MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,640
2,000

Download
720

Waziri wa Afya anatakiwa kubadilisha utaratibu mbaya unaofanywa Mjini Dares-Salaam Airport. kuhusu Wageni ama sivyo Mwaka huu Tanzania itakosa wageni wengi na pato la Taifa kuhus wageni litashuka. Sikiliza hiyo video.

====

WASAFIRI katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, wamelalamikia utaratibu mbovu uliopo katika kupata namba, kulipia na kupimwa corona kwa wasafiri wanaowasili nchini kutoka nchi mbalimbali.

Hali hiyo ambayo imekuwa ikijirudia kwa wasafiri wapya imekua kero kiasi cha baadhi kuachwa na ndege, kukaa zaidi ya saa tatu hadi nne bila huduma, na mtandao kutokufanyakazi, jambo ambalo limekuwa likijirudia.

Aidha, muda mwingi wasafiri wanautumia kusubiri utaratibu wa kupata namba ya kulipia, kulipia na kupata fomu ya kuruhusiwa kwenda kupima.

Mathalani, msafiri aliyewasili na Ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia, ambayo inatua saa 8:40 usiku, aliondoa uwanjani humo saa 11 alfajiri.

Hata hivyo, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imethibitisha kupokea malalamiko ya wasafiri na kufafanua hali hiyo ilisababishwa na maboresho yanayofanyika kwenye kulipia mtandaoni na kukosekana mtandao.

HALI ILIVYOKUWA JUZI

Majira ya saa nane usiku hadi saa 10 ziliwasili ndege nne ambazo ni Ndege ya Shirika la Ndege Ethiopia, Shirika la Ndege la Kenya, (KQ), Shirika la Ndege la Egyp na Shirika la Ndege la Uturuki, kila mmoja likiwa na abiria wengi.

Abiria hao walitakiwa kupanga foleni huku wakiingia kwenye mfumo wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto uitwao Afya Msafiri kwa ajili ya kujaza fomu na kupata namba maalum ya malipo.

HAKUNA UTARATIBU

Katika eneo hilo kuna wahudumu watatu ambao anahudumia abiria wote (wastani wa watu 500) waliopanga foleni ambao wanatakiwa kuwa na namba ya kulipia ambayo lazima ihakikiwe ndipo msafiri aruhusiwe kwenda kupima.

Aidha, abiria wote wenye watoto, wajawazito, wenye ulemavu, aliokaa kwenye viti mwendo, wazee, wagonjwa na wazima wanapanga foleni moja, huku kutokana matatizo ya mtandao wanasimama kwa muda mrefu.

“Nimewasili na Ndege ya Ethiopia tangu saa nane kasoro na nimesimama kwenye foleni kwa zaidi ya saa mbili bila huduma, wanasema hakuna mtandao wa kuhakikisha kama namba ya kulipia niliyopata ni sahihi, lakini hakuna utaratibu sasa kila mtu anapita atakavyo, hakuna matangazo juu ya utaratibu kiasi sasa cha kuwa mwenye nguvu apite,”alisema mmoja wa wasafiri.

“Kama unavyoona ndege nyingine imewasili na abiria waongezeka na wote tunasubiri huduma hii, huu utaratibu unaumiza wengi, na sasa tunaelezwa mtandao haufanyikazi,”alisema.

MTANDAO KUSUMBUA

Kwa mujibu wa msafiri huyo, mara baada ya kukaa kwa saa mbili ndiyo alipata huduma ya namba kuangaliwa kuwa iko sawa baada ya mtandao kurejea, na alipofika pa kulipia alishindwa kufanya hivyo kutokana na mtandao.

Aidha, wasafiri waliokuwa wanalipia kwa kadi za VISA alishindwa kufanya hivyo na hata waliosimama kwenye dirisha la benki inayotoa huduma eneo hilo alishindwa kupata huduma na kulazimika kusubiri kwa saa moja nyingine.

Aidha, wasafiri wengi walijaziwa fomu za malipo kwa mkono kwa madai mtandao hauwezi kutoa nakala ya fomu ambayo mteja anatakiwa kupewa.

Mara baada ya kulipia msafiri anatakiwa kwenda kwa wahudumu wa afya, ambao humjazia fomu maalum ya kumruhusu kwenda kupima ambako napo kulikuwa na tatizo la mtandao.

UPIMAJI

Aidha, upimaji unafanyika kwa haraka kwa kuwa hakuna foleni na ndani ya dakika 10 msafiri anapewa majibu yake.

WANAOBADILI NDEGE

Baadhi ya wasafiri ambao walikuwa anabadili ndege walijikuta wakitumia muda mwingi kwenye utaratibu huo na baadhi kushindwa kuwahi ndege za ndani za kuelekea Arusha, Mwanza na Kigoma.

“Naombeni mnihudumie muda wa ndege yangu umeshafika, nitachwa ninakwenda Mwanza na muda wa kuingia umeshafika,” alisikika abiria mmoja akilalamika, lakini kutokana na wingi wa abiria alijikuta kwenye foleni na kuambiwa kuwa mtandao haufanyikazi ambaye baadaye aliachwa na ndege yake.

UCHACHE WA WAHUDUMU

Katika eneo hilo kulikuwa na wahudumu watatu ambao wanaangalia namba na pasi za kusafiria za wasafiri kabla ya kuwaruhusu kulipia.

Aidha, baada ya kulipia wasafiri wanatakia kujaziwa fomu kwenye kompyuta na kisha kusubiri nakala lakini kutokana na kukosekana mtandao alijaziwa kwa mkono.

Katika eneo hilo daftari linalotumika ni moja kurekodi taarifa za wasafiri na kuwapa namba za kwenda kupima, ambao hutumia chini ya dakika tano kupimwa na kupata majibu, na baadaye kwenda kuvuka mpaka ili kuchukua mizigo.

UFAFANUZI WA WIZARA

Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu, Mkurugenzi wa huduma za kinga, Dk. Leonard Subi, alisema changamoto zilizojitokeza juzi ni kutokana na mtandao, na kwamba wamefanya mabadiliko ya mtandao ili msafiri aweze kujaza fomu na kulipa kabla ya kufika nchini.

“Tumepokea malalamiko ya kilichotokea jana (juzi) usiku kuwa ziliwasili ndege nne kwa wakati unaofuatana na kulikuwa na shida ya mtandao kuanzia kwenye kuhakikisha namba ya malipo, malipo na kujaza fomu, tumechukua hatua,”alisema.

Dk. Subi alisema kwa mtandao uliobadilishwa inatakiwa safiri kukamilisha utaratibu wote ndani ya dakika 10 hadi 15, lakini kwa kuwa tupo kwenye kipindi cha mpito ndiyo maana usumbufu ulijitokeza.

Aidha, alisema serikali ilianzisha utaratibu wa kupima tena mara msafiri anapowasili kutokana na kuwepo vyeti vya COVID-19 vya kughushi huku wengine wakipata maambukizi wakiwa safarini na kuingiza nchini.

“Kipimo tunachotumia sasa kinaonyesha majibu kwa muda mfupi na hata kama amepata maambukizi ndani ya saa mbili au tatu zilizopita tunambaini. Hii ndiyo namna ya kudhibiti maambukizi yasiingie nchini,”alisema Dk. Subi.

GHARAMA ZA KUPIMA

Kwa mujibu wa utaratibu wa sasa msafiri yeyote anatakiwa kujaza fomu ya kuomba kupima Corona mtandaoni, kisha kwenda kwenye hospitali au kituo husika na kupima.

Gharama za malipo ni Dola za Marekani 100 (sawa na Sh. 230,000 ), Sh. 10,000 ya Hospitali au kituo ulichopimiwa na siku ya kurudi au kuingia nchini unatakiwa kulipa Dola 25 (sawa na Sh. 57,750)
 
Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
654
1,000
Na Mwandishi wetu

Wasafiri katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, wamelalamikia utaratibu mbovu uliopo katika kupata namba, kulipia na kupimwa corona kwa wasafiri wanaowasili nchini kutoka nchi mbalimbali.

Chanzo: Nipashe
 
mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
8,881
2,000
View attachment 1812535

Acha wasumbuke tu wameyataka wenyewe!!
 
MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,640
2,000
Acha wasumbuke tu wameyataka wenyewe!!
Kwa sababu ya wwe hausafiri ndio maana unasema wacha wasumbuke?Wanao kujna ni Watalii wengi wao wataacha kuja kwa ajili ya huo usumbufu wa Uwanja wandege wa Dares-Salaam.Halafu Serikali itakosa pesaza Utalii.
 
Ngariba1

JF-Expert Member
Jan 12, 2017
1,183
2,000
Nimeshuhudia hali hiyo wiki 2 zilizopita. Ni kero isiyo ya kawaida.
 
Root

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
40,989
2,000
Hapo Wizara ya Afya inavuna mahela, hebu fikiria 230,000 kwa watu 10000 ni kama 2.3bil
 
Smart911

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
65,648
2,000
Hayo mambo ya network ipo down ni kama wimbo wa Taifa hapa nchini...
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom