Wasaidizi wa Mnyika wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kuhisiwa kufanya uharifu

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
34,857
2,000
Mpeni habari hii ,mnyika asahau ubunge mwaka ule alikoswakoswa jimbo likagawanywa sasa hana chake


USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
Mav. yako! Umeleta taarifa za kishenzi kisha unaongeza na ushenzi tena.
Mie nawaambia jeshi LA polisi sasa limekuwa idara ya uenezi Chadema bila kujijua kwa upumbaf wao.
Hivi wangenyamaza sio ajabu no wachache wangejua kuwa Mnyika yuko Mwanza, lakini wanafanya matendo ambayo hata wenye kadi za ccm lakini wanaakili wanajikuta huruma inaingia kuwa uonevu umezidi kwa Chadema.


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kisima

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
3,825
2,000
"wanahisiwa kuwa ni waharifu"
Kwamfano ikithibitika kwamba siyo waharifu?!
Na why umtie mtu korokoroni kwa kuhisi??
 

mbenge

JF-Expert Member
May 15, 2019
1,034
2,000
Jeshi la polisi wilayani mwanza limewashikiria wasaidizi wawaili wa mbunge wa kibamba John Mnyika kwa tuhuma za uhalifu

Kamanda wa polisi mkoani mwanza amewataja wanaume wawili Abdukarimu muro ambaye ni derava wa mnyika na said haldani kwa kufanya uharifu jijini humo, wawili hao watapelekwa mahakamani wakati wowote uchunguzi ukikamilika ili wajibu tuhuma zinazo wakabili

Kamanda huyo amesea makosa yao yatawekwa wazi hivi punde
******

Tukio la kukamatwa, kuhojiwa na kushikiliwa kwa muda na kabla ya kuachiwa kwa wasaidizi wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika umeibua mgongano kati ya Jeshi la Polisi Tanzania na chama hicho.

Mgongano huo umeibuka baada ya pande hizo mbili kutaja eneo tofauti la tukio na sababu za kukamatwa kwa watu hao ambao ni Ofisa Habari wa Chadema na Msaidizi binafsi wa Mnyika, Abdulkarim Muro na dereva wa Katibu Mkuu huyo, Said Haidan.

Wakati Jeshi la Polisi kupitia kwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro inadai maofisa hao wa Chadema walikamatwa kwenye nyumba moja jirani na Hoteli ya Paradise eneo la Mahina jijini Mwanza, Chadema wao wanadai ukamataji ulifanyika ndani ya hoteli hiyo.

Pande hizo pia zimetofautiana sababu za ukamataji kwa Polisi kudai ulitokana na taarifa kutoka kwa raia wema kuhusu kuwepo wa watu wanaohisiwa kuwa ni wahalifu wakati Chadema wanadai maofisa wake walikamatwa kama sehemu ya kumsaka Katibu Mkuu wake, John Mnyika aliyekuwa jijini Mwanza kwa mapumziko na shughuli za kifamilia.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari leo Desemba 30, 2019, Kamanda Muliro amesema maofisa hao waliokamatwa Desemba 29, 2019 walikutwa kwenye nyumba moja iliyo karibu na hoteli ya Paradise eneo la Mahina jijini Mwanza kutokana na taarifa kutoka kwa raia wema.

“Baada ya taarifa hizo, jeshi la polisi lilifanya ufuatiliaji wa haraka na kuwakamata watu hao wawili ambao katika mahojiano ya awali walikataa kutoa utambulisho wao kuwa ni akina nani na wamefika maeneo hayo kufanya shughuli gani,” inasema taarifa hiyo

“Hivyo jeshi la polisi liliwachukua na kuwapeleka kituo cha kati ambapo hata hivyo baadaye walitoa ushirikiano kwa askari na kutaja majina yao,” inaeleza zaidi taarifa hiyo

Anasema baada ya kujiridhisha kuwa watu hao hawakuwa wahalifu, Polisi iliwaachia huru.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu leo Desemba 30, 2019, Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itifaki na Mambo ya Nje ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema taarifa ya polisi imepotosha kuhusu eneo la tukio na sababu za kukamatwa kwa maofisa wa chama hicho.

“Maofisa wetu ambao wako Mwanza na Katibu mkuu (John Mnyika) kwa mapumziko na shughuli ya kifamilia walikamatwa wakiwa ndani ya eneo la hoteli ya Paradise; taarifa ya polisi kuwa waliwakamata nyumba jirani na hoteli inaibua hisia ya nia ovu katika tukio hili,” amesema Mrema na kuongeza

“Hata madai kuwa walihisiwa kuwa wahalifu siyo sahihi kwa sababu baada ya kuwakamata (polisi) waliwahoji kuhusu alipokuwa katibu Mkuu, John Mnyika,”

Pamoja na kulaani kitendo hicho, Mrema ameiomba jeshi la Polisi kufanya kazi kwa weledi bila kujiingiza kwenye masuala ya kisiasa kwa kuwadhibiti viongozi, wanachama na wafuasi wa vyama vya upinzani.

“Mbona Katibu Mkuu wa CCM (Chama Cha Mapinduzi) anazunguka kila sehemu nchini akifanya vikao vya ndani na kuhutubia mikutano ya hadhara bila kubughudhiwa na polisi ambao huonekana wakisindikiza msafara wake,” amehoji Mrema.
***

My take

Mnyika umekimbia jimbo lako miaka mingi na sasa umeibukia kwenye ukatibu na kuanza kugombana na dola ili kutengeneza kura za huruma sisi wakazi wa kimbambq tunakwambia imekula kwako


Malizana na polisi uje 2020 tukuvue ubunge

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
"My take

Mnyika umekimbia jimbo lako miaka mingi na sasa umeibukia kwenye ukatibu na kuanza kugombana na dola ili kutengeneza kura za huruma sisi wakazi wa kimbambq tunakwambia imekula kwako

Malizana na polisi uje 2020 tukuvue ubunge"


Baada ya kuja na maelezo yooote hayo kumbe hoja yako ipo kwenye hitimisho lako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

LIMBOMAMBOMA

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
6,260
2,000
Wajiandae kupigwa money loundering.kwa sasa kazi kuu ya jeshi LA polis Ni kupambana Na wapinzani Wa ccm kwa kuwambikia kesi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom