juvenile davis
JF-Expert Member
- Apr 13, 2015
- 4,752
- 4,463
Katika hali isiyo ya kawaida na ya kustaajabisha, juzi watu walisafirisha jeneza hewa wakidhani lina maiti kutokea Muhimbili hospitali hadi Lindi. Nimeshindwa kuelewa kosa ni la nani?? Ndugu au msimamizi wa mochwari maana walipofika Lindi ndipo walipogundua ya kwamba jeneza halina mtu, na hapo ni baada ya kutaka kumtoa marehemu ili wamuweke kwenye mkeka maana ni muislamu, ilibidi warudi muhimbili kumchukua huyo maiti tu na ndipo walipomkuta, sasa sijajua ni uzembe wa Nani hapo