Uchaguzi 2020 Wasambaa tuamkeni jamani, miaka mitano jimbo la Bumbuli ni aibu tupu

monoclinic

JF-Expert Member
Nov 15, 2013
262
321
Kuanzia tuianze hii awamu ya tano ya Raisi MAGUFULI,Jimbo la BUMBULI tulikuwa na matumaini kibao ya kuwa na mbuge kijana na Mwenye exposure kubwa ya kisiasa ndani na nje ya nchi yetu(hata upinzani waliogopa kumweka wa kupambana nae) lakini mpaka Leo tukiangalia Hali halisi inakatisha tamaaa.

Sasa hivi tuna halmashauri ya Bumbuli lakini njia ya kuelekea halmashauri hiyo kuanzia Kijiji Cha Soni haifai kabisah,mashimo na makorongo yanayokatiza barabarani ni mengi na ya kutisha na iko chini ya Tanroads hii barabara.Kabla ya uchaguzi mwaka 2015 zilianza harakati za kutaka kuijenga kwa kiwango cha lami hii barabara lakini sijui uliishia wapi huu mradi.

Yuko wapi kiongozi wetu tuliyemchagua kutusemea shida hizi bungeni?
Stendi ya Soni haifai na kipindi hiki Cha mvua.

Jimbo hili takribani miaka 25 lakini naweza sema halina hata maendeleo ambayo unaweza kujivunia.Nakumbuka zamanı nikiwa nakua kulikuwa na kiwanda Cha chai mponde, Kiwanda Cha chai Kwekulo,tulikuwa na Vuga Press,Usadeko(Kama sijakosea), viwanda vyote hivi vilitupatia ajira Sana vijana lkn vilikufa kifo Cha milele.

Kitu pekee nachoona Ni uwekwaji wa changarawe njia ya kutoka Soni Hadi sokoni takribani nusu kilometa.Na hii pongezi Ni kwa TARURA.

Ni muda Sasa vijana na wazeee tuamke,tupiganie maendeleo ya Jimbo letu.Hakuna wa kuja kutuletea maendeleo na kutatua kero Kama hizo hapo juu Kama tutabaki kushangaa.

Tunataka tupate kiongozi jasiri,shupavu,Mwenye uchungu na Bumbuli yetu.

Sisi wasambaa tunasema
"Mwena ndio,ne ndie jimuunguike"
IMG_20200420_144043_1.jpg
IMG_20200420_182247_6.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumekucha wewe ndo unakumbuka shuka; wakati mnampa nguvu ya kupita bila kupingwa kwa kufanya figisu hamkujua kua amna yote hayo?
Jimbo la New york yenyewe amna anaepita bila kupingwa sembuse Bumbuli!!
 
Bora umeliona hilo mkuu..ile barabara ni kisanga,tangu uhuru..na ile njia kuna mazao mengi sana..binafsi nimeshawahi kuishi pale Soni nashindwa kuelewa ilikuaje hizo taasisi ulizozitaja zikafa,mbaya zaidi ndugu zetu kule hawana hata presha,wakipigiwa mdumange wakigonga mchele na kupewa kofia na t-shirt "kama kawaida" wanarudia makosa yaleyale.
 
kipi bora kati ya jimbo na urais? wewe ungeweka wapi nguvu na harakati zako? kweli sijui mko nchi gani nyie! tangu lini mtu mwenye ndoto za alinacha za urais akaishi mjini na kujali wa kijijini? chukueni maamuzi acheni kulia lia!
 
Kumekucha wewe ndo unakumbuka shuka; wakati mnampa nguvu ya kupita bila kupingwa kwa kufanya figisu hamkujua kua amna yote hayo?
Jimbo la New york yenyewe amna anaepita bila kupingwa sembuse Bumbuli!!
Unadhani tatizo ni letu.hakuna chama kilikuwa na ubavu wa kupambana nae.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bora umeliona hilo mkuu..ile barabara ni kisanga,tangu uhuru..na ile njia kuna mazao mengi sana..binafsi nimeshawahi kuishi pale Soni nashindwa kuelewa ilikuaje hizo taasisi ulizozitaja zikafa,mbaya zaidi ndugu zetu kule hawana hata presha,wakipigiwa mdumange wakigonga mchele na kupewa kofia na t-shirt "kama kawaida" wanarudia makosa yaleyale.
Elimu bado hatuna huku..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nan aliwaambia mchague CCM
Mnavuna mlichopanda

god is good
 
Unadhani tatizo ni letu.hakuna chama kilikuwa na ubavu wa kupambana nae.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huo ndo ujinga wenu; yaani mnaona kiongozi dhaifu badala ya kupambana nae mnawaacha eti chama kipambane nae!!!

Kiongozi asipotekeleza majukumu yake anaondolewa na wananchi siyo kusubiri chama flani eti ndo kiwe na nguvu au wewe hujui kua kuna kura za hapana zinaweza kuzidi kura za ndiyo mpaka akili zimrudi.
 
Nadhani hujui hata kinachoongelewa hapa.

Hujui 2015 hali ilikuwaje.
Ngoja tu nikupuuze.

Sasa uchaguzi bado itamuondoaje kiongozi wa kuchaguliwa??umpige mawe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom