WilsonMwalukasa
Member
- Dec 26, 2021
- 33
- 23
Habari zenu.
Swala la elimu nchini Tanzania, ni swala ambalo wanasiasa wengi nchini iwe chama tawala na hata vyama pinzani kiujumla Kwa pamoja wameshindwa kuona kama ni miongoni mwa kikwazo Cha maendeleo nchini.
Serikali imekuwa ikipanga malengo na maono makubwa, ambayo ni tofauti na aina ya elimu na mitaala iliyopo nchini.
Mipango ya serikali haiwiani na sera zetu za elimu, aina ya elimu na mitaala ya elimu nchini.
Serikali inasema wahitimu wa vyuo wajiajiri, lakini je elimu waliopewa vyuoni ni ya kuwawezesha wao wajiajiri? Umesoma nadharia za Entrepreneurship chuoni, ukihitimu practical unakuja kufanya mtaani.
Hiyo ni dhahiri kuwa malengo na maono ya serikali juu ya wahitimu haiendani na maandalizi yaliyo fanyika Kwa wahitimu wake.
Serikali kupitia wizara ya elimu imepanda mihogo na inategemea kuvuna mahindi.
Aina ya elimu na mitaala katika taifa letu bado ni changanoto, tuna-andaliwa Kwa elimu ya kukalili na sio kukufikirisha.
Ukiwa una uwezo mkubwa was kukalili elimu ya Tanzania ni rahisi sana.
Ndio maana wasomi au wakufunzi wetu, ni ngumu kuwa creative maana ili uwe creative inabidi uweze kufikiri.
Kuna taaluma nchini kama Civil Engineering, ni ngumu kukuta Engineer aliyehitimu UDSM au Ardhi au MUST Mbeya kwenda nje ya misaafu yake kama British Standard BS, maana elimu yetu haijatufunza kufikiri imetufunza kukalili.
Vyama pinzani wamekosea sana kuanza kudai Katiba Mpya, walipaswa kudai mabadiliko ya Elimu (Education Reforms). Endapo elimu na mitaala yake ikibadilika tutapata elite citizens, ambao wenyewe watakuja kudai mabadiliko ya katiba endapo wakiona Ina kasoro.
Natoa Rai Kwa watanzania wenzangu, tudai mabadiliko ya Elimu kwanza. Na ndio kiwe kipaumbele chetu.
Maendeleo ya Taifa hutegemea wananchi wake, na wananchi waweze kuwa chachu ya maendeleo ya nchi yao nao hutegemea wameandaliwa katika elimu ya aina gani.
Tunaweza pata mifano Kwa mataifa ambayo, yaliwekeza kwenye elimu na yakaweza kupata maendeleo ndani ya muda mfupi mfano ni zile nchi za Southern Tigers.
Nawasihi watanzania wenzangu, tupaze sauti tufanye mabadiliko ya mitaala yeti nchini, tuachane na elimu ya urithi kutoka kwa mkoloni. Asanteni.