Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 5,897
- 10,358
Watoa huduma za usafiri pamoja na wafanyabiashara mjini Mtwara,wamesitisha kutoa huduma kwa madai kwamba wanaomboleza vifo vya wenzao waliofariki katika vurugu zilizotokea mwaka jana tarehe 22 may.
Source: Radio One stereo
Source: Radio One stereo
Habari zilizotufikia punde ni kwamba watoa huduma za usafiri pamoja na wafanyabiashara mjini Mtwara,wamesitisha kutoa huduma kwa madai kwamba wanaomboleza vifo vya wenzao waliofariki katika vurugu zilizotokea Mei 22, 2013.
Maduka mbalimbali yamefungwa kuanzia asubuhi hadi mda huu wakishinikiza kupewa nafasi ya kuwakumbuka wenzao waliokufa katika vurugu za kupinga gesi kusafirishwa kwenda Dar es Salaam,
Baadhi ya watu waliokufa katika vurugu hizo ni pamoja na Mama mjamzito huku baadhi ya wakazi wa mkoa huo wakiwemo akinamama na watoto waLIyakimbia makazi yao kuogopa Mabomu ya Machozi yaliyopigwa na Askari wa kutuliza ghasia (FFU).
Wakuu mwenye taarifa zaidi atujulishe...
Source: ITV