Wasaaniii wetu na shoo za nje | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wasaaniii wetu na shoo za nje

Discussion in 'Entertainment' started by Fredwash, Jan 25, 2010.

 1. Fredwash

  Fredwash JF-Expert Member

  #1
  Jan 25, 2010
  Joined: Oct 27, 2009
  Messages: 593
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 60
  Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita wimbi la wasaniii wetu wa nyumabani wa bongo kuanza kwenda ulaya kwa kile kinachoitwa kwenda kufanya shoo (wenyewe eti wanaita WORLD TOUR) wasaniii kibao wamekwenda nchi mbali mbali wengine wakitengeneza link (kwenda zaidi ya nchi mbili katika safari moja)

  SASA BASI.........

  katika hizi tour zao za kwenda kufanya shoo tumeshuhudia mengi yakisemwa kutoka kwa wadau wa mziki huu( wasanii wenyewe , mashabiki na wengine wahusika) kuwa shoo hizo sio kama vile zinavyotangazwa , na hazina manufaa makubwa kwa msanii binafsi. wengine wakisema ni bora ya shoo za hapa ndani kuliko hata hizo zinazoitwa za ulaya....


  TUmesikia na wasanii wengine wakijiapiza kutokwenda tena kweney hizo shoo mbuzi, wengine wakilalamika kunyonywa... Ukweli unaosewma ni kuwa hizo zinazoitwa shoo ambazo vyombo vya habari vya burudani ndio vinavyolaumiwa kwa kuwapotosha watu na kuwapoteza wasanii kwa kuzitangaza utadhani ni shoo inayokusanya watu walau elfu moja... Eti ni shoo ambazo watu (wajanja) hasa watanzania wachache waishio huku magharibi kuamua kuchangishana pesa na kumleta msanii flani huku wakimgharamia viza malazi na chakula kwasiku zote atakazokuwa huku (na viza yenyewe inasadikika ni kuwa ni ya mualiko wa matembezi na sio ya kuwa anakwenda kikazi) huku yeye mwenyewe akipewa pesa ya shoo isiyozidi pesa ya kitanzania laki tano.... ama basi walau ikifika milioni ujue kafanya shoo zaidi ya nne......

  Kikubwa kinachosemwa hao wajanja wanachokifanya wakishakubaliana na msaniii kupitia jamaa zao walioko huku... huanza kualikana au kutengeneza matangazo ya shoo na kuanza kutangaza kwenye kilasehem ambazo mtanzania ( na hata watu wote wa East africa ) kuwa flani atakuja kuperfom.. huku wao wakitumia eneo flani la nyumba ya mtu au kajiukumbi kadogo ambacho hakibebi hata zaidi ya wato 200... kuwa ndio sehem ya shoo...

  hawa jamaa wao wanafaidika kwa kulipisha watu viiingilio... YAANI NI KAMA HIZI SHOO TULIZOZIZOEA KUZIONA HUKU MTAAANI KWNEYE VIJIUKUMBI VYA BAAA KWA KIINGILIO CHA 3000 au 2000...na wengine hualikwa kwenye sherehe za birthday au harusi tu kuperfom...


  SWALI na HOJA

  Je kuna ulazima wa wasaaniii wetu kuanza kuwa strictly kidogo ikiwa wanataka kupiga hatua zaidi kwa kuwa wa wazi na kuthami kazi yao pia... yaani aende akaimbe kwenye kijiukumbu kilicho na watu thelathini kwa kutumia mult player ya deck moja au tatu za CD... kisa yuko ulaya?.....


  haileti picha kutangaza onyesho utdhani anakwenda kuperfom wembley kumbe jamaa wachache wamemleta kama mgeni wao .. then wanachuma pesa kupitia wao..

  JAMANI LEO SIKO VIZURI ILE NIMEONA NILETE HII CHALLENGE... mtanisamehe kwa uandishi mbovu ila naamini hoja imeeleweka

  MFANO ANGALIA VIDEO ILIYOREKODIWA HIVI KARIBUNI ALI KIBA AKIPERFOM HUKO UK... yaani ni kama kijiukumbi flani cha jengo la kanisa tuseme huku huyo so called DJ akiwa na redio ya mult system anamuwekewa plyaback zake ...yaani u cant jkust be serious and call that a SHOW?.... goosh

  HTML:
  <"http://www.youtube.com/v/-IY02Wq8YnA&color1=0xb1b1b1&color2=0xcfcfcf&hl=en_US&feature=player_embedded&fs=1">
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Jan 25, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Wajinga ndio waliwao....Hawajui thamani ya talent zao!

  Utaendaje mahali hujui hata regulations za perfomances za namna hiyo zinakuwaje?

  Kibri kinawatesa hawa...wakisikia ni ulaya tu..basi wako tayari kwenda hata kwa kulipiwa nauli na hela ya kula..damn them!
   
Loading...