Wasanii kushiriki kampeni, tusitegemee Muziki wetu kwenda Kimataifa

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Sep 6, 2014
6,170
7,661
Wasalamu Wakuu.

Naomba Ieleweke kuwa Sisi Kama Tanzania mziki wetu kutoboa Kimataifa Bado Sana Na Tuna Safari Ndefu Mnooo. Hatuwezi Kukaa Kuwa Sawa kama Nigeria, SA na Nchi zingine Zilizotoboa Kimataifa. Hivyo Wasanii Watanzania Nina amini Wanakazi Kubwa Sana Kuhakikisha Mziki Wetu unakuwa Mziki Pendwa Nje ya Tanzania Na Nje Ya Afrika.

Lakini Nachelea Kuamini kama wasanii Wetu Wanaelewa Wanachokifanya Na Kama Sisi Watanzania Tunahitaji Sana Kwenda Kimataifa Kuliko Hii Local.

Kule Ambako tunataka mziki Wetu Uende Kimataifa Tunatambua Ni Watu Wa Aina Gani Wale? Oky Ieleweke kuwa Wale Watu Wametuzidi Kila Kitu kuanzia Mitazamo, Fikra, Utendaji kazi Na Vitu Vingine Vingi. Huwa Ni Watu wakupambanua mambo kuchambua na Kufanya Maamuzi.

Kitendo Cha Asilimia 90% ya Wasanii Wetu Kushiriki Kampeni za Kisiasa Zinaondelea Tanzia Na Ushiriki wao ni Zaidi ya 89%, Hii inadhihirisha kwamba wasanii Wetu hata wale Tunao Wategemea Kutusua Zaidi Kimataifa Hawajui Walifanyalo Na Hawajuii Thamani Yao. Tusitegemee Tuzo Za Kimataifa Zitaona Wasanii Wetu Kama Ni Best Performers Kupitia Hizi Perfomance za Kwenye Kampeni Ambako Kiingilio ni Miguu Yako, Tusitegemee Mziki Wetu Utaenda Kimataifa Kwa Vyombo Vya Mziki Vilivyopo Kwenye Majukwaa haya Ya Kampeni ambavyo Vitanatoa Sauti Mbovuu Kupitiliza Zaidi Zaidi Ni Kujishusha, Hata Kama Mgombea Anapendwa Kimataifa Au Hapendwi.

Lakini Hizi Show za Kwenye Kampeni Inashirisha Ukweli Kwamba Wasanii wa Bongo Maisha Yao ni Magumu sana Bila Show, Mtu Atajituma Kuwa Na Wimbo Mzuri Tanzania Ili Apate Show Za Kwenye Kampeni Lakini isiwe Kwenda Kimataifa, Inasikitisha Sana.

Kule ambako Mziki Wetu Tunataka Ufike Sio Waumini Sana Wa Siasa Au Serikali Iyopo Madarakani Ni Watu wa Kusimamia Haki Na Ukweli. Mfano Mzuri Ni DAVIDO na WIZKID kwenye Issue Ya SARS, Kitu Ambacho Wasanii Watanzania Hawataweza Kuja Kufanya Kwasababu Watu ni sehemu Ya Watu Walioshiriki kufanya Kampeni hivyo sisi Kama Watanzania Tusitegemee kama Wasanii au Mziki Wao Utakuja Kutusaidia Katika Kutetea Haki Zetu pale Itakapotokea Issue kama SARS kule Nigeria.

Lakini Mwanasiasa Ni Nani? Mwanasiasa ni mtu anaehitaji kutimiza Mambo Yake ndani Ya Miaka 5 tuu baada ya Hapoo Hakutambui Tena. Msaada Wanao utoa Wanasiasa Kwa Sasa Kwa Wasanii hawatautoa Wasipokuwa Madarakani. Wasanii Wetu Management zao Zinakosa Uelewa Na Zinakosa Umakini Katika Kusimamia Wasanii Wao. kitendo Cha Wasanii kushiriki kampeni ni Ishara pia Wasanii wetu wana Management Mbovu sanaa...

Hivi Kuna Nchi ambayo Wasanii wanashiriki kampeni Kama TanzaniA? Ni wapi Mziki Wa Tanzania Unaelekea? Tunapiga Hatua Moja Mbele na Kurudi Hatua Kumi Nyuma.

Tuwakumbe wasanii Wetu Wajibu wao.
 
Sioni tatizo. Wanamuziki moja ya vyanzo vyao mapato ni kufanya shoo, sasa kama wanalipwa si wapo kazini?! Wafanyabiashara wa aina nyingine kwani hawafanyi biashara na CCM? Kwanini wanamuziki iwe ndo nongwa kufanya biashara na CCM?! Au sijaelewa?
 
Mpumbavu manake nini?

Maneno ''Mjinga'' na ''Mpumbavu'' yametumika mara kadhaa katika Biblia ili kuwajulisha
watu kwamba wasiwe wajinga na kwamba haiwapasi kuwa wapumbavu.

Jifunze kitu leo kupitia somo hili itakusaidia sana.

Mithali 1:32 "Maana kurudi nyuma kwao wajinga kutawaua, Na kufanikiwa kwao wapumbavu kutawaangamiza. Bali kila anisikilizaye atakaa salama, Naye atatulia bila kuogopa mabaya."
Nini maana ya neno mjinga?
Mjinga ni mtu asiyejua jambo fulani au kitu fulani lakini akijulishwa anaweza kujua.

Nini maana ya Mpumbavu?
Mpumbavu ni mtu anayeshindwa kuelewa jambo hata kama akielekezwa sana.
Pia mpumbavu ni mtu ambaye anafahamu jambo lakini halitendi, mfano wa mpumbavu ni mtu ambaye anajua kabisa kwamba inampasa kuishi maisha matakatifu ya Wokovu haishi maisha hayo matakatifu.

Tofauti ya mjinga na mpumbavu ni kwamba mjinga hajui kitu ila akifundishwa anaelewa na ujinga unaondoka lakini mpumbavu anajua mema lakini hawezi kuyaishi hayo mema.
Biblia hapo juu inatambua kwamba katika wanadamu wajinga pia wapo na wapumbavu pia wapo,
 
Shida ni unafki. Huwezi kutaka wasanii wetu wafike kimataifa wakati nyimbo zao mnapakua na hamlipi hata shilingi 100 tu. Kingine ni chuki kwa hao wanaoonekana wanajitahidi kufika huko (kimataifa) pia hata taasisi zinazohusika na kuinua wasanii wetu bado hazijawa na uwezo wa kufanya hivyo.
 
Maneno ''Mjinga'' na ''Mpumbavu'' yametumika mara kadhaa katika Biblia ili kuwajulisha
watu kwamba wasiwe wajinga na kwamba haiwapasi kuwa wapumbavu.

Jifunze kitu leo kupitia somo hili itakusaidia sana.

Mithali 1:32 "Maana kurudi nyuma kwao wajinga kutawaua, Na kufanikiwa kwao wapumbavu kutawaangamiza. Bali kila anisikilizaye atakaa salama, Naye atatulia bila kuogopa mabaya."
Nini maana ya neno mjinga?
Mjinga ni mtu asiyejua jambo fulani au kitu fulani lakini akijulishwa anaweza kujua.

Nini maana ya Mpumbavu?
Mpumbavu ni mtu anayeshindwa kuelewa jambo hata kama akielekezwa sana.
Pia mpumbavu ni mtu ambaye anafahamu jambo lakini halitendi, mfano wa mpumbavu ni mtu ambaye anajua kabisa kwamba inampasa kuishi maisha matakatifu ya Wokovu haishi maisha hayo matakatifu.

Tofauti ya mjinga na mpumbavu ni kwamba mjinga hajui kitu ila akifundishwa anaelewa na ujinga unaondoka lakini mpumbavu anajua mema lakini hawezi kuyaishi hayo mema.
Biblia hapo juu inatambua kwamba katika wanadamu wajinga pia wapo na wapumbavu pia wapo,
Kwa maelezo hayo inaonekana una experience kubwa ya upumbavu.

Asante kwa maelezo mazuri.
 
Mbona baadhi ya wasanii wetu washatoa kimataifa unataka watoboe Mara ngapi? Diamond mwaka Huu ameshirikishwa kwenye album ya msanii mkubwa mwenye tuzo 5 za Grammy Alicia key mwaka Huu pia atafanya show ureno jukwaa Moja na Bruno Mars huyo huyo diamond kashachukua tuzo si chini ya 90 za kimataifa.

Rayvanny amechukua tuzo ya BET, kiba aliwahi kupata tuzo ya MTV EMA,tuzo za Afrimma za mwaka huu tumeingiza almost wasanii si chini ya 6 wa Kitanzania.

Mtoa mada acha kuteseka waache Wasanii wale mpunga waandeshe maisha yao nilichogundua kutoka kwake shida yako si Wasanii kufanya kampeni ila Ni wasanii kuwafanyia CCM Kampeni.
 
Siungi hoja mkono, unataka kutuaminisha kwamba chanzo cha wasanii wetu kwa wingi wao kushindwa kufikia soko la kimataifa ni kushiriki kwenye kampeni za uchaguzi.? Pili unataka kutuaminisha hao wanaoandaa tuzo wanatumia shows za kampeni kupata nominees kwenye categories? Unataka kutuaminisha Huko Nigeria wasanii ndio walianzisha maandamano? Siyo kwamba wananchi walianzisha Kisha wasanii wakaunga juhudi? Ni lini wananchi wa Tanzania mumewahi kujitokeza kupinga jambo fulani lisilo la kisiasa dhidi ya serikali kuhamasisha haki itendeke? Tatizo la watanzania ni wanafiki sana mnapenda kutupia watu lawama kwa kushindwa kwenu wenyenyewe kutimiza majukumu yenu.
 
Sioni tatizo. Wanamuziki moja ya vyanzo vyao mapato ni kufanya shoo, sasa kama wanalipwa si wapo kazini?! Wafanyabiashara wa aina nyingine kwani hawafanyi biashara na CCM? Kwanini wanamuziki iwe ndo nongwa kufanya biashara na CCM?! Au sijaelewa?
Wapi mleta mada kasema ccm? Kwani ukiwa mataga unaamua kuwa mpumbavu??

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom