#COVID19 Wasafiri wakamatwa Uganda wakiwa na vyeti bandia vya Covid-19

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,862
Wasafiri


Maafisa polisi katika uwanja wa ndege wa Entebbe nchini Uganda, leo wamewakamata wasafiri 23 waliowasili katika uwanja huo wakiwa na vyeti bandia vinavyoonesha kwamba hawana maambukizi ya virusi vya corona.

Washukiwa hao ni pamoja na wanaume 13 na wanawake 10 ambao wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Entebbe.
Patrick Onyango, msemaji wa eneo hilo anasema washukiwa hao watashtakiwa kwa undanganyifu na umiliki wa vyeti bandia.

Bwana Onyango amesema timu ya usalama inachunguza washukiwa hao ili kupata taarifa zaidi. Wasafiri wote wanaopitia uwanja wa ndege wa Entebbe wanahitajika kuwa na vyeti vinavyoonesha wamepimwa virusi vya corona ndani ya saa 120 na imethibitishwa kwamba hawana maambukizi kabla ya muda wao wa kusafiri huku abiria wanaoingia nchini humo wakistahili kuonesha cheti kinachothibitisha wamepimwa virus hivyo ndani ya 72 na kuwa hawana maambukizi kabla ya safari yao.

Miongozi mipya imeanza kutekelezwa Oktoba 1, 2020 baada ya serikali kufungua tena uwanja wa ndege wa Entebbe kwa ajili ya safari za kibiashara baada ya kufungwa kwa miezi sita.
 
Back
Top Bottom