Wasafi Media na anguko la East Africa Radio

mayowela

JF-Expert Member
Nov 2, 2014
2,124
1,744
Hii wiki imeanza kwa kishindo upande wa Kiwanda cha media baada ya Wasafi Fm kufanya utambulisho wa watangazaji wa kipindi cha michezo cha Sport Arena, utambulisho uliojaa manjonjo na mbwe huku wakiwa wameacha vilio na mapengo kwenye baadhi ya vyombo vya habari,

Biashara ni Ushindani, eeeh ndio ushindani, naona yale yaliyofanyika kwa Clouds kuiba watangazaji wa EA Radio, na EFM kuiba kwa sasa naona yakitokea tena, issue kubwa ni dau, sehemu yoyote ukitangaza Dau mtu hufanya kwa kiwango cha juu sana plus taaluma na uzoefu,

Biashara ya media inabebwa na matangazo, matangazo nayo yanaangalia vipindi gani hupendwa na wasikilizaji, wasikilizaji nao huangalia kipindi kinaendeshwa na nani, ndiomaana tunaona wenye majina makubwa ndio wanufaika,

kuna watangazaji wadogo lakini wanauwezo mkubwa sana na wako mikoani au media kubwa Dar ila nafasi hawapewi, na kuna watangazaji wakubwa wanamajina ila maslah madogo sasa hapa ndio tunaona wenye upeo na biashara hucheza karata vizuri,

EA Radio kwenye usajili au nyakua nyakua, waliwapoteza Mammy Babby, Bantu, Kennedy, Sinyorita, na Ommy Crazy
hapo nyuma walishawapoteza Seba the warrior, Marygoreth Richard, nk
Mafuvu
pia walikosa kwa sababu zao binafsi

sasa kwenye usajili wa WASAFI fm katika kujitangaza na kujiboresha na kuteka hisia za watu, naona wafuatao wanaondoka,
Jr Junior, King Smash, Sam Misago pia kuna tetesi za watu wa team ya tv production kubebwa,

Hili litaleta anguko la pili baada ya lile la kwanza ambalo walipoteza sana mvuto kwa wasikilizaji na ikabaki ufanyaji wa kazi kwa mazoea bila initiative/strategy, pigo walilopigwa kuondoka Zembwela ni kubwa Supa Mix ndio basi tena, au wataendelea kuwazalishia watangazaji wazuri washindani wao..?
 
Sioni sababu ya kuendelea kunyang'anyana wazee kama kina Kitenge et.al wakati kuna young talents nyingi na zinafanya vizuri mnoo...
Ni kukosa ubunifu tu na kutojiamini.

Kwa hili Wasafi wamechemka sana..

Ilibidi kama kituo kipya kipike watu wake ..wapya.

Hovyoo kabisa.
 
Mimi pale EA RADIO hata aondoke nani, nitadumu kuwa msikilizaji wao.

Kuna vichwa mwanzo viliondoka bwana, achana na kina zembwela hawa.

Mwanzo mpaka nikawa nasema, nini hiki? Lakini mpaka leo EA RADIO wako imara.

DJ Mafuvu alipotoweka pale mjengoni, nikadhani pengo halitazibika, kumbe nilikuwa nadhani uongo, mpaka leo pengo lake limeshazibwa.

Haya, kuna yule dada aliyeko CLOUDS, nilidhani pengo lake halizibiki, lakini mpaka hapa pengo lake limezibwa, n.k n.k...
Ea Radio kile ni kiwanda, kila siku kinafyatua vichwa vipya.

Kwahiyo hao kina nani sijui wewe waache waende, lakini mimi na EA RADIO, Sijui aondoke nani pale ndipo niache kuisikiliza
 
Tena sana
Sioni sababu ya kuendelea kunyang'anyana wazee kama kina Kitenge et.al wakati kuna young talents nyingi na zinafanya vizuri mnoo...
Ni kukosa ubunifu tu na kutojiamini.

Kwa hili Wasafi wamechemka sana..

Ilibidi kama kituo kipya kipike watu wake ..wapya.

Hovyoo kabisa.
 
Yaani karahisi tu unatamba east africa kuanguka pengine mgeni wewe kile kituo achana nacho kitabaki milele na uibuaji wa vipaji clouds na mbwembwe zote east africa tv na radio vipo palepale hata aondoke nani ile station ni moto sana ina misingi yake haikuanza leo wala jana

East africa tv na radio vitabaki juu daima usiteme bigijiii kwa karanga za kuonjeshwa
 
Tz tukiwa na magenious wengi kama Diamond tutakua mbali sana.
Idea ya Wasafi imegeuka ajira na industry kubwa sana.
Haya mapinduzi anayofanya huyu ndugu yetu tena bila kugeuza usogo ni makubwa na yamepitilizaa
yaani kila mtangazaji kwa sasa moyo wake mguu ndani mguu nje, pesa haina adabu
 
Back
Top Bottom