Wasafiri muwe makini na wizi huu wa kwenye mabasi

mustry75

Member
Sep 23, 2014
82
89
Habari za muda huu wakuu wa JF,

Leo nimekutana na huu wizi ambao si mpya ila umeanza kurudi, vijana umakini unahitajika mnapokuwa safarini hasa mabasi ya mikoani yanayo chukua abiria,

Leo nilifanya safari ya kuenda Tanga na basi la Tash Riff ya jioni ndani ya basi kulikuwa na abiria wengi kama ilivyo kawaida watu wana panda na kushuka kigiza kinaingia.

Mpaka tuna fika maemeo ya kange akashuka kaka mmoja na dada mmoja, wakati wanashuka kuna dada akapiga kelele ya mwizi kumpigia yule kaka lakini yule dada Alikuwa kachoka watu wakamkimbilizia yule kaka wakakuta kachukua simu smart phone ya yule dada then wakamuachia kwakua ni usiku kama saa 2 safari ikaendelea yule dada akiulizwa anasema alimpa arushe salio mara akasinzia, nikama alie mpa dawa ya usingizi ila alikuwa haija mkaa sawa akashtuka,

Safari tukaenda tulipo fika mjini sasa tunashuka ile siti alio kaa yule dada kuna kijana wa makamo. Like 26 au 28 yaani yuko hoi nizaidi ya usingizi tumeamsha abiria wote yaani nikaput hatari yaani hajiwezi yuko usingizini. Chakusikitisha yule dada amemuibia kila kitu na alikuwa na simu kubwa yule kijana kwakweli sijui walimpeleka wapi maana watu walishuka wote kila anavyo amshwa hawez kunyanyua kope yuko hoi.

Zingatio:

Unapo safiri ukikaa siti na dada au kaka hata awe mzuri kama nani zaidi ya salamu usijenge mazoea yatawakuta mabaya kwa Tanga nasikia haya ni matukio yakawaida sasa ila mjifunze kujikaza mtaibiwa mpaka soksi.
 
sasa hapo haieleweki hiyo dawa wanaitumiaje mana unaweza kua unapumua Jamaica kumbe ndo unauvuta, kuna haja ya kuweka chumba cha kukagulia abilia wote kabla hawajapanda mabasi
 
Ile sijui dawa sio mpaka akupe pipi wala nini, sometimes anaweza kuwa kama anamfukuza inzi ivi kwa kitambaa kumbe loh.
 
Ile sijui dawa sio mpaka akupe pipi wala nn, sometimes anaweza kuwa kama anamfukuza inzi ivi kwa kitambaa kumbe loh...!!
 
Hata mimi sijaelewa yupi ni nani! Mwizi ni kaka aiyeshukia Kange au aliyebakia( dada)
Mkuu mimi nilivyoelewa hapa kuna wezi wawili, wakwanza ni yule kaka aliyeshukia Kange alimuibia yule dada akapiga kelele,, wapili ni huyu dada alipoibiwa akalipa kisasi kwa kumuibia yule kaka wa mwisho aliyelala fofofo.
 
Back
Top Bottom