Wasaidizi wa viongozi wetu wajifunze hapa

KANYEGELO

JF-Expert Member
Nov 12, 2019
2,149
4,752
Na Thadei Ole Mushi.

Shida kubwa waliyonayo Viongozi wetu kwa Sasa ni kuongoza jamii yenye maarifa na Elimu kwa wingi.

Jamii aliyoongoza Nyerere si sawa na aliyoongoza Mwinyi. Jamii aliyoongoza Mwinyi si sawa na aliyoongoza Mkapa. Jamii aliyoongoza Mkapa si sawa na aliyoongoza JK na jamii aliyoongoza JK si sawa na anayoiongoza JPM na jamii anayoiongoza JPM itakuwa si sawa na itakayoongozwa na atakayemrithi. Huu ni ukweli na haitaji uwe na Elimu ya chuo kikuu kuuona ukweli huu.

TWENDE SAWA.

Imekuwa kawaida kabisa Sasa kiongozi anajifungia ndani anajiandaa haswa anatoka hadharani anaongea Jambo lake anaingia kwenye Gari yake kabla ya kufika nyumbani Jambo lile linachambuliwa na kuonekana kaongea kituko kabisa. Wasikasirike Bali wajifunze kuwa ni aina ya jamii waliyonayo kwa Sasa.

Kwa Sasa tuna wahitimu wengi haswa wa vyuo vikuu, na vyuo vya Kati wenye maarifa mbalimbali, Sasa hivi technolojia ya kupashana habari imekuwa, siku hizi watu wanajua haki yao ya kutoa maoni nk. Katika jamii Kama hii lazima Viongozi wetu wajiongeze na watafute maarifa mapya ya kukabiliana na jamii Kama hiyo.

Niliwahi kuwaandikia umuhimu wa hotuba za Viongozi wetu kuandaliwa kabla ya kuzisoma public. Nikiwasimulia kisa Cha Ghana na Marekani msaidizi wa Obama kwa kuandika haya nanukuu:-

"Kuna mtu anaitwa Nana Addo Dankwa Akufo-Addo huyu ni Rais wa Ghana. Ukimuuliza Leo mojawapo ya vitu ambavyo viliwahi kumkasirisha atakuambia ni January 7 mwaka 2017 siku aliyokuwa akiapishwa.

Siku hiyo mwandishi wa Hotuba zake bwana Eugene Arhin alifanya copy and paste ya hotuba ya Hotuba za marais wa Marekani Bill Clinton na Bush na kumpatia Rais ili akaisome kwa wananchi wa Ghana.

Hotuba hiyo ilisifiwa sana ila baada ya muda mfupi hata kabla ya Raisi kutoka kwenye Sherehe za kuapishwa watu walianza ukosoaji kitendo kilichomfanya Eugene Arhin kuomba msamaha kwa Rais na kwa wananchi wa Ghana. Ilikuwa aibu ya Mwaka ambayo Nana Akufo- Addo aliingia nayo Ikulu."

NATAKA KUSEMA NN?

Nataka kusema kuwa Viongozi wetu wasaidiwe vyema katika maandalizi ya hotuba wanazokwenda kuzitoa kwenye majukwaa.

Kiongozi anaweza kukumbukwa kwa mambo makuu mawili moja speech zake au mambo aliyokuwa akiyafanya.

Ni Mara Chache sana kiongozi anaweza kuaandaa speech yake mwenyewe na kuitoa hadharani bila kupitia kwa mtu mwimgine kuihariri na kuifanyia marekebisho.

Mandela mpaka anakufa alitoa hotuba nyingi zenye msisimko lakini iliyovunja rekodi ni ile aliyoandaliwa na mhariri Nadine Gordimer akisaidiana na mwandishi Antony Sampson hotuba hii inaitwa "Iam Prepared to die"

Wataalamu wa mambo wanasema hakuna speech ambayo imewahi kuvunja rekodi speech hii katika kusomwa na kutumika kama reference katika taifa la Afrika kusini.

Hapa kwetu Kuna Mama alikuwa akiitwa Joan Wicken huyu alikuwa ni raia wa uingereza ndiye alikuwa nyuma ya Speech za Baba Wa taifa Mwalimu Nyerere. Hotuba zote alizozitoa Nyerere njee ya nchi zilipitia kwa mama huyu Mwingereza aliyekuwa msaidizi wa mwalimu Nyerere.

Duniani kwa sasa Speech za Obama zinaendelea kuingiza mamilioni ya shilingi baada ya kuunganishwa kwa pamoja na kutengeneza kitabu. Piteni kwenye maduka ya kuuza vitabu mtaona

Sio Obama alikuwa akiandika hizi Speech Bali ni mtu aliyeitwa Jon Favreau ambaye Obama alianza naye pindi alipochaguliwa tu kuwa seneta na baadaye alihamia naye Ikulu. Obama alikuwa akimuita Favreau jina la utani "Mind Reader" kwa uwezo aliokuwa nao wa Kugundua nini Rais anataka kukisema na kukiweka kitaalamu ili kivutie watu na kifanye Clarification ya matatizo au Minongono ya wananchi.

January Makamba alijitutumua Kweli kuacha alama kwa Mzee Kikwete alikuwa anausoma mchezo, kwa vyama vya Siasa, Mitandaoni na kimataifa ndio anakaa anaandika speech ya Rais. Kwa kweli alijitahidi sana sintoshangaa Speech za Kikwete kuzikuta madukani, nimeshaona na kusoma kadhaa za Mzee Mkapa.

Pale Kenya Uhuru Kenyatta anao watu wawili Muhimu Sana mmoja anaitwa Eric Ng'eno na wa pili ni Denis Ithumbi. Eric Ng'eno yeye anahusika na kuandika Speech za Rais huku Denis yeye akiwa ni mzee wa media kwa ajili ya kuset Propaganda na kujibu propaganda zote zinazomhusu Rais. Hawa ndio wanaompa Kenyatta Mvuto alionao Sasa. Kwa Nature ya wakenya ku win makabila yote Kama Kenyatta ni kazi kubwa Sana na kazi hii inafanywa na Hawa vijana wawili kwa ustadi mkubwa. Wanajua jamii inataka Nini na ipo katika Hali gani.

Viongozi wetu wafahamu kuwa wao ni zaidi ya watabibu speech zao zinaweza kutibu majeraha ya watu au kuwatonesha, au kuwagawa watu au kuwapa mfadhaiko watu. Lazma viongozi wetu kwa umuhimu wao wasaidiwe eneo hili la public speaking.

Speech zao ziache alama na zije kutumika vizazi na vizazi hadi mashuleni wanafunzi wajifunze kwa kutumia hotuba hizi. Hatuba hizi zionyeshe uwezo alionao kiongozi katika kutatua matatizo sio kusababisha matatizo.

Ukifuatilia mijadala mingi na mitafuruku mingi kwenye jamii yetu yanaibuliwa na viongozi wetu hasa kupitia hotuba zao. Tujitahidi kujenga taifa lenye umoja, haki na Ustawi bora kwa jamii yetu.

Wanaoandaa speech hizi za viongozi walenge mahitaji ya jamii na ustawi wa jamii husika. Speech hizi ziondoe Sintofahamu na mpasuko wa jamii, Speech hizi ziwaunganishe wana jamii zaidi. Speech hizi ziwe bora kiasi cha kuja kutumika na vizazi vingine.

Pichani ni Barack Obama akiwa na Msaidizi wake Ikulu ambaye ndiye humwandikia hotuba zake.

Picha ya pili ni January makamba akiwa na JK kwenye Kampeni kule Maswa hapo Ni baada ya kuwalisha Uongo na matumaini kibao wananchi wanaolima Pamba huko.

Picha ya tatu ni Uhuru Kenyatta akiwa na mashine ya Uongo na matumaini Denis Ithumbi.

Picha ya Nne ni Mwalimu Nyerere akiwa na Msaidizi wake wa Hotuba Mwanamama Joan Wicken.

CC: Polepole
CC: MATAGA

Ngoja nirudi jalalani.

Ole Mushi
071270602
FB_IMG_1585738377382.jpg
FB_IMG_1585738383697.jpg
FB_IMG_1585738389290.jpg
FB_IMG_1585738473255.jpg

sent from HUAWEI
 
Attachments

  • FB_IMG_1585738383697.jpg
    FB_IMG_1585738383697.jpg
    24.5 KB · Views: 1

071270602View attachment 1405835View attachment 1405836View attachment 1405837View attachment 1405838

sent from HUAWEI
Kwa jiwe atakuwa ni bashite ndio maana mambo yako hovyo hovyo.
 
KANYEGELO nashukuru kwa kuleta bandiko hili la Ole Mushi. Kwa kweli limejaa ushauri mwanana sana na mjarabu kwa uwasilishaji mawazo ya viongozi wetu kwa wananchi!!
 
Mbona wa JPM hujatutajia ni nani?
Natamani kumjua maana jamaa anamwambia nenda kaseme tumetoa elimu bure, sgr tunajenga kwa hera zetu, tumejenga maviwanda n.k
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom