Wasanii Tanzania,Hii Ndiyo Maana Yenu Ya Comedy?

Naisujaki Lekangai

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
1,340
1,377
Mimi napenda sana mizaha, ucheshi na kucheka ili kuniondolea stress za maisha.Hapa jf jukwaa la utani udaku na gossip nalitembelea sana ili kujifurahisha.Pia kwenye tv zetu ikitangazwa kwamba kuna kipindi cha comedy lazima nikitazame.

Bahati mbaya sana comedy za kwenye tv hapa tz si comedy zenye maana ya comedy - ni kitu kingine kabisa.Kwenye comedy ya kweli lazima mtu utabasamu na kucheka sana kwa mizaha na matani ya wahusika - misemo na maneno ya kuchekesha nk. Lakini comedy za hapa tz ni wahusika kufokeana, kukimbizana na kukatana mtama na magumi juu! Eti hiyo ni comedy! Mtu mzima (mimi) sicheki nikiona watu wakifokeana kukimbizana na kukatana mtama kushikana mashati.Hiyo inawachekesha watoto zaidi.

Kuna kituo kimoja cha tv mwanza kila alhamisi saa 3.30 usiku wanaonesha huo upuuzi wa kufukuzana na kukatana mtama na kuita eti ni comedy! Rimoti yangu imechakaa kwa ajili yao.Hata hiyo iitwayo ze komedi ya EATV ni sarakasi hizohizo, si comedy.

Enyi wasanii wa comedy tanzania chunguzeni vizuri maana ya comedy ili mfanye vitu vya komedi kweli mbali na kufokeana, kushikana mashati nk.
Hii ni wazi kabisa kwamba kama komedi ya kikundi mnachemsha hata standup comedy itakuwa shida.
 
Sure unachosema lakin pia unakosea maana kuna watu m nawawelewa kama vile joti, kuna watu comedy yao ni kwny maneno na hyo ndo comedy za nchi nyingne. Mtu kama mpoki, mc pilipili kuna hawa jamaa Mambo na vijambo wako vema pia. Shughuli hawa wenzangu walobaki watumia nguvu nyingi
 
Hii ni wazi kabisa kwanamba kama komedi ya kikundi mnachemsha hata standup comedy itakuwa shida.
Au MTU anavaa kiatu usawa Wa panga suruali au shati kuubwa na mawani...hasa hao Wa E.Africa...huyo anayeongeaga kichaga ni aibu yaan hapan MTU badala ucheke unasonya
 
Mimi huwa namaliza bando kwa kumcheki teacher mpamire na MCA treak baaas za bongo tupa kapuni
MCA tricky na teacher mpamire hao ni standup comedy. Comedy za hapa tz ni za kikundi(ensemble comedy) ambazo kwangu ni sifuri tupu.Sijaona standup comedy hapa tz, wanaojaribu wako chini ya kiwango.
 
Unazungumzia Stand up comedy au siyo? Wapo kama kina Mc pilipili.
Hapana Amalinze, nazungumzia comedy za kikundi kama futuhi, mizengwe,nk.Hawa hawafanyi comedy ila ni ujuha mtupu! Standup comedy ni kitu kingine kabisa na hapa tz hakuna standup comedy yenye viwango vinavyostahili kuitwa standup comedy
 
Mm nimehamia YouTube mkuu....Kuna Nigeria akina marc angel comedy nawakubal sana......wabongo wanaihiza saut maneno mengi.......zaid naingia kwa katuni za Disney animation hapo ndipo palipo utamu.
 
Sure unachosema lakin pia unakosea maana kuna watu m nawawelewa kama vile joti, kuna watu comedy yao ni kwny maneno na hyo ndo comedy za nchi nyingne. Mtu kama mpoki, mc pilipili kuna hawa jamaa Mambo na vijambo wako vema pia. Shughuli hawa wenzangu walobaki watumia nguvu nyingi
Hapo umenena.Comedy ni maneno yenye kuvutia na kuchekesha.Kwa muktadha huo Mpoki na maneno yake aweza kuwa standup comedian mzuri sana hapa tanzania.Lakini siyo Joti.Huyu amejiharibia kwa kuigiza taswira za kike - haichekeshi ila inaudhi!
Halafu mimi sidhani mambo na vijambo yaweza kuingizwa kwenye tasnia ya comedy!Kipindi hicho kinachooneshwa EATV kila jumapili saa 12.30 jioni kwangu ni igizo tu lisilo na mwelekeo wowote labda sanasana kuonya juu ya tabia za watu.
 
Mm nimehamia YouTube mkuu....Kuna Nigeria akina marc angel comedy nawakubal sana......wabongo wanaihiza saut maneno mengi.......zaid naingia kwa katuni za Disney animation hapo ndipo palipo utamu.
Unazungumzia standup comedy mkuu! Kiboko ya standup comedy ni........... achana na hao matapeli wa nigeria....... kiboko ni Trevor Noah mkuu! Ulishamcheki huyu mtu lakini? Ni balaa kwenye standup comedy!
 
Standup comedy kuna hawa wakenya kwenye Churchill show akina omond akina processor nk
 
Lakini comedy za hapa tz ni wahusika kufokeana, kukimbizana na kukatana mtama na magumi juu! Eti hiyo ni comedy! Mtu mzima (mimi) sicheki nikiona watu wakifokeana kukimbizana na kukatana mtama kushikana mashati.Hiyo inawachekesha watoto zaidi.
Kwa kuanza fuatilia hizi comedy Youtube:
- SIO HABARI
- JAMBO NA VIJAMBO
- TIMAMU TV
- JOTI TV
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom