Wasafirishaji Abood, Alsaid, BM, Champions na watu wa malori mjiandae kisaikolojia

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,722
Mabadiliko chanya yote yanamadhara kwa upande mwingine...
Kama ndani ya miezi 30 ijayo tutakuwa na hiyo treni basi watu wa mabus dar Moro/Dodoma wafanye restructuring ya biashara zao.

Kama tunaenda kuwa na reli yenye Uwezo wa kubeba malaki ya Tani watu wa malori hawana jinsi zaidi ya kurestrcture biashara zao.

Ila cha ajabu Kuna watu wanadhani hizi ni story au ndoto siku wakiona treni inapita kama mkuki na waliambiwa mapema utasikia maandamano ya madereva.

Ushauri boresheni huduma zenu mfano free WiFi, bei Nzuri, muanze na kutugawia soda, wanaweza kuboresha routes za nje ya reli na tanzania itakua exponentially.
Kama mimi nakuja Moro kwa treni basi nakuta express ya abood au pm Moro kilosa au ifakara sio zile coaster zinazojaza masaa sita. Watu wa malori pia wajipange...
Mabadiliko hayapingwi Bali yanakumbatiwa....
 
treni ya mwendokasi sio km unadhani za umeme ni kwamba sg ni reli yenye upana na ubora ya kufanya treni isafiri kwa mwendo zaidi kuliko na hizi za sasa hapo inategemea na aina ya treni serikali itakayo nunua. sio kwamba ni treni za umeme km ethiopia kwanza zile hazimii mataruma ya reli km hz
 
Sawa mkuu nakupata kwa hiyo watachagua walete za umeme au za mafuta?
 
Maroli ndo manini hayo... Au ulitaka sema malori... Duuh kiswahili balaa. .alafu mnataka kujua na kingereza
R na L ni janga hasa kwetu tuliokulia moyoni mwa tanzania. Asante kwa marekebisho. @mods fanyeni yenu pale heading Lori sio roli.
Rudi kwenye contents. Tunaomba mchango wako suala la lugha lisiwe kikwazo cha kubadilishana ujuzi na maoni mkuu
 
Kwa hii nchi naweza kuwaambia wasiwe hata na hofu biashara itafanyika tena zaidi ya hapa.

Treni hizo zinaweza kuja zikakosa umeme au zikikwama porini mabasi yatakuwa yamepata biashara nzuri.
Mkuu kama umewasikiliza viongozi hiyo treni inaoption zote ikitokea umeme umeleta shida inaendeshwa manually tena kwa speed Nzuri isiyo na Shaka... Ndio maana Kuna operator muda wote
 
Mkuu kama umewasikiliza viongozi hiyo treni inaoption zote ikitokea umeme umeleta shida inaendeshwa manually tena kwa speed Nzuri isiyo na Shaka... Ndio maana Kuna operator muda wote
Kusema ni rahisi kuliko kutenda ndugu,,hii ni Afrika na hao waliozungumza tunawafahamu,,waliwahi kutuletea boati ya kwenda Bagamoyo,,,speed waliyoisema mwanzo na waliponunua ilikiwa ni Mbingu na Ardhi......Hakuna jipya maneno mengi kuliko vitendo,,,,,umeambiwa hapo inaweza kuwa Treni ya Diesel....Kenya nako wamepigwa changa la macho. African leaders most are the same.
 
Angalia marudio ya uzinduzi umsikilize mkurugenzi anavyofafanua kwa mifano specifications na sifa za hiyo treni. Inaoption zote umeme ukisumbua katikati ya safari unachange mode inaendelea kama kawaida Bila umeme pia Kuna macontroller wanaoweza kuiwasha kuizima kuongeza speed hata kupunguza nje ya huyo anaeendesha na wanakuwa dsm hivyo unauhakika wa usalama muda wote
Na wewe unayetaraji kupanda treni jiandae kisaikolojia siku moja utalala porini kwa kuwa wenye treni hawajalipa bili ya umeme
 
Kusema ni rahisi kuliko kutenda ndugu,,hii ni Afrika na hao waliozungumza tunawafahamu,,waliwahi kutuletea boati ya kwenda Bagamoyo,,,speed waliyoisema mwanzo na waliponunua ilikiwa ni Mbingu na Ardhi......Hakuna jipya maneno mengi kuliko vitendo,,,,,umeambiwa hapo inaweza kuwa Treni ya Diesel....Kenya nako wamepigwa changa la macho. African leaders most are the same.
Sitofautiani na wewe mkuu, na ndio wazo la kwanza lililoingia kichwani niliposikia Ile 160-200km/hr
Nadhani kwa sababu wahusika wanajua hayo watakuwa wamejifunza maana pamoja na yote wanataka kuacha legacy.
 
Mkuu kama umewasikiliza viongozi hiyo treni inaoption zote ikitokea umeme umeleta shida inaendeshwa manually tena kwa speed Nzuri isiyo na Shaka... Ndio maana Kuna operator muda wote
Safi sana sasa nimeelewa vyema ubarikiwe sana ( ningejibiwa kwa matusi najua ila nashukuru kwa kunielewesha)
 
Back
Top Bottom