Wasafiri zaidi ya 100 kutoka China watengwa baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege mjini Kampala kutokea nchini China

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Wasafiri zaidi ya 100 kutoka China watengwa baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege mjini Kampala kutokea nchini China.

Mamlaka ya uwanja wa ndege huo nchini Uganda umefahamisha kuwa uamuzi huo umechukuliwa kutokana na virusi vya corona kuathiri binadamu na kusababisha maada kwa muda mfupi kwa mtu alieambukiwa.

Mwishoni mwa mwaka 2019, China ilitangaza kugundua virusi vipya vya corona aina ya nCoV katika jimbo la Wuhan.

Ulimwengu mzima ulichukuwa tahadhari na kuanza mikakati ya kukabiliana na maambukizi mapya ya virusi hivyo.

Waziri wa afya wa Uganda Dr. Jane Aceng amezungumza na wanahabari na kuwafahamisha kuwa watu 100 kutoka nchini China wametengwa kiafya na wasalia katika uchunguzi wa kiafya kwa muda wa siku 14 katika hospitali tofauti.
Waziri wa afya huyo amesema kwamba miongoni mwa watu waliotengwa wamo raia 44 wa China.

Kwa uapnde mwingine, raia mmoja wa Argentina na mwengine wa China wametengwa kwa ajili ya uchunguzi wa afya nchini Gana.
 
Hii ngoma ikiingia EA twafa tu! Nzige nao bado wana trend EA..! Tumuombe tu Mungu ataulinde na kutuepusha..
 
Back
Top Bottom