Elections 2010 Wasaidieni chadema kwa hili la upotoshwaji wa hoja yao na propaganda

Hakuna media zenye nguvu hapa nchini kuandika haya.Media nyingi zina milikiwa na wana ccm.Media 4 tu zina uwezo a kuandika kitu bila woga wakiongozwa na Mwanahalisi.Hvi nyie waandishi wa habari hamuwezi kusimama kwa miguu yenu hadi muegemee kwa wamiliki?mmiliki hajasoma fani hiyo kwanini akubabaishe?kama ni kazi utapata nyingine si lazima ufie hapo.Tatizo kubwa linalowasumbu wana media ni kuganga njaa.Tazama media kama New habari,utabaini kuwa njaa kali.Nimeapa kutonunua magzeti kam hayo.Simameni kwa miguu yenu jamani.CDM itapata support toka kwetu na mitaani tunaendelea kuonyesha udhaifu wa ukandamizaji wa ccm kwa wananchi.Binafsi naamini ahadi walizoahidi hawana uwezo wa kutekeleza.JK HATAJENGA UWANJA WOWOTE WA NDEGE WA KISASA HUKO MISENYI KAMA ALIVYOSEMA.TUKAE TUONE.ATUAMBIE UWANJA WA SONGWE MBEYA UMEISHA?
 
Kitu kilicho kikubwa ni kwetu wananchi kujua ukweli na kuhamasishana, kususia vyombo vyote vya habari vinavyopotosha ukweli wa mstakabali nchi yetu. Mimi naomba wana JF tuanzishe mchakato wa kutambua magazeti, radio na TV vya kususiwa, tuhamasishe wananchi ili tuonyeshe Peoples power. Huko Kenya, Raila Odinga na ODM waliamua kwa kauri moja kususia bidhaa wakasikilizwa.

Hapa kwetu tunaweza pia. Kwa uwingi wetu tunaotaka mabadiliko, tunaweza kutumia nguvu ya umma na kuwafanya waandishi wenye mtindio na wamiliki wa vyombo vyao wakabadilika wakaanza kuandika habari za ukweli au za mlengo wa kimageuzi!

Mimi nafikiri tunaweza kususia Magazeti ya
1. Mtanzania, Rai na The African.
2. Uhuru na Mzalendo
3. Habari Leo
4. Al Hulda
5. Zanzibar leo
6. ENDELEZA
TV TUACHA KUANGALIA TBC, CHANNEL TEN NA BAADHI YA VIPINDI VYA STAR TV.
Halafu tuache kusikiliza Vipindi vinavyoendeshwa na watangazaji wanaojipendekeza pendekeza kama Kibonde, mario hassan, etc
 
slaa mwenyewe alikuwa ccm, na katiba ilitungwa na yeye akiwa mbunge kupitia ccm leo hii adai katiba mbovu kwanin hakudai kipindi kile yuko ccm au ndo giya ya kwenda ikulu?
 
Back
Top Bottom