Wasanii kushtakiwa na kufungwa: Baada ya TID je atafuatia Sir Nature? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wasanii kushtakiwa na kufungwa: Baada ya TID je atafuatia Sir Nature?

Discussion in 'Celebrities Forum' started by WomanOfSubstance, Nov 20, 2008.

 1. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #1
  Nov 20, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Msanii wa muziki wa kizazi kipya "Sir" Juma Nature anakabiliwa na tuhuma za "kubaka" baada ya kukaa kwa siku kadhaa na binti wa chini ya amiaka 18.Endapo mashtaka yatasimama akaonekana na hatia, kuna hatari ya kufungwa kwa muda usiopungua miaka 35 jela chini ya sheria ya makosa ya kujamiiana ( Sexual Offences Special Provisions Act 1998) .

  Kama vile haitoshi, matangazo yanayodhaminiwa na Johns Hopkins yanayotolewa kwenye Radio ( Radio One) kuhusu kuwakinga mabinti dhidi ya ukware wa wanaume watu wazima kama njia ya kupambana na maambukizi ya ukimwi ambamo Sir Nature ameshiriki yamesitishwa.Vilevile filamu ya FATAKI nayo alishiriki - udhamini wa John Hopkins umesitishwa hadi itakapothibitika hana hatia.

  Mbona ni pigo kwa wasanii! Inabidi wasanii waeleweshwa kwamba kuwa star kunaendana na risks ( occupational hazards!!)kama kujikuta kwenye matata na kubanwa na sheria.Huyu Nature inawezekana kabisa hakujua kuwa huyo binti yuko chini ya 18 ( she is 16 yrs) na hata angejua miaka, bado anaweza akawa haujui kuwa kuwa na mahusiano na under 18 hata kama kuna kuridhia ni statutory rape.Kazi ipo.
   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Nov 20, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Atafute lawyer wa kueleweka vinginevyo jela ni yake!!
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  Nov 20, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Huyu jamaa si kaoa juzi juzi hapa tuliskia sasa kwenda kwa kisichana kidogo hicho nini kimemponza tena?Duh am kweli njaa za penzi zitawamaliza wasanii.
   
 4. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #4
  Nov 20, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Fidel80,
  Wasanii wanafanya kazi kwenye mazingira magumu sana...angalia issues kama za akina R Kelly..au kina Papa Wemba hadi alifungwa kisa ni vischana vidogo... unajua these gals at times throw themselves at the artists ..they love them na wanaume wengi hawajui kusema hapana! Hiki ndicho kinachowaponza.Wanahitaji kusaidiwa zaidi on how to manage themselves and the newfound fame ili wasipate madhila kama haya.

  Ushirombo amesema vema kabisa..asipopata lawyer wa kumsimamia kwa makini...ataziona mvua 35! Watanzania kwenye kesi wakati mwingine hudharau na kuona ni kitu kidogo they can manage.Hii kesi si ndogo.Fundisho lilishapatikana kwa what happened to TID!
   
 5. M

  Mangereza Member

  #5
  Nov 20, 2008
  Joined: Oct 28, 2008
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mhh sasa huyo Sir Nature naye mbona anajitafutia matatizo? anatakiwa sasa atafute lowyer ili amsaidie.Sasa naye ajifunze kutokana na makosa aliofanya.
   
 6. S

  Semjato JF-Expert Member

  #6
  Nov 20, 2008
  Joined: Jun 26, 2008
  Messages: 225
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  duh...mathalani wazazi wa binti wakiamua kuachana na hiyo kesi bado jamhuri itakuwa inambana?maana namna ya kuthibitisha kuwa hakuwa anajua umri wa binti ndio kimeo kilipo..namuhurumia though,i personally know him and he's a good person,ukiacha mbali ulevi wa 24/7.
   
 7. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #7
  Nov 20, 2008
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Kazi kweli kweli,

  Hivi unajua hawa wasanii wetu sasa wanatakiwa waweke budget au kuretain wanasheria. Kwa mtaji huu kazi kweli kweli...Upande mwingine wa shilingi, hawa wasanii wajiandaye kupambana na sheria kwani sheria msumeno...i am sorry, this is a second wake up call kwa wasanii...fame is nothing when you are before the court of justice.

  The weakest person is that defame a young gal ... consent is imaterial si ndio women of substance!!
   
 8. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #8
  Nov 20, 2008
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,274
  Likes Received: 4,259
  Trophy Points: 280
  Huyu jamaa FELA alikuwa anamsaidia sana ,anahitaji mtu wa kumshauri kwani kundi lake kazi kuvuta bangi tu
   
 9. M

  Malila JF-Expert Member

  #9
  Nov 20, 2008
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Ok ni vizuri kweli kuweka mwanasheria ili amsaidie, je upande wa pili wa shilingi mbona hatuangalii? Upande ninaotaka tuangalie pia ni huu, je kama kweli kabaka sheria inasemaje juu ya wabakaji.Na vipi kama aliyebakwa naye akiweka mwanasheria kumsaidia ili apate haki yake?
   
 10. Y

  Yassin JF-Expert Member

  #10
  Nov 20, 2008
  Joined: Jul 23, 2008
  Messages: 326
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0


  Awe na kama M.2 amfate huyo hakimu anayesimamia kesi nyumbani kwake basi kila kitu kinakwisha kimya kimya yaani TZ hata kwa dawa sikuamini kabisaaaaaaa maana nchi yetu kwa rushwa imekaa mkononi......
   
 11. m

  mayala luswetul Member

  #11
  Nov 21, 2008
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  naomba kuelewehwa kuhusu kikristu au kiislamu kwa mtu mwenye imani yake sheria ya nchi inasemaje kuhusu Nature?
   
 12. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #12
  Nov 21, 2008
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  I concur with you Mafole.

  Funga macho na ufikirie ni binti yako ndo kafanyiwa kabakwa( kumbuka chini ya miaka kumi na nane hakuna suala la kusema alikubali-SOSPA). Tuache sheria ichukuwe mkondo wake. Hakuna aliye juu ya sheria.

  Sheria ni msumeno...hakuna cha wanaumeeeeeeee!!
   
 13. Chacha wa Mwita

  Chacha wa Mwita Senior Member

  #13
  Nov 21, 2008
  Joined: May 17, 2008
  Messages: 166
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  ina maana tukitaka kufanya ngono sasa ni mhimu kumuuliza binti kwanza ID yake ili uwe na uhakika na umri wake, kama hana ID unamwambia alete passport....? kazi kweli kweli.
   
 14. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #14
  Nov 21, 2008
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mh. unajua kwamba
  1. watoto wadogo chini ya miaka 18 wanalindwa na sheria na hawawezi kukubali(consent). Sasa, wale mabazazi wakae wakijua kwamba ukishikwa na kibinti ni sawa na kuweka rehani maisha yako.

  2. Suala jinginene ni kwamba sheria ni nzuri inajaribu kulinda hawa watoto, si umeona watu wanatumia fedha kulaghai watoto na siku hizi magonjwa mengi..wengine wanatumia tu umaarufu kuadaha hawa watoto.

  3. Suala la kusema kwamba passport au I.D haisaidii... suala ni kukwepa hiyo biashara ya kuvizia binti za watu(chini ya miaka 18).

  UJUMBE KWA SERIKALI:
  Jamii itanyooka tu. Wizara ya elimu Tanzania, wekeni somo la kuhusu sheria ya kujamiaana ndani ya mitaaala ya shule za msingi na hata sekondari kwenye somo la elimu ya uraia... hatupendi kuona damu changa ikiputika kwa UKIMWI.

  Shadow.
   
 15. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #15
  Nov 21, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Na je kila upande ukimfuata huyo hakimu unadhani itakuwaje?
  Na kumbuka kesi kama hii investigation na prosecution ni simple and straightforward. Kinachotakiwa kuthibitishwa ni je, msichana ni under 18 na siyo mke wa mtuhumiwa ( umri mdogo kisheria kuolewa ni 15 yrs), na je mtuhumiwa na msichana husika walifanya kitendo?Mpaka tuhuma zimeenda vyomba vya sheria ni kuwa tayari kuna madai ya kufanyika kitendo.Issue si kuwa msichana alikubali ama lah maana kisheria haitaangaliwa.Its a strict liability thing... it is statutory rape.
  Sasa kwenye hali hii huyo hakimu atakula rushwa hajipendi?
  Kaulize uelezwe mshikemshike wa kesi ya TID ambayo kwanza haifanani kwa seriousness of the offence na bado jela aliionja.
   
 16. Kilbark

  Kilbark JF-Expert Member

  #16
  Nov 21, 2008
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 558
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Watu kama wewe ni mfano mbaya kwa jamii. Kwa sababu unachochea rushwa unabahati sana Invisible hajakuona akakuban. Wewe badala ya kukemea vitendo viovu ndio unavikumbatia? Huu ni mwanzo tu wako wasanii wengi wenye vitendo kama hivi habu fikiria kama angekuwa ni binti yako au mdogo wako au dada yako ungefanyaje? Tuache mambo ya kizushi cha msingi ni kusubiri hukumu itoke kama ana hatia au la na sio kusema mambo ambayo sio ya kiungwana. TUPIGE VITA RUSHWA NA UFISADI.
   
 17. tonge nyama

  tonge nyama JF-Expert Member

  #17
  Nov 21, 2008
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 372
  Likes Received: 377
  Trophy Points: 80
  Ewe kijana Nature, kama kweli umefanya kitendi hicho(pengine kwa kushawishiwa na bange, pombe na elimu ndogo), basi unastahili adhabu kali. Hebu fikiria kama ni binti yako mdogo kabakwa tena kwa zamu (wenyewe mnaita mtungo au kolabo), ni jinsi gani itakuuma.

  Naomba sheria ichukuwe mkondo wake na ikibainika kama kweli ulihusika sheria ichukuwe mkondo wake.
   
 18. B

  BeNoir Member

  #18
  Nov 21, 2008
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana kabisa. Ni wakati mzuri wa jamii kujifunza na kujirekebisha ikibidi.
   
 19. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #19
  Nov 21, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Kama unapenda ku-scratch ovyo ujue jela inakuita! Be careful! Kwani lazima ? Usipofanya utakufa?
  Tafuta mtu mzima mwenzio kama huwezi kujizuia.
   
 20. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #20
  Nov 21, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
   

  Attached Files:

Loading...