Wasanii na Wanamuziki wengi kugombea Uraisi nchi za Afrika je wasomi na wataalamu wamekata tamaa au nini?

Hujui kuwa kuna watu tuliamini ni wasomi kwa sababu wamefundisha kemia hadi shule za upili lakini bure kabisa?
Hujui kuwa kuna watu wamehitimu digrii ya kwanza, ya pili na ya tatu aka PhD na kumbe ni bure kabisa?
Hujui pia kuwa wapo wenye sifa nilizotaja hapo juu wakaongezea na uzoefu wa miaka 20 ya ubunge/uwaziri lakini walipopewa kazi hiyo ni bora hata angepewa Sugu mwenye uzoefu wa Hip hop na ubunge miaka 10 pekee?
Acheni jamani, kuna watu na viatu!
 
Kila msanii anaweza kuwa msomi lakini siyo kila msomi anaweza kuwa msanii,hii ni kwa sababu elimu unaipota darasani lakini usanii unazaliwa nao na unakwenda kusomea sanaa kama sehemu ya kuongezea nyenzo za sanaa yako.
Ipo hivi,mtu kuwa msanii haimaanishi kuwa siyo msami landa kama tu ulikuwa ufahamu ipo hivi,Mwalimu Nyerer alikuw ana kipaji cha sanaa ya uandishi wa mashairi na leo ni mtu muhimu katika bara la Afrika,meya wa kwanza muafrika Kaluta Abeidi alikuwa na kipawa cha kuandika mashairi lakini alivunja rekodi kubwa ya uongozi Tanganyika na hata Afrika.
Kaa uelewa kuwa uongozi siyo elimu,uongozi ni kipawa kingine,hata usomi mpaka mwalimu akimbie na ubao kama hauna kipawa cha kuwea kiongozi hata upewe uongozi wa ubalozi wa nyumba kumi utafeli kuongoza
Heshimu sanaa acha kukariri maisha.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom