Wasanii na Waandishi wa Habari watema Big G kwa karanga za kuonjeshwa

Kichakoro

JF-Expert Member
Sep 10, 2008
3,061
5,393
Leo sikuwa nataka kuandika chochote lakini baada ya kusikiliza wimbo wa AllY Kiba hasa kipande chenye maneno "WATEMA BIG G KWA KARANGA ZA KUONJESHWA"

Nimetafakari sana sana nikakumbuka visa vichache sana. Hapo nyuma wasanii walinyimwa kufanya shows mbali mbali kwa sababu mbali mbali zilizotolewa na viongozi wetu. Nakumbuka wasanii wengi walijiapiza kutokuirudisha hii Serikali. kuna wengine hadi leo hawana tena show including live band maana bar lazima zifungwe saa sita usiku.
Uchaguzi umekuja wameonyeshwa karanga wamejisahau wametema BIG G

Wakati wa Azory na Kabendera waaandishi walisema maneno meeeengi na kujiapiza kama wasanii, leo nao wameonjeshwa karanga wametema big G

wafanyakazi lilipokuja suala la kikokotoleo na ongezeko la mishahara walilia sana walipotoka MAY MOSI walisonya sana kwa kutokuongezewa mishahara au baba kutotoa tamko la ongezeko la mishashahara, leo wamepewa karanga za kuonjeshwa WAMETEMA BIG G List ni ndefu

USHAURI WANGU:

Katika maisha ukishaamua kufanya jambo fulani ambalo hapo awali lilikua kikwazo na ukajiapiza kulifanya basi fanya usiwe na ndimi mbii maana hata Mungu hapendi.
 
Back
Top Bottom