Wasanii nyimbo za Injili kujichubua, tujifunze nini?

Mzalendo_Mkweli

JF-Expert Member
Jan 30, 2012
1,579
2,000
HAKUNA jambo ambalo linanikera kama mtu anapobadili rangi ya ngozi yake, kwani hivi sasa imeshakuwa fasheni si tu kwa wanawake, bali hata kwa wanaume na mbaya zaidi, jinamizi hilo limehamia hadi kwa waimbaji wa nyimbo za Injili na wachungaji wao.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, nilibahatika kutazama moja ya kazi ya msanii wa nyimbo za Injili ambaye ukweli ni kwamba awali alikuwa akinigusa sana kutokana na sauti yake nzito ya asili, sambamba na ujumbe anaoutoa.
Sitamtaja jina mwimbaji huyo, lakini ukweli ni kwamba hivi sasa hata upako wake umeshuka, amepoteza mvuto, kwani tangu nimeanza kumfahamu ni takriban miaka 10 imepita, lakini kadiri siku zinavyozidi kwenda, ninaona mashiko aliyo nayo na heshima ninayompa inazidi kushuka na ninaelekea kumdharau kutokana na mabadiliko aliyo nayo.
Wakati ninaanza kumfahamu, alikuwa ni binti mweusi mzuri aliyevutia, lakini hivi sasa amekuwa kama ‘nguruwe' aliyetoroka kwao na kuanza kuzurura majalalani.
Ninasema haya kwa sababu msanii huyu amejichubua kiasi cha kutisha, kupoteza mvuto alionao na kuniachia maswali, je ni nani aliyemdanganya kwa jinsi alivyo, hata shetani hawezi kufanya kama yeye. Lakini pia nilijiuliza, ina maana hafahamu madhara ya kiafya yatokanayo na kujichubua?
Je, ni kweli tunayemuabudu anapendezwa na hali hii ambayo inamfanya mtu abadilike hadi afanane na kinyago?
Hakika, hata Mungu anasikitika juu ya hilo, lakini anaanzaje kusema naye wakati alionywa mara nyingi na njia mbalimbali akajitoa ufahamu wa kiroho, akashupaza shingo matokeo yake imevunjika; sasa amebakia kuwa mwimbaji wa nyimbo za Injili kwa mazoea.
Na je, kuwa na rangi tofauti tofauti, uso mweupe, miguu mieusi, mkono rangi ya mbao ndiyo kukamilisha usanii?
Awali, tulishazoea kuona raia kutoka nchi fulani (ninawahifadhi), ndiyo wenye hiyo tabia ya kubadili rangi ya ngozi zao, lakini hivi sasa ninasikitika kuona hata watumishi wa Mungu wanaoheshimika, wanaoelekeza roho za watu kwenda mbinguni wakiwa mstari wa mbele katika kujichubua kulikopitiliza.
Tena cha kusikitisha ni kwamba, wengine ni watu wazima, je mnafundisha nini waumini au wapenzi wa nyimbo zenu? Mnaweza kusema fuata maneno yangu msifuate matendo? La hasha, hilo silikubali kamwe kwa sababu hata maandiko matakatifu yanatueleza kwamba, mtumishi uwe mchungaji, Mwinjilisti, mwalimu au mwimbaji, imani bila matendo ni sawa na bure.
Tukiachana na hayo, mimi bado niko na wasanii hasa waimbaji wa nyimbo za Injili, je, ndiyo maisha waliyoyachagua?
Bado ninaugua kwa ajili yenu, kwa sababu muda mwingi mnautumia katika kuhangaikia ya mwilini ambayo siyo kazi mliyotumwa kuifanya duniani, au na ninyi mtuambie kama ni magugu mlio ndani ya ngano?
Kwa upeo wangu mdogo, ninachofahamu ni kwamba, kila jambo linatakiwa kufanyika kwa utaratibu na maadili yanayoendana, ili tunaopokea ujumbe tusiwe na maswali, ingawa nia yangu si kusema kwamba, ati ukiwa msanii wa aina yoyote ile uwe mchafu; hapana! Hatuendi hivyo.
Hivi sasa si kwa waimbaji tu, bali hata watumishi wa Mungu wahubiri, pia wameingia katika meli hiyo mbovu ya kujichubua kupita kawaida, kuvaa nguo za ajabu zilizokosa staha, kujiremba kulikopitiliza hadi mnaogopesha, jambo ambalo linanisikitisha na kujiuliza, hivi kwani mkibakia kuwa na rangi za asili mtameguka? Mnaona ufahari gani?
Hizo gharama mnazotumia si afadhali msaidie wasiojiweza kuliko kutafuta urembo unaowafanya muonekane kama makahaba na mashangingi yaliyoshindikana duniani!?
Hata mimi pia nina mapungufu yangu, lakini kwa kutumia kalamu yangu ninapenda niseme kwamba angalieni mlipoangukia mkatubu, tambueni Mungu hapendezwi na hilo. Timizeni wajibu wenu, toeni huduma katika misingi inayotakiwa, kila jambo lina kiasi.
Ni mtazamo wangu kuwa ninyi ni mabalozi wa muziki wa Injili duniani na lengo ni kuhubiri kwa njia ya uimbaji na kuponya roho za watu, hivyo yafaa mtambue wajibu wenu na muwe mfano wa kuigwa.

Source: http://www.freemedia.co.tz/daima/wasanii-nyimbo-za-injili-kujichubua-tujifunze-nini/
 
  • Thanks
Reactions: prs

NullPointer

JF-Expert Member
Feb 7, 2011
3,467
2,000
Hakuna cha kuokoka kiroho wala kimwili, hata wanayoimba yenyewe wanaimba tamaa tu, ohh utaponywa hiki ohh hiki, hata wachungaji wao ndicho wanachohubiri, ku-convice watu kumfata Yesu sababu ya kupata hela au kutibiwa ugonjwa flani, sio sababu ya upendo... Nuksi tu, dini imechakachuliwa
 

yutong

JF-Expert Member
Apr 15, 2011
1,602
0
Kweli hata mimi linanikera sana hilo jambo! Si kujichubua tu, ni mambo mengi wanafanya maana hata mavazi wanayovaa pia ni tabu. wengi wao wanaimba ili kupata pesa tu maana hata style wanayoimbia ni ya mziki wa bongo flavor. Wengi wamejaa siku hizi kila leo tamasha tu sijui tutafika kweli
 

Okhondima

JF-Expert Member
Jul 10, 2013
1,114
1,500

Before

After

"Nlikuwepo":bolt:
 

AlP0L0

JF-Expert Member
Apr 23, 2011
5,073
2,000
Hakuna cha kuokoka kiroho wala kimwili, hata wanayoimba yenyewe wanaimba tamaa tu, ohh utaponywa hiki ohh hiki, hata wachungaji wao ndicho wanachohubiri, ku-convice watu kumfata Yesu sababu ya kupata hela au kutibiwa ugonjwa flani, sio sababu ya upendo... [Bcolor=red]Nuksi tu, dini imechakachuliwa

[/color]
DINI IMECHAKACHULIWA! YESU HAKUWA MUIMBAJI WALA MCHEZA NGOMA KANISANI
 

oel200e

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
276
225
Kusema ukweli hili jambo limenisikitisha....lakini karne hii kila kitu kinawezekana....watu wa injili wamezama sana kwenye umaridadi wa mwili,si jambo baya kuvaa vizuri au kutembelea gari zuri,lakini kwa mtu unayehubiri kuwaokoa watu lazima ukubali mabadiliko ya kiroho,kiuchumi na kadhalika kwa kondoo wako kwanza......tumkumbuke nyerere na Nelson mandela...watu kwanza,Mali na uzuri baadae....after all mshahara si mbinguni? (hata wahubiri wenyewe wanasema hivyo)...haraka ya nini hapa duniani?
 

tata mvoni

JF-Expert Member
Jan 14, 2011
535
195
Si mwasema wakristo mko kiroho,hamko kimwili,hata mtu akivaa nguo za uchi kwenu,mwasema in sawa,lakini kuwa kiroho kuliko kimwili hamtembei name chupi .

Ni utetezi mbaya sana wanaoutumia na madhara yake yameanza kuonekana mtu yuko uchi afu anakwambia nimeokoka kiroho sasa mh!?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom