Wasafirishaji Arusha waigomea serikali ,wasusia chakula, Mkutano wavunjika

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Wadau usafirishaji wakiwemo Madereva wa Malori Mkoani Arusha wamegomea kikao na kumemalizika bila maafikiano kutokana na kutokuelewana kati ya wadau na serikali kutokana na hoja za wadau kutaka kupewa muda zaidi ili wakaisome rasimu hiyo .

Wadau wamedai kuwa wamechelewa kupata nakala za rasimu hiyo hivyo inawawia vigumu kuijadili kwa kuwa hawajaipitia na kuelewa na hivyo kusisitiza wapewe muda zaidi .

Huku upande wa serikali ukisisitiza kuwa wanatakiwa kutoa maoni kwa kuwa tayari rasimu imeletwa kwao hivyo hawana budi kiuijadili na kuwataka watenganishe changamoto zao na utendaji kwa kuwa serikali itarejesha rasimu hiyo ili waweze kuipitia.

Kisaka, amesisitiza kwamba baadhi ya vyama vya watoa huduma walipokea rasimu hizo muda wa siku nne zilizopita kabla ya kikao hicho kulingana na kumbu kumbu zilizopo hivyo anawashangaa kudai hawajapata nakala hizo .

Mwenyekiti wa AKIBOA,Loken Masawe, akichangia ameomba wadau wa huduma ya usafirishaji kuwapa muda zaidi ili waisome rasimu hiyo wailewe waweze kutoa maoni yao ,na wasilazimishwe kwani hawana ugomvi na serikali .

Kwa upande wake mmiliki wa mabasi ya Mtei,mwenyekitio wea TABOA mkoa wa Arusha, Felix Mtei, rasimu ilichelewa kuwafikia wahusika ,wamiliki na madereva walitakiwea kufafanuliwa maeneo yanayowagusa.

Alisema kuwa kwa minajili hiyo wadau tunatakiwa walione suala hilo kwa Hivyo wanahitaji muda zaidi ili wafafanuliwe kisheria kuweza kujadili suala hilo kuweza kutoa maoni yao kuboresha rasimu hiyo kwa uwazi na muda.
 
Hii serikali ya CCM ijitafakari sana.

Wananchi wameshachoka na mengi.

Kuanzia Watumishi wa umma wanaodai kupandishwa madaraja lakini hakuna hata senti iliyoongezeka katika mishahara.

Wafanyabiashara wanalia

Wahitimu wa vyuo mbalimbali wanalia kukosa ajira

Wachuuzi pia

Yaani wanaofaidi pesa ya serikali ni walewale wachache.

Ndio maana watu wanafurahia baadhi ya matukio kama la kukamatwa kwa ndege ya Taifa.

Huwezi kuongelea uzalendo tena kwa wananchi walalahoi wa kitanzania wanaonyanyaswa na serikali yao.
 
Back
Top Bottom