Wasanii na Bendi za Muziki Tanzania hivi mnajua kuwa kufagilia watu kwa kutaja majina yao ni kitega uchumi cha Bendi nyingi za Congo DR?

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Nilihudhuria live band moja hapa mkoani Dar es Salaam siku si nyingi na kilichotokea kilinisikitisha sana na kuamini kuwa bendi za Tanzania bado sana Kushindana na za Congo DR na Congo Brazzaville.

Wakati bendi inapiga na watu tunaserebuka kwa sebene akaja mmoja wa marapa jirani yangu na kumwambia naomba anifagilie kwa kunitaja Pedeshee MINOCYCLINE nakati ya Pemba na kuna pia zake tatu kaunta kweli akafanya hivyo hivyo huku nikimcheka mno moyoni na kumuona bonge la juha.

Leo natoa elimu ya bure kuwa moja ya sababu ya ama bendi au wanamuziki wengi wa Congo Kinshasa na Congo Brazzaville kuwa matajiri ni huu ubunifu wa kutaja majina (kufagilia watu) katika nyimbo za kurekodi au zile za ukumbini (live shows)

Ni kwamba ukiusikia wimbo wowote mpya na uliobeba album anatajwa mtu mwanzoni jua ameshatoa dola za Marekani 5000 bila hiyana.

Ukisikia mtu anatajwa katikati ya wimbo uliobeba album jua ameshatoa dola za Marekani 2500 bila hofu.

Na ukisikia mtu anatajwa (anafagiliwa) wimbo uliobeba album ukiwa unaelekea mwisho jua hapo amelipia dola za Marekani 1000 bila mjadala.

Na ukiwa unayasikia majina mengine yanachomekewa ndani ya wimbo uliobeba album jua hao wote wamelipia dola za Marekani 100 kwa raha zao.

Sasa nauliza wakitajwa watu wa kwanza hao watatu wa dola 5000, dola 2500, dola 1000 na watu 25 wa kuchomekewa majina yao kwa malipo ya dola 100 kwa kila mmoja jumla yake atakuwa kapata shilingi ngapi za Kitanzania?

Na ndiyo maana mnawaona wanamuziki wa Congo Kinshasa na Congo Brazzaville akina Koffi Olomide, JB Mpiana, Ngiama Makanda Werrason, Felix Wazekwa, Marehemu Madilu System na akina Fally Ipupa na Ferre Gola wanamiliki mahekalu (Mansions) huko kwao na kumiliki magari ya kifahari karibu matano hadi saba majumbani mwao huku pia wakiwa wamewekeza mno katika ujasiriamali wa vitu mbalimbali.

Haya bendi za dansi za Tanzania hebu nanyi badilikeni na muwaige hawa wenzenu ambao hufagilia (hutaja) majina ya watu kwa malipo na achaneni na hii tabia ya Kufagilia watu katika nyimbo zenu kwa ahadi za bia au mvinyo na kuna wengine hadi mnahaidiwa kutafutiwa mademu Ili mkawabandue kwa ahadi ya nyie kuwataja (kufagiliwa) katika nyimbo.
 
Hili ni kweli kabisa, Wacongo hua wanapiga hela ndefu kutaja majina,
Wanamuziki Wacongo ni matajiri sana ndio maana familia zao zinaishi ulaya, mwanamziki Koffi Olomide kwake kuna petrol station kabisa akitoka na gari yoyote anaweka mafuta kwake,
 
Hamia Congo mkuu ukalipe dola 5000, maana kutoa bia 3 imekusikitisha sana.
 
Apo umesema kweli bwana mkubwa nyimbo za uku Congo lwazima utakuta majina za watu :

-Ahmed Bakayoko
-Didier Drogba
-abd'achour
-samuel eto'o
 
Waambie waimbe vizuri , waloge sana shooting kali, na wawekeze kwenye promotion tuu
 
Tafuta pesa acha kunywa pombe bar za vichochoroni, hizo sio band ni vikundi vya ngoma, halafu itakua una sifa za kitoto na ushamba mwingi sana unaenda bar unaomba kutajwa jina 😂😅
 
Rayvanny angezaliwa Congo walahi angepiga hela ndefu kutoka kwa wimbo wake wa " Natafuta Kiki"

Humo jamaa kataja watu Kama wote Yaani.
 
Back
Top Bottom