Wasaliti waiomba radhi CHADEMA kutoa matamko kwa kushinikizwa maamuzi Kamati Kuu

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,886
6,883
Amani Golugwa..jpg
Amani Golugwa
Mkuu Kanda ya Kaskazini

Viongozi wanne wa Chadema Mkoa wa Tanga, wamedaiwa kukiri kuhusishwa katika mtandao wa kukivuruga na wameomba kusamehewa wakidai kwamba walidanganywa.

Viongozi hao ambao waliwahi kutoa tamko la kupinga maamuzi ya Kamati Kuu ya Chadema kwa kumvua uongozi aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe, Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk. Kitila Mkumbo na Mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba, waliomba radhi mbele ya katibu Mkuu Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Golugwa alisema viongozi hao Tanga wameomba kusamehewa.

Alisema walikiri kuwa walikuwamo katika mtandao ujulikanao (MK1-50) na kwamba waliamua kupinga kwenye vyombo vya habari maamuzi ya Kamati Kuu kutokana na kudanganywa.

“Miongoni mwa majukumu yaliyonileta hapa Tanga ni kuwashughulikia hawa viongozi waliotoa matamko ya kupinga maamuzi ya chombo halali cha Kamati Kuu, lakini wameomba msamaha na kukiri kuwa walidanganywa,”alisema na kuongeza kuwa wamesamehewa, ingawa wataendelea kufuatiliwa nyendo zao.

Katibu huyo alisisitiza kuwa kinachoendelea hivi sasa ndani ya Chadema ni kutumbua majipu yaliyokuwa yakikisumbua na kwamba hakitarejea nyuma bali kitahakikisha kinasafishika.
 
Candid Scope Mtabakiza mbao mwaka huu.
Chama cha Kichaga hakiwezi kuitawala nchi ya makabila 126
 
Last edited by a moderator:
dah...poleni chadema naona mko na tough job kuna changamoto ya kupambana na ukweli ambao unaitwa propaganda
 
Mtabakiza mbao mwaka huu.
Chama cha Kichaga hakiwezi kuitawala nchi ya makabila 126

Yakhe mbona unababaika bila kutuliza kichwa uandike kinachoendana kujibu mada inayoeleza waliotumika kuhongwa kutoa matamko wameanza kujirudi na kuamua kuanika ukweli kwamba walitumiwa na hao wasaliti wahujumu wa chama na sasa wameamua kurudi ndani ya kundi, wewe umepatapata hapo? Ulifikiria wataendelea kutoa matamko na sasa imekuwa kinyume cha matarajio siyo?
 
Safi sana kamanda, wote wenye nia ovu watajitokeza wenyewe, na bado wataumbuka sana safari hii. Watajuta kuchagua chama makini wakat wao hawako makini
 
ili msamaha uwe murua lazima wadisclose timu yao waliyokuwa wanaitumikia, wamtaje mfadhili wao n.k
Na umma ufahamishwe kupitia wanahabari.

Sio vizuri ku disclose mambo yote yanayopatikana kutoka kwa wanamtandao bali muda muafaka ukifika basi kila kitu kitawekwa hadharani na ni vizuri tukikumbuka kuwa "Kumchinja kobe yapaswa kumlia timing"
 
mtabakiza mbao mwaka huu.
Chama cha kichaga hakiwezi kuitawala nchi ya makabila 126

mkuu acha kueneza chuki kama jina lako na tukisema ccm ni chama cha muslim bcs viongozi wake woote ni muslim italeta picha gani. Acheni ujinga ninyi ma ccm.
 
"Miongoni mwa majukumu yaliyonileta hapa Tanga ni kuwashughulikia hawa viongozi waliotoa matamko ya kupinga maamuzi ya chombo halali cha Kamati Kuu, lakini wameomba msamaha na kukiri kuwa walidanganywa,"alisema na kuongeza kuwa wamesamehewa, ingawa wataendelea kufuatiliwa nyendo zao.
Sie watu wa mwambao tafsiri ya "kuwashughulikia" ni mzito kidogo! God forbid isiwe hiyo tafsiri tunayoifahamu sisi.
 
21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom