine na kurudi kwenye gemu kwa kishindo na ngoma yake ya Mwana. Kiba, kama alivyo mshindani wake, Diamond Platnumz, naye amekuwa akifanya shoo nyingi ndani na nje ya nchi hasa nchini Kenya na kujiingizia mkwanja mrefu.
Mbali na kuuza muziki na shoo zake, Kiba amekuwa akitia kibindoni mamilioni ya shilingi kila anapoachia ngoma mpya ambapo hupata ‘views’ nyingi na kusababisha apate fedha nyingi kutoka YouTube. Pia ni mmoja wa wamiliki wa lebo ya muziki ya Rockstar4000 kwa upande wa Afrika huku kwa hapa nyumbani akiwa anamiliki lebo yake mwenyewe ya Kings Music ambayo imeanza kuwasimamia wasanii wachanga.
Kiba yupo mbioni kuzindua kile kinywaji chake cha Mofaya ambacho tayari kimepata promo kubwa. Kwa jitihada zake hizo za kujiingizia mkwanja, Kiba anamiliki mjengo wa kifahari wa ghorofa moja uliopo Tabata na viwanja jijini Dar. Kwa upande wa usafiri, jamaa huyu anamiliki gari aina ya BMW X6 na magari mengine ya kawaida.

JUDITH WAMBURA ‘JIDE’
Jide au Lady Jaydee ni msanii mwenye heshima kubwa Tanzania. Kama ilivyo kwa kina Jay, Jide amefanya muziki wa Bongo Fleva na kujitwalia heshima kubwa na kujikuta akiogelea kwenye mafanikio. Jide kwa sasa amekuwa akifanya shoo chache akiwa na bendi yake ya Lady Jaydee and The Band, lakini zimekuwa zikimuingizia mkwanja mrefu kwani zimekuwa za watu f’lani wenye nazo na viingilio vikubwa.
Kwa uchapa kazi wake, Jide anamiliki vitu mbalimbali ikiwemo nyumba moja iliyopo Kimara-Temboni huku akiendelea na ujenzi wa mjengo wa kifahari maeneo ya Madale- Tegeta. Kwa upande wa magari, mwanadada huyu anamiliki Range Rover Evoque na magari mengine ya kawaida.

AMBWENE YESSAYA ‘AY’
Tofauti na wasanii wengine, AY huwa anapiga shoo za kimyakimya za ndani na nje ya nchi. Pia fedha anazoingiza zinatokana zaidi na biashara zake za nje ya muziki. AY ambaye aliwahi kuwa Balozi wa Bia ya Peroni ya Italia pia ni mwanzilishi mwenza wa Kipindi cha Mkasi kilichokuwa kikiendeshwa na Salama Jabir ambacho kinatajwa kumwingizia mkwanja mrefu.
AY ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Unity Entertainment inayojihusisha na kuandaa shoo, matangazo na kuleta Tanzania wasanii wa nje. Kwa muziki aliofanya jamaa huyo, kwa sasa anamiliki bonge la mjengo uliopo Calabasas huko Los Angeles nchini Marekani na kuna tetesi anajenga ghorofa maeneo ya Kigamboni jijini Dar. Kuhusu usafiri, AY anamiliki ndinga kali aina ya Range Rover Sport.

LUCAS MHUVILE ‘JOTI’
Mmoja wa wacheshaji wakali Bongo ni Joti. Jamaa huyu, kama ilivyokuwa kwa Masanja, baada ya kupita kwenye Kundi la Ze Comedy kisha Orijino Komedi, amekuwa akifanya vichekesho vya kujitegemea kupitia Joti TV ya mtandaoni na kujipatia mkwanja mrefu kutokana na kupendwa na wengi.
Mbali na kulamba mkwanja mtandaoni, Joti amekuwa akipata madili manono ya matangazo kama Tigo. Kwa mkwanja huo, Joti anamiliki nyumba kadhaa jijini Dar likiwemo ghorofa la kifahari lililopo Kigamboni huku akisukuma magari makali.

OMARY NYEMBO ‘OMMY DIMPOZ’
Kabla ya kusumbuliwa na ugonjwa wa koo kisha kufanyiwa operesheni mwaka huu, jamaa huyu alikuwa vizuri mno kwa shoo za ndani na nje.
Ommy amefanya ziara nyingi za kimuziki nchini Marekani na Ulaya. Mwaka jana, Ommy alithibitisha kuwa na kiasi cha shilingi milioni 400 kwenye akaunti benki. Huku akimiliki nyumba mbili ikiwemo moja iliyopo Mbezi- Beach na nyingine Kigamboni, Ommy alisema anamiliki viwanja viwili anavyotaka kuangusha mijengo mingine. Kwa upande wa usafiri, Ommy anamiliki ndinga aina ya Toyota Prado.

EMMANUEL ELIBARIKI ‘NAY’
Pamoja na kwamba Nay amekuwa akidai kufilisika, uchunguzi wa Ijumaa Wikienda ulibaini kwamba bado jamaa huyo ana utajiri wa kutisha.
Nay ni mmoja wa wasanii wanaopiga shoo nyingi za kimyakimya mikoani na nchi jirani. Mbali na muziki, Nay ana biashara nyingi zikiwemo saluni za kiume, bodaboda, Bajaj, daladala na usafiri wa Noah zinazotoa huduma nje kidogo ya jiji. Pia ana mashamba ya mpunga mkoani Morogoro ambapo huko pia ana mradi mkubwa wa ufugaji wa kuku wa kienyeji.
Kwa mkwanja huo anaoingiza, Nay anamiliki nyumba tatu mjini ikiwemo ile anayoishi ya Kimara, Dar. Pia Nay anamiliki magari ya aina mbalimbali yakiwemo Toyota Prado, Nissan Murano, Toyota Verossa, Toyota Noah na mengine ya kawaida.

Source: Global Publishers online.
NahIsi hii list anayekimbiza kwa uhakika ni AY, ni mtu mkimya ila hakuna anayekataa kuwa ni the most successful
 
Hapo kigogo Diamond,Sugu,Jay,Masanja,Joti na Ney ila wengine ni kawaida tu.,,,,,,,Jay D tangia miaka hiyo anamiliki Envoque na nyumba kimara sijasikia kaongeza kingine.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom