Amoxlin
JF-Expert Member
- May 30, 2016
- 3,782
- 4,108
Salaam wanaJF,
Nimebahatika kuishi na wasaidizi wa kazi za ndani kwa vipindi mbalimbali na kujionea maswahibu yao kama ifuatavyo.
Nikiwa na umri wa miaka sita tulikuwa na dada wa kazi na kila wazazi wakienda kazini alikuja kaka mmoja na waliingia chumbani na kujifungia pamoja na kufunga pazia. Sikufahamu kilichokuwa kinaendelea ila hasira zangu ilikuwa kwanini wajifungie wenyewe waniache nje?
Baadae tukapata msaidizi mwingine, huyu alikuwa msabato basi kila Jumamosi akienda kanisani anarudi mida mibovu. Kazi ikamshinda akafungasha.
Miaka ikazidi kusonga tukapata mwingine mtu mzima. Huyu alikuwa akiuza vitu vya ndani kama mchele, nyanya na vitunguu ambavyo vilikuwa vinanunuliwa kwa jumla. Hakuwa mwaminifu, alikuwa mdokozi sana.
Miaka ikasogea tena tukapata msaidizi mchapakazi sana, huyu katika zoezi la kupima afya kwa familia nzima aligundulika na VVU. Alipoenda hispitali kupima na kupata ushauri akagundulika pia ana mimba changa. Alichukua uamuzi wa kutoroka bila kuaga, aliiba tu vipodozi.
Baada ya huyo walipita wengine kadhaa. Nikampata mmoja funga mwaka, yeye ikimuelekeza mambo yanayohusu maisha anaanza kulia. Hajui kusoma wala kuandika, ilibidi nimfundishe japo kusoma saa ili aende na muda.
Katika suala la kazi alikuwa mvivu hafai, anafanya kazi huku anajitegea mwenyewe. Akisikia kishindo ndo anakurupuka na kuendelea na kazi.
Akibandika chakula jikoni hawezi kukisimamia kisiungue, ni balaa tupu maana hata ugali hauivi anaogopa kuunguza sufuria.
Hao ndio niliokutana nao.Vipi nyinyi wenzangu?