Wasafirishaji na wafanyabiashara Mtwara wasitisha kutoa huduma ili kuomboleza vifo vya wenzao

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Watoa huduma za usafiri pamoja na wafanyabiashara mjini Mtwara,wamesitisha kutoa huduma kwa madai kwamba wanaomboleza vifo vya wenzao waliofariki katika vurugu zilizotokea mwaka jana tarehe 22 may.

Source: Radio One stereo

Habari zilizotufikia punde ni kwamba watoa huduma za usafiri pamoja na wafanyabiashara mjini Mtwara,wamesitisha kutoa huduma kwa madai kwamba wanaomboleza vifo vya wenzao waliofariki katika vurugu zilizotokea Mei 22, 2013.

Maduka mbalimbali yamefungwa kuanzia asubuhi hadi mda huu wakishinikiza kupewa nafasi ya kuwakumbuka wenzao waliokufa katika vurugu za kupinga gesi kusafirishwa kwenda Dar es Salaam,

Baadhi ya watu waliokufa katika vurugu hizo ni pamoja na Mama mjamzito huku baadhi ya wakazi wa mkoa huo wakiwemo akinamama na watoto waLIyakimbia makazi yao kuogopa Mabomu ya Machozi yaliyopigwa na Askari wa kutuliza ghasia (FFU).

Wakuu mwenye taarifa zaidi atujulishe...

Source: ITV

Ndo ukweli wenyewe huo mimi niko mjini hapa huduma hakuna leo! Sababu km zilivyotajwa na itv!
 
Mimi naungana nao kwani wanaonyesha uzalendo,Mungu awape faraja familia yawafiwa japo wote niwafiwa,Mungu hawarani walio tupotezea ndugu zetu nakujiona wao ndio wanahaki yakuishi,Mungu walaze ndugu zetu mahali pema
 
watoa huduma za usafiri pamoja na wafanyabiashara mjini mtwara,wamesitisha kutoa huduma

hawajafunga kwa hiyari yao, ila wameshinikizwa kwani wanaogopa kuchomewa biashara zao, kama ilivyotokea mwezi mei, wale waliokaidi kutofunga biashara baadhi yao mali zao ziliporwa au kuchomwa na kuendelea kuishi kwa vitisho.
 
wakuu jf kuna taarifa nimepata kuwa mtwara leo yanafanyika maombolezo kuwakumbuka wahanga waliofariki wakati wa madai ya kudai kunufaika na gesi asilia,shughuli mbalimbali ikiwemo usafiri,masoko na maduka zimesimama, kama kuna mtu ana taarifa za kutosha kuhusu kadhia hii atuwekee hadharani tafadhali
 
Back
Top Bottom