Wasafirishaji Abood, Alsaid, BM, Champions na watu wa malori mjiandae kisaikolojia

Tatizo lako hutaki kufikiri nje ya box. Dunia kote treni hizi zipo hakuna usafiri wa aina nyingine? Kila mtu ana mahitaji yake. Mwingine ataona bora basi nikishuka inakuwa karibu n ninapokwenda. Usafiri wakutoka hapo aliposhuka ni rahisi kupata. Biashara itapungua km alikuwa wakifanya safari kumi zinaweza kuwa 6.
 
Tutengemee Vituo vingi vya mafuta kupunguza wafanyakazi.....

Kama biashara ya ma bus/malori itazingua hapa Tz biashara zao watazihamishia nchi nyingine
 
wenye malori wajianade.. nafikiria hawa madereva 500 watafanya kazi gani wakati vijana wanaomaliza chuo hawana cha kufanya
 
Mabadiliko chanya yote yanamadhara kwa upande mwingine...
Kama ndani ya miezi 30 ijayo tutakuwa na hiyo treni basi watu wa mabus dar Moro/Dodoma wafanye restructuring ya biashara zao.

Kama tunaenda kuwa na reli yenye Uwezo wa kubeba malaki ya Tani watu wa malori hawana jinsi zaidi ya kurestrcture biashara zao.

Ila cha ajabu Kuna watu wanadhani hizi ni story au ndoto siku wakina treni inapita kama mkuki na waliambiwa mapema utasikia maandamano ya madereva.

Ushauri boresheni huduma zenu mfano free WiFi, bei Nzuri, muanze na kutugawia soda, wanaweza kuuboresha routes za nje ya reli na tanzania itakuwa exponentially.
Kama mimi nakuja Moro kwa treni basi nakuta express ya abood au pm Moro kilosa au ifakara sio zile coaster zinazojaza masaa sita. Watu wa malori pia wajipange...
Mabadiliko hayapingwi Bali yanakumbatiwa....
Hiyo treni ya kupita kama mkuki haijazaliwa bado Tanzania.
 
Kwa hii nchi naweza kuwaambia wasiwe hata na hofu biashara itafanyika tena zaidi ya hapa.

Treni hizo zinaweza kuja zikakosa umeme au zikikwama porini mabasi yatakuwa yamepata biashara nzuri.

Mkuu, kwahio unamaanisha mabasi yatakuwa yakienda sambasamba na treni kuvizia wateja baada ya treni kuharibika maporini au?
 
Kwa kuongezea hapo mkuu, biashara ya mabasi na malori itaboreka zaidi na zaidi. Like the Maxwell's equation, wherever there is a big plus there is also a big minus and vice versa and that is life!

Licha ya hivyo pia demostiration itakuwa high spendable ukilinganisha na Simply value ambayo inapatikana kwenye huo mradi ila uzuri ni kuwa Potential za Trimland zitakuwa vizuru wiki mbili za mwanzo.

Pumbafuuuuu, ukiona tunajadiri masuala ya Nchi kaa kimya tukusaidie kesho usije vaa magunia.
 
Sisi wa Mdaula, Chalinze, Bwawani, Ubena Zamozi na maeneo mengine ya katikati bado haya mabasi tuna yahitajia ni sawa na MWENDO KASI UPO MJINI lakini daladala nazo zina saiidia.
 
Siku utakapoambiwa nauli ya Dar-Moro ni 45,000 kwa treni ndio utakapolikumbuka abood lipo wp! Nashangaa mkisema mtu alale Moro kazi afanye dar hata km abood lingekuwa linafika ndani ya saa 1 isingewezekana sababu ya gharama yake ni wachache wangemudu.
 
Treni haipiti mjini,maporini,aboud na wenzie watawapata wengi wanaoshukia njiani,au ambao watahitaji usafiri wakati treni ilishaondoka,au wale ambao hawahitaji kushushiwa treni inapoishia
 
Hiyo nauli tutambiwa ni sh.30,000/= hadi Dar toka Moro. Basi 7000/= malofa tutaendelea na mabasi yetu na coaster.
 
Amezidi abood gari mbaya analeta mbeya na nzuri dar mpaka Moro utacheck picha sasa
 
Malori na mabasi yataendelea kuwepo tuu na kufanya biashara. Marekani, China, Europe kuna matreni ya ukweli mengine yanapeba mpaka tani laki moja lakini trucks, buses zinapiga kazi kama kawaida. Treni haiwezi peleka mzigo godown, haiwezi peleka mzigo mall, mizigo inayoitaji haraka malori bado yana nafasi.....ila ni faida kwa wafanyabiashara huenda bei za usafirishaji zikapungua kutokana na ushindani.
 
Kwa safari ya treni kutoka dar mpaka moro hayo yatakuwa ni mauzauza ya dunia. Labda mpaka itapoweza kwenda mbali zaidi.
Kwa maana kama treni ina mabehewa labda 15 hivi, sasa itabidi mpaka wapatikane hao abiria wa kutosheleza ili treni isisafiri kwa hasara.
Kwa hali hiyo lazima kutakuwa na muda maalum wa treni kusafiri, hii lhuenda ikaleta tatizo kwani itapingana kidogo na ratiba za wasafiri. Mfano mtu unataka kusafiri saa 2 wakati ratiba ya treni ni saa 8, sasa kwa nini usipande basi.
 
Tatizo lako hutaki kufikiri nje ya box. Dunia kote treni hizi zipo hakuna usafiri wa aina nyingine? Kila mtu ana mahitaji yake. Mwingine ataona bora basi nikishuka inakuwa karibu n ninapokwenda. Usafiri wakutoka hapo aliposhuka ni rahisi kupata. Biashara itapungua km alikuwa wakifanya safari kumi zinaweza kuwa 6.
Hapa box halihusiki, mfanyabiasha yoyote lazima aforecast changes zozote na athari zake zote kwake.
Mfano serikali inaweza kubadili policy kuongeza lifespan ya barabara ya zake kwa sababu Kuna alternative ya cargo transportation.
Mabadiliko yoyote tena Kumbuka kutakuwa na mass transportation hivyo upungufu wa abilia kwao. Kama kwa siku abood anasafirisha bus 20 kwa siku basi zinaweza kushuka hadi kumi. Lazima kuanticipate this possibility of change
 
Kwa hii nchi naweza kuwaambia wasiwe hata na hofu biashara itafanyika tena zaidi ya hapa.

Treni hizo zinaweza kuja zikakosa umeme au zikikwama porini mabasi yatakuwa yamepata biashara nzuri.
Mfano Mzuri kwa DAR ni basi za mwendokasi....wameondoa Daladala mwendokasi wenyewe watu wanakaliana kama mizigo Abiria wanakaa vituoni masaa....
 
23 Reactions
Reply
Back
Top Bottom