Wasanii Profesa J na Mzee Yusufu kugombea ubunge jijini Mwanza

nyampanaga

JF-Expert Member
Nov 16, 2012
346
195
Wakuu wa Fikra, heshima kwenu

Nime inasa hii katika pitapita zangu.Chanzo ni ufa wa mahusiano kati ya wafanya biashara ndogo ndogo(wamachinga) ambao ndiyo wapiga kura wengi na uongozi wa jiji la Mwanza umekuwa ukiongezeka kila kukicha na kufifisha matumaini ya kurirejesha jiji la Mwanza kuwa ngome ya ccm.

Kete ya kuchomeka mameya wa kichina imeonyesha kutokuzaa matunda kwani wakazi wengi jijini Mwanza wameonyesha hasira za wazi kama walivyokaririwa na badhi ya radio za jijini hapa.. na kuashiria kuwepo upigwaji wa kura za hasira tena dhidi ya ccm hapo 2015.

Mkakati uliopo sasa ni kutafuta watu wenye umaarufu wao binafsi na unaokubaliwa na jamii ili iwe rahisi kuwa nadi na wasanii hao ndiyo wanofikiriwa.mmoja atagombea Jimbo la Ilemela na mwingine Nyamagana.Yote hii nikuhakikisha jiji haliwi chini ya wabunge wa upinzani hasa cdm kama ilivyo kwa sasa.

Naendelea kufuatilia kwa karibu undani wa tetesi hizi, nitawajuzeni...ila chanzo changu kimedokeza kuwa baada ya sikuuku ya mwaka mpya 2013, watakuwa wakifanya show za mara kwa mara jijini Mwanza chini ya udhamini wa kigogo mmoja wa NEC-CCM(Jina kapuni kwanza)

Nawasilisha.
 
nyampanaga

JF-Expert Member
Nov 16, 2012
346
195
sugu kafungua njia, kama yeye alipata basi hata afande sele atagombea. Heshima ya bunge ilipotea alipo ingia wenje,mdee na sugu.
Majebere acha kuvuruga mjadala hapa tunawajadili Profesa J na Mzee Yusuf..sasa hawa unawaingiza vipi! Kwanza nikuulize kweli mnaelekea kuishiwa mbinu kiasi hiki? basi huenda hata ya Mch. Mwakasyege kule Arusha ikawa ni kweli, ngoja tusubiri hukumu ya Lema, tujue mbivu na mbichi.
 
luhombi

Member
Oct 17, 2012
85
0
umaarufu si kigezo pekee cha kumfanya mtu ashinde uchaguzi, wakumbuke kala pina aligombea udiwani kule kinondoni na akashindwa licha ya umaarufu wake
 
kimboka one

JF-Expert Member
Jan 23, 2010
734
170
ubunge umekosa heshima kweli.na bi kidude apewe jib8 lolote jamani, huyu bibi anakubalika sana mbagala cdm mwandaeni!
 
kiwatengu

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
15,245
2,000
Mzee Yusuful ndyo yupi huyo? Hawa wazee zamu hii hatutawapigia kura hata kidogo..michango yao bungeni ni hasi! inshort they are outdated, let them go away from politics! waende wakatoe ushauri huko mashambani kilimo kikue..
 
C.T.U

JF-Expert Member
Jun 1, 2011
4,802
2,000
Majebere acha kuvuruga mjadala hapa tunawajadili Profesa J na Mzee Yusuf..sasa hawa unawaingiza vipi! Kwanza nikuulize kweli mnaelekea kuishiwa mbinu kiasi hiki? basi huenda hata ya Mch. Mwakasyege kule Arusha ikawa ni kweli, ngoja tusubiri hukumu ya Lema, tujue mbivu na mbichi.
JF inajadili hoja sio watu
 
Kimweli

JF-Expert Member
Oct 4, 2011
899
225
Hahahaha, kumbe professor J ni CCM naenda kufuta nyimbo zake kwenye computer yangu na kuchoma cd na kada zake zote. Huu ni mwendelezo wangu wa chuki kwa hawa wasafirisha pembe za ndovu.
 
Angel Msoffe

JF-Expert Member
Jun 21, 2011
6,790
1,225
Leo mi nacheka tu,Yn umekaa umejitungia mambo yk unatuletea umbea tujadili....Kwa wale wote wenye muda wa mchezo endeleeni na mjadala
 
nyampanaga

JF-Expert Member
Nov 16, 2012
346
195
Leo mi nacheka tu,Yn umekaa umejitungia mambo yk unatuletea umbea tujadili....Kwa wale wote wenye muda wa mchezo endeleeni na mjadala
Kama wewe ni mfuasi wa late Shekhe Yahaya kiasi cha kujua kuwa nimekaa na kujitungia basi hongera zako..otherwise waweza ni imbox nikutiririkie zaidi.
 
Baba V

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
19,500
2,000
Wakuu wa Fikra, heshima kwenu

Nime inasa hii katika pitapita zangu.Chanzo ni ufa wa mahusiano kati ya wafanya biashara ndogo ndogo(wamachinga) ambao ndiyo wapiga kura wengi na uongozi wa jiji la Mwanza umekuwa ukiongezeka kila kukicha na kufifisha matumaini ya kurirejesha jiji la Mwanza kuwa ngome ya ccm.

Kete ya kuchomeka mameya wa kichina imeonyesha kutokuzaa matunda kwani wakazi wengi jijini Mwanza wameonyesha hasira za wazi kama walivyokaririwa na badhi ya radio za jijini hapa.. na kuashiria kuwepo upigwaji wa kura za hasira tena dhidi ya ccm hapo 2015.

Mkakati uliopo sasa ni kutafuta watu wenye umaarufu wao binafsi na unaokubaliwa na jamii ili iwe rahisi kuwa nadi na wasanii hao ndiyo wanofikiriwa.mmoja atagombea Jimbo la Ilemela na mwingine Nyamagana.Yote hii nikuhakikisha jiji haliwi chini ya wabunge wa upinzani hasa cdm kama ilivyo kwa sasa.

Naendelea kufuatilia kwa karibu undani wa tetesi hizi, nitawajuzeni...ila chanzo changu kimedokeza kuwa baada ya sikuuku ya mwaka mpya 2016, watakuwa wakifanya show za mara kwa mara jijini Mwanza chini ya udhamini wa kigogo mmoja wa NEC-CCM(Jina kapuni kwanza)

Nawasilisha.
baada ya mwaka mpya 2016!!!!???, ili wagombee 2020 au!??
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom