illegal migrant
JF-Expert Member
- Oct 18, 2013
- 1,277
- 1,121
Kama mtu umeamua kuwa msanii ni vyema ukajua mipaka yako ukweli ni kwamba wasanii wana wafuasi wengi hivyo ni rahisi kwao kuleta hamasa kwa jamii na kwa kila rika, ndiyo maana huwa wanatumika kwenye kampeni ili kuvutia wafuasi, sasa inapotokea msanii unanunuliwa kwa sababu tu unawashabiki wengi ndipo unapokaribisha matatizo, vivyo hivyo kwa waandishi wa habari mtu anahongwa ili amchafue mtu fulani bila kujali habari zake zina wafikia wananchi wangapi, sasa hivi naona sanaa yetu ikipotea kisa ni kila mwenye jina kujiingiza kwenye siasa ama kwa kuamini atahama na wafuasi wake aliokuwa nao kwenye mziki ama kwa kutumiwa kwa malipo ili afikishe ujumbe potofu na chochezi....bila kujali taharuki na chuki atakayoijenga kwa wananchi. Huwezi ukawa mwanamuziki halafu unafanya kazi za kiunaharakati just be ready to face the music as well, chagua moja sanaa ama siasa.