Wasanii kushtakiwa na kufungwa: Baada ya TID je atafuatia Sir Nature?

Kama unapenda ku-scratch ovyo ujue jela inakuita! Be careful! Kwani lazima ? Usipofanya utakufa?
Tafuta mtu mzima mwenzio kama huwezi kujizuia.

womenofsubstance,

inabidi tujitolee muda wetu kufanya elimu ya sheria hii kwa watoto wa shule hasa za msingi. Make hawa watoto wakijua haki zao basi tutakuwa tumezuia" kina maumba" kurudi katika jamii yetu.

Yes we can....tunaweza kujenga jamii safi na yenye kutii sheria...nikuwafanya watoto kuwa pro-prosecution like. Zamani mtoto alikuwa wa jamii, kiasi jirani akiona kitendo kichafu anakivalia njuga hata mpaka polisi...siku hizi lililobaki ni kuwaonyesha mwanga hawa watoto under 18.
 
Nature ni mwana mtandao hivyo si rahisi kufungwa na akifungwa tu atapata presidential msamaha. maana wanamtandao wote wako juu ya sheria za nchi hii. Subiri uje uone!
 
Huyu jamaa si kaoa juzi juzi hapa tuliskia sasa kwenda kwa kisichana kidogo hicho nini kimemponza tena?Duh am kweli njaa za penzi zitawamaliza wasanii.
Nasikia kamla mtungo "mtoto wa Mama sitta" na jamaa mwingine.Kavuta jiko kweli majuzi lakini unajua hivi "vi underground" mkuu vinajipitisha pitsha kama weipa na kuviachia huwezi.
TID alifanya uzembe kesi yake akala mvua,nature awe makini
 
Mlalamikaji katika kesi hii ni nani? Je wazee wa binti huyo ndio wamemshitaki Nature au Republic? Ukishajua majibu ya maswali hayo then unaweza kujua wapi kwa kuanzia kutegua kitendawili!!
 
Mlalamikaji katika kesi hii ni nani? Je wazee wa binti huyo ndio wamemshitaki Nature au Republic? Ukishajua majibu ya maswali hayo then unaweza kujua wapi kwa kuanzia kutegua kitendawili!!

It will be R VS Juma ............... a.k.a nature"
Mtendewa kitendo/mlalamikaji ni shahidi wa kwanza tu.Hata wazazi wake hawana usemi hapa kam ani kufuata sheria strictly.
 
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Temeke , ilisheheni umati wa watu, wakiwemo wazazi wa Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya ( Bongo fleva) jijini Dar es Salaam, Juma Kassim Nature, (28) akikabiliwa na tuhuma za kumbaka Mwanafunzi wa Kidato cha tatu (16) kwa zamu. Tuhuma hiyo, inamuhusisha pia Godwine Malima (26), ambaye ni Mwalimu anayekabiliwa na tuhuma za kumbaka mwanafunzi huyo na kumchukua kwenda kuishi naye kinyume na ridhaa ya wazazi. Aidha Mwendesha Mshtaka, Mrakibu wa Polisi Basill Pandisha, alisema kuwa washtakiwa hao, walitenda kosa hilo mnamo Novemba 1 mwaka huu eneo la Sugar Rays, jijini Dar es Salaam, na kudai kuwa, mtuhumiwa namba moja ambaye ni Juma Kassim alimbaka mwanafunzi huyo bila ya ridhaa yake, huku akijua kufanya hivyo ni kosa kisheria. Ilidaiwa katika maelezo ya malalamikaji kuwa, mnamo majira ya saa 1:40 usiku maeneo ya Sugar Rays, mlalamikaji alikuwa ameenda kwa mtuhumiwa kwa lengo la kuzungumza naye, kwani wiki mbili zilizopita mtuhumiwa alikuwa akimsumbua kupitia namba yake ya simu. Ilielezwa kuwa, mlalamikaji alipofika nyumbani kwake alimkuta rafiki yake Godwine Malima ambaye ni mshtakiwa wa pili na kudai mtuhumiwa hayupo hivyo aliamua kumsubiri. Hata hivyo ilielezwa kuwa, wakati mlalamikaji akiendelea kumsubiri ghafla mtuhummiwa namba mbili, alimwambia mwanafunzi huyo, waende naye na walifikia katika vyumba vya kulala wa geni, iliyoko Sugar Rays, ndipo alipofika Juma Kassim na kuzungumza naye. Katika kosa la pili Pandisha aliieleza mahakama kuwa mnamo mmuda na majjira yanayofanana, mshtakiwa namba mbilii, Godwine Malima, anatuhumiwa kinyume na sheria kumchukua mlalamikaji huyo, na kwenda naye nyumbani kwake, bila ya ridhaa ya wazazi wake, huku akijuafika kuwa ni mwanafunzi na anaumri wa miaka chini ya 18. Watuhumiwa kwa pamoja walikana shtaka hilo, na kupewa dhamana kwa mmasharti ya kuleta mdhamini mmoja mwenye mali isiyo hamishika, na mfanyakazi wa serikali kwa dhamana ya shs. 5 milioni. Hata hivyo, mtuhumiwa namba moja, Juma Kassim alipewa dhamana baada ya kuweza kutimiza masharti ya dhamana, huku mwenzie akionekana kusuasua baada ya wadhamini wake kutokuleta barua ya dhamana.
 
lol Nature kwenye lile tangazo redion kama mtu kwel ? ... ila huyu mwanafunzi nae atakua mtumzimahasidi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom