monoclinic
JF-Expert Member
- Nov 15, 2013
- 262
- 321
Kuanzia tuianze hii awamu ya tano ya Raisi MAGUFULI,Jimbo la BUMBULI tulikuwa na matumaini kibao ya kuwa na mbuge kijana na Mwenye exposure kubwa ya kisiasa ndani na nje ya nchi yetu(hata upinzani waliogopa kumweka wa kupambana nae) lakini mpaka Leo tukiangalia Hali halisi inakatisha tamaaa.
Sasa hivi tuna halmashauri ya Bumbuli lakini njia ya kuelekea halmashauri hiyo kuanzia Kijiji Cha Soni haifai kabisah,mashimo na makorongo yanayokatiza barabarani ni mengi na ya kutisha na iko chini ya Tanroads hii barabara.Kabla ya uchaguzi mwaka 2015 zilianza harakati za kutaka kuijenga kwa kiwango cha lami hii barabara lakini sijui uliishia wapi huu mradi.
Yuko wapi kiongozi wetu tuliyemchagua kutusemea shida hizi bungeni?
Stendi ya Soni haifai na kipindi hiki Cha mvua.
Jimbo hili takribani miaka 25 lakini naweza sema halina hata maendeleo ambayo unaweza kujivunia.Nakumbuka zamanı nikiwa nakua kulikuwa na kiwanda Cha chai mponde, Kiwanda Cha chai Kwekulo,tulikuwa na Vuga Press,Usadeko(Kama sijakosea), viwanda vyote hivi vilitupatia ajira Sana vijana lkn vilikufa kifo Cha milele.
Kitu pekee nachoona Ni uwekwaji wa changarawe njia ya kutoka Soni Hadi sokoni takribani nusu kilometa.Na hii pongezi Ni kwa TARURA.
Ni muda Sasa vijana na wazeee tuamke,tupiganie maendeleo ya Jimbo letu.Hakuna wa kuja kutuletea maendeleo na kutatua kero Kama hizo hapo juu Kama tutabaki kushangaa.
Tunataka tupate kiongozi jasiri,shupavu,Mwenye uchungu na Bumbuli yetu.
Sisi wasambaa tunasema
"Mwena ndio,ne ndie jimuunguike"
Sent using Jamii Forums mobile app