Wasaidizi wa rais wengi wana-underperform ila wakisikia ziara ya kiongozi mkuu wanahaha sana kuficha underperformance zao

Buffet

JF-Expert Member
Aug 11, 2018
639
1,569
juzi hadi Jana zilikiwa zinazagaa taarifa kuwa mhandisi wa manispaa ya songea kawekwa ndani na mkuu wa mkuo wa ruvuma kisa ni chambers za maji taka kuonekana juu katikati ya barabara ya mtaa sovi-mabatini,huenda uamzi wa mkuu wa mkoa ulikuwa sahihi lakini kwanini hili lifanyike Jana?

Hii barabara ilianza kujengwa na kampuni ya wachina toka 2017 na hizi chambers zilionekana toka kipindi hicho,mfano zipo chamber mbili mbele ya pappaya lodge kwenye barabara hii ya sovi mabatini,pia kuna chamber moja iko kwny diversion ya kuingia manzese Sokoni,ukiachana na hii barabara ya huu mtaa,njoo barabara ya majengo ukitokea lamoly pub kuelekea majengo mitumbani,mkabala na greenbelt lodge kuna chamber barabarani,inamaana viongozi wa mkoa walikuwa hawajaikagua hii barabara toka 2017,au baada ya iringa waziri mkuu atafanya ziara ruvuma????

Nawaza tuu,,,,,,,,,,,,,matukio haya ya viongozi kujihami wayafanye kwa namna ambayo haiwaumizi watendaji wa chini yao,kama ni uwajibikaji wahusike wote maana mkuu wa mkoa alijua kuwa hizi chambers zipo hata kabla barabara hawajakabidhiwa,ila engineer na wewe ulienda chuoni kusomea uhandisi gani hadi uruhusu hili kwny eneo lako la kazi?????
 
Mtoa mada toa mfano
RC ruvuma na ishu ya chambers za maji taka juu ya barabara,zilikuwepo tangu barabara walipokabidhiwa na mkandarasi ila harufu ya ziara ya waziri mkuu mkoani ruvuma imefanya RC amruke mhandisi wa manispaa kutaka kujiweka safe kwa upande wake,kuna yule Gabriel wa Geita,saiv yupo kimya ila ikipangwa ziara ya kiongozi mkuu wa serikali mkoani humo huwaga anapagawa,alishawahi kupiga marufuku waalim kuvaa suti,mifano ni mingi muda hautoshi
 
Mkuu Umenikumbusha nyumban ulipo taja mitaa Swali la kizushi VP mkuu ile Barabara ya lami inayo anzia hapo manzese kwenda mjimwema ishafika maeneo ya hospital ya mjimwema?
 
..hata Raisi ana underperform.

..hali ya kipato cha wananchi haijaimarika tangu aingie madarakani.

..ukosefu wa ajira umeendelea kuwa tatizo sugu.

..ameshindwa kuwaunganisha waTz.

..kumeibuka utamaduni mpya wa matendo ya kinyama na kikatili dhidi ya wafuasi na viongozi wa vyama mbadala.

..amechafua taswira ya Tz kimataifa,na ameharibu mahusiano ya Tz na marafiki zetu wa muda mrefu.
 
Ni Kwa sababu wote kazi yao ni moja tu,kuwawinda wapinzani ndio kazi yao kubwa na inayowaweka kazini
 
Back
Top Bottom