Wasafiri msaada juu ya Mtanzania anayesafiri kwenye nchi zilizo katika orodha ya visa free

Umenena vyema na siwezi kuongeza chochote. Nami pia walinisumbua wakati narudi Singapore nikitokea Malaysia pale Johor Baru lakini yule mzee wa immigration alikuwa fare sana.

Alikuwa ‘ fare’ sana, maana yake alikuwa ‘nauli’ sana. Haa! Ndiyo maana huwa mnabanwa mbavu sana aisee! Kwa kiingereza hicho!!!
 
Kwa SA una free visa ila changamoto ni kuwa jamaa wanataka rushwa hasa mipakani pia kwenye hizo siku tisini wanaweza kukipa siku 14 tu ukitaka zaidi uwape hela ukimkuta mgonga mhuri ni mzungu tegemea maswali kadhaa tofauti na weusi
 
Sasa hivi na hii ishu ya Corona mambo ya kupima kwa wakati au kuwa na chanjo inaonekana ni moja ya kigezo kikuu kuingia Nchi hizo..ngoja nianze kwa SA wao ukipima tuu Tanzania ukafika Oliver Tambo ukiwa na cheti ambacho akijapita masaa 72 nadhani ukifika kwa uhamiaji wao wanakuuliza hicho cheti unapewa siku 90...kwa Hong Kong huo mji ni wa kibiashara tuna siku 90 za kupewa ukiingia tuu ila kutokana na Watanzania kuharibu hasa wauza sembe na wengine wakiingia hawatoki wamekua na maswali mengi mno kuhusu kiasi cha pesa unaenda kununua nini na utafikia wapi hayo maswali unaulizwa kabla hujamfikia mgonga mihuri ugongewe wakiona hueleweki na kwa kuwa una tiketi ya kurudi utarudi na ndege uliyokuja nayo hata kwa kuzuiliwa hapo hapo airport siku kadhaa wamedundisha sana watu...ila ukiingia pako poa kwa Singapore hao ndio watata kuliko hata Hong kong hao singasinga mnafanyiwa interview wote hata Mmarekani wanampiga maswali wakiina hawamuelewi wanamridisha ila ni mara chache mno...Thailand ni visa kupo vizuri ukiweza chukua visa..Vietnam ni visa ila Cambodia sio visa hizo nchi unaweza kuzizarau ila wapo Wageni wanapiga maisha hapo maana ni Nchi zenye viwanda vingi na bidhaa zake soko lake kubwa ni Afrika,Ulaya na China...swala fanya utoke Afrika ukifika huko maujanja ya kuishi utakutana nayo huko huko hakuna kitu kigumu.
Unaizungumziaje Singapore katika suala la fursa za ajira skilled/unskilled jobs utaratibu wa kupata kazi/sheria zao??
 
Mara nyingi ukienda kwenye Visa free countries wanaangalia sana kama una ticket ya kurudi ndani ya zile siku za free, pia proof of residence kama hotel nk, pia wanaweza kuuliza purpose ya visit yako na wakaomba vitambulisho kama itaonekana haujielezi vizuri.

Bahati nzuri mie almost nchi zote nilizowahi kwenda ambazo ni Visa free nimekuwa nikitoa passport wanauliza return ticket basi nagongewa visa fsta, labda kidogo Malaysia ndio waliniuliza vimaswali kadhaa na nilikuwa na jamaa alisahau kuniambia hotel aliyonichukulia nikawa nahangaika kumpigia Ila aliwaambia wakaconfirn Sheraton ya Subang province west Java.

Mostly ukienda kwa kaunta anamuangalia kama upo suspicious, muonekano wa nje inasaidia sana pia, unakuta kijana kavaa microphone anatafunatafuna big G, haujielezi purpose na hana hela au residence ni zile za uswekeni aisee wanakudetain kwanza wakuhoji vizuri.

Ukishindwa kutoa majibu yanayoeleweka safari unaishia hapo next flight wanakutua DSM
Hivi mkuu kaunta za bongo hawakusumbui kwenda hizo nchi bila visa?
 
Mkuu mfano kwa singapore ambapo ni visa free naweza kwenda ubalozini kwao nikagongewa ingali nikiwa bado nipo bongo..kuliko.kwenda na kurudishwa airport?
Mkuu hili swali sikuliona Ubalozi wa Nchi ambayo ni Visa free unaweza kwenda kuomba kibali kama cha kusoma,kufanya kazi ila matembezi utapewa pale pale Airport vigezo vyao ni rahisi lipia hotel ya bei rahisi ukiwa Tanzania na uwe na show money hata 4000 usd na pia ukiwa na kadi za Bank za Tanzania unawaambia hela zipo humu hakuna ofisa ambae atataka mkakague pesa zako Bank watakugongea tuu..
 
Back
Top Bottom