Mh Lissu kushambuliwa: Celebrities wa Kitanzania wanasemaje?

M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
13,203
23,020
Je, kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii wasanii na watu wengine maarufu wanatoa kauli gani kuhusu Mh Tundu Lissu kushambuliwa na risasi jana?

Uzi huu umeanzishwa specially kwa ajili ya kufuatilia kauli za watu wa jinsi hiyo - tutiririke watu wa Mungu!

Ninaanza hapa chini na nukuu kutoka kwa baadhi ya wanasoka maarufu hapa nchini (Gazeti la Mwananchi leo).

Wachezaji watumia mitandao ya kijamii kumtakia afya njema Lissu.

By Fredrick Nwaka, Mwananchi; fnwaka@mwananchi.co.tz
Dar es Salaam.

Tukio la kupigwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu limewagusa wachezaji mbalimbali.

Wachezaji hao wamekuwa wakutumia akaunti zao za mitandao ya kijamii kumtakia kheri mbunge huyo.

Mbwana Samatta katika ukurasa wake wa Instagram ameeleza mshtuko wake baada ya tukio hilo.

"Hili ni tukio baya, tumuombee mheshimiwa Lissu," ameandika nahodha huyo wa Taifa Stars anayeichezea Genk ya Ubelgiji.

Mshambuliaji wa Simba, Shiza Kichuya aliweka picha ya Lissu kwenye ukurasa wake wa Instagram na kusema anamuomba Mungu ampe nafuu Tundu Lissu.

Mchezaji mwingine aliyeweka picha ya Lissu kwenye ukurasa wake ni kipa wa Simba, Aishi Manula.

Kwa sasa Lissu yuko Nairobi nchini Kenya anakopatiwa matibabu katika Hospitali ya Aga Khan
 
Celebrity Mange kimambi kamtakia heri na pia apone haraka mheshimiwa Lissu..kaonyesha kuguswa sana na tukio hilo,pia kawatusi waliohusika moja kwa moja na kujaribu kumuua Lissu wetu....


Hongera kwa uthubutu celebrities wote maana wengine wameogopa kukomenti kwasababu ya woga....
 
Celebrity Mange kimambi kamtakia heri na pia apone haraka mheshimiwa Lissu..kaonyesha kuguswa sana na tukio hilo,pia kawatusi waliohusika moja kwa moja na kujaribu kumuua Lissu wetu....


Hongera kwa uthubutu celebrities wote maana wengine wameogopa kukomenti kwasababu ya woga....
HUYU YUPO MBALI NA MUNGU SANA...ATAMTIA NUKSI NA NAJISI....
 
Bongo movie kiboko wanapiga hadi selfie huku wanatoa machozi na kusikitika

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hili swala kila mtu limemgusa yani...ni asilimia kubwa sana ya watu wamelia na watu mtaani hawana amani...
Nimeamkia magazetini leo watu hawana amani kabisa vijiweni...
Wazee wamelaani sana hili tukio kwakweli.....
Mungu azidi kumpa afya Lissu
 
Labda bongo flava hao bongo movie wapo mfukoni tayari wanasubiri posho zao kuzunguka nchi nzima kumnadi sizonje
 
Karibia wote wameguswa,kila mmoja ukitembelea page yake Instagram utaona...
Diamond
Nikki wa pili
Kala Jeremiah
Joh Makini
Roma
Faiza Ally
Vanessa
Nikki mbishi
....
....
....
List ni ndefu

Naipenda JF
 
Jana nchi ilizizima baada ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kushambuliwa kwa risasi zinazoelezwa kuwa 32 mjini Dodoma.
Mazungumzo katika mitandao yalichukuliwa na tukio hilo kila mmoja akiomwombea mbunge huyo baada ya risasi tano kuingia katika maeneo mbalimbali ya mwili wake.


Watu maarufu hawakubaki nyuma kuelezea hisia zao kwa tukio hilo na hivi ndivyo baadhi yao walivyoandika katika mtandao wa Instagram wakiambatanisha na picha yake.


Shilole: Hatma ya maisha mtu yeyote anayo Mungu na si mwanadamu. Mungu mwenye kutoa uhai na uzima akupe nafuu mkuu. Watanzania tumeguswa na naamini una maombi ya wengi sana.


Aunty Ezekiel: Dah!Nakosa la kuongea mwenyezi Mungu tenda miujiza yako.


JB: Naamini Mungu atakuponya na utarudi katika afya yako...Tunakuombea..Mungu atafanya.


Diamond: InshaAllah mwenyezi Mungu akusmamie na kukurudishia afya njema


Irene Uwoya: May you get a quick recovery honourable in God's power....My prayers are with you!!Amen


Idris: At This point tupunguze uchama kuhakikisha Tundu Lissu anakuwa stable, baada ya hapo tutajua nchi imekuwa ya namna gani.


Benpol: Pray for Tundu Lissu

Roma: God. Amen

Jux: [HASHTAG]#Prayfortundulissu[/HASHTAG]


Lulu: Tuweke pembeni tofauti ya vyama na maono ya kisiasa...kwa sasa kwa imani/dini zetu tumuombee kama mtoto wa mama na baba fulani, mume wa mama fulani, baba mwenye watoto, familia na watu mbalimbali wanaotemgemea. Tusimuombee Tundu Lissu mbunge au mwanasiasa, tumuombee Tundu Lissu wa kawaida kabisa kama baba yetu, kaka yetu au mtu yeyote wa kawaida tunayemjua.


Lady Jay Dee: Mwenyezi Mungu aliyekuumba akakuinue kutoka kwenye kitanda walichokulaza binadamu tusiowafamu. Huwa tunaamini kwa jina la baba, la mwana na la roho mtakatifu.


Mpekuzi
 
Kuna wachezaji wa mpira pia wametoa pole zao kama Samatta, Kichuya n.k Alikiba hajatoa pole?
 
Back
Top Bottom