Was Zitto Wrong? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Was Zitto Wrong?

Discussion in 'Great Thinkers' started by Zitto, Oct 1, 2007.

 1. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #1
  Oct 1, 2007
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Was Zitto wrong?

  By Sunday Citizen Team

   
 2. Dua

  Dua JF-Expert Member

  #2
  Oct 1, 2007
  Joined: Nov 14, 2006
  Messages: 2,481
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Hukuwa wrong Zito ni aibu kwa taifa kama letu lenye utajiri wa kila aina, lakini tunaambiwa rais anatembea kwenda kujiuza kwa mataifa makubwa ili waweze kutusaidia.
  Kwa ajili ya mafisadi. Tulikuwa tunawalaumu watemi kwa kuuza wenzao utumwa kwa sukari leo hii tunashuhudia malaya wanaokwenda kujiuza kwa peremende.
   
 3. K

  Koba JF-Expert Member

  #3
  Oct 1, 2007
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  ....yaani 30% corporate tax haijalipwa for 5 yrs an the reason behind "HEAVY LOSSES" na wala sio ile Tax holiday...sometimes najuliza ni rushwa au incompetence ya hawa viongozi lakini sipati jibu au labda tuna wrong information sisi lakini NO kuna ufisadi wa hali ya juu hapo ambao wanatumia loopholes kisheria zilizomo katika hiyo mikataba inayosainiwa na incompetents the like of Karamagis...angalia Sheraton walivyocheza deal chafu na wameondoka bila hata kulipa ndululu na wakibadilisha jina tuu kumbe same guys ....too bad tuna viongozi wajinga na hao investor wanatumia hiyo weakness.
   
 4. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #4
  Oct 1, 2007
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Mimi ingawa nai support CCM, lakini baadhi ya viongozi wetu kweli wanaboa sana!

  Damn!
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Oct 1, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kuna mtu alitakiwa afungiwe kuhudhuria vikao vya Bunge but I doubt it kwamba alikuwa Zitto...
   
 6. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #6
  Oct 1, 2007
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Mheshimiwa Zitto,

  Heshima mbele mkuu, now kama nime-read vizuri betweeen the lines, hii ndio in general your charge against Waziri Karamagi:-

  Na katika charge yako, ulifanya makosa yafuatayo:-

  Sasa mkuu wangu I have a lot of respect na jinsi ulivyoisimamia hii ishu bungeni, lakini I must admit kuwa sikuwa na hizi facts ulizozileta hapa kwenye hii article,

  Now honestly, ninakuomba unisaidie kuelewa ni nini legal ramifications za bunge kwa mbunge yoyote yule kwa ajili ya some technical mistake katika charge yako as pointed hapo juu.

  Maana sitaki kuamini kuwa ni big enough as far as the bunge letu sherias are concerned, kwamba wanaweza kuwa justified kukataa kuunda kamati ya uchunguzi wa madai yako, to the point ya kuwa pia justified legally kukufukuza bungeni,

  Tafadhali sana ninakuomba uambatanishe majibu yako na sheria za bunge letu na applications zake kwenye hii ishu yako ikiwezekana mkuu, otherwise heshima mbele mkuu kwa kujitolea kuja hapa always kutuweka sawa na yanayojiri huko ground zero!

  Ahsante Mheshimiwa.
   
 7. Gigo

  Gigo JF-Expert Member

  #7
  Oct 1, 2007
  Joined: Aug 6, 2006
  Messages: 455
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Nilikua sijui Kama Zitto ni mwenzetu Humu Kwenye Jumba letu La Jambo F...Usiache
  Mi Mina penda Kuku ambia Zitto Jambo moja ...
  Naona Kama Una Jizolea Umaarufu Peke yako Bala Kuhusisha Maisha yako asilia...Ni-vizuri Ukimtambulisha Mchumba wako!!au Mke wako..

  Ni vizuri Kufanya hivyo mapema!!Ili tuende Tukijua Maisha yako vizuri..Hata Tutakapo kuchagua Kama Raisi Tuwe tunajua Mambo Hayo..mapema!! sio kama viongozi wetu wa CCM- Hata hawafahamiki vizuri!!-Kazi kujua walizalia na watu wa kawaida hapa Duniani.


  Jitahidi sana kuikosoa Serikari- Na siasa yako ni Kukosoa serikari..Mpinzani simama hivyo hivyo- lakini usije Ukakosea hata siku moja Uka isifia serikari...
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Oct 1, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  FMES.. hicho unachosema ni kweli kwani kama Zitto alikosea nukuu au mwaka the same standard should be applied to Mramba ambaye inasemwa kuwa
  Sijui kama Zitto aliadhibiwa kwa "uongo" huu though.. Nafikiri ilikuwa ni issue ya yeye kusema Karamagi alidanganya Bunge.. which I think ni kweli ukisoma vizuri hapo juu.
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Oct 1, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Anzisha kule kwenye mada ya mapenzi or something, watu wanajadili vitu muhimu...mambo ya Mchumba ake fulani ni nani yanahusiana vipi ni income tax? Wakati mwingine tumia njia nyingine kubadili mjadala.
   
 10. K

  Katibu Tarafa JF-Expert Member

  #10
  Oct 1, 2007
  Joined: Feb 16, 2007
  Messages: 980
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Jamani hawa matapeli tuwafanye nini ?maneno matupu hayavunji mfupa.inabidi tufike mahali sasa tuyarekebishe haya.nchi imekuwa kama danguro kila kiongozi analinda maslahi yake na kuwacha wananchi ktk lindi la ufukara..sasa imetosha tunaitaji mapinduzi ya kweli dhidi ya viongozi wabadhirifu na wafujaji wa mali ya watanzania.
   
 11. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #11
  Oct 1, 2007
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0


  Mkuu wangu MMJ,

  Ninakusikia mkuu na you are very right, nia na madhumuni yangu kumuomba mheshimiwa Zitto, amwage vitu zaidi ni kutaka kujua tu kama sheria za bunge zinakuwa applied namna gani kwenye hizi ishus, maana sitaki kuamini kuwa Spika Sitta na wenzake walikuwa right kumfukuza bungeni,

  maana wanaweza kulilia kuwa wako justified kutokana na hayo makosa ambayo kwangu mimi ni madogo sana, lakini siwezi kuhukumu how much weight they carry as far as sheria za bunge is concerned maana kwenye hii sihu ninaamini kuwa politics comes to an end, ni sheria zinatakiwa kuwa at play, hata kama zimevunjwa na Mramba, ukweli uwekwe hapa ili tuelewe hizi double standards za bunge letu la taifa!
   
 12. K

  Koba JF-Expert Member

  #12
  Oct 1, 2007
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  haya mambo tutajadili mpaka yesu arudi na tunajua na yanajua wao ni wezi tuu na wameiba sana lakini bila kuwapiga nje uchaguzi ujao na kudai katiba irekebishwe sioni any chance ya mabadiliko ya kweli na nyimbo zitakuwa ni hizi hizi na mwisho tutaitwa vichaa kama walivyomwita Mrema...Zitto i warn you brother kwa sasa umaarufu wako ni kama Mrema mwanzoni kuwa carefully wasije wakakugeuzia kibao na kuanza kukubambikia kesi ili muda mwingi uishie mahakamani
   
 13. K

  Koba JF-Expert Member

  #13
  Oct 1, 2007
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180

  ...solution ni kutowachagua tuu na kudai mabadiliko ya katiba ili kuondoa sheria za kulinda aliyeko madarakani bila sababu ya msingi
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Oct 1, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Mzee mwenzangu..wakati Mudhihir Mudhihir alipotoa hoja ya Zitto kuchukuliwa hatua ya kufungiwa alikuwa ameweka msingi wa hoja hiyo kuwa Karamagi alisema "kweli" wakati akielezea suala la 15 percent ya capital allowance. Hivyo, yeye (Mudhihir) aliridhika na maelezo ya Karamagi ambayo yalikuwa yanahusu jambo hili.

  Kiini cha uongo wa Karamagi (aliodai Zitto) ni kuwa mabadiliko ya maana ya maneno (ambayo ndiyo yalifanyika) yanamaanisha mabadiliko ya sheria nzima (kuondolewa). Niliuliza wakati ule kuwa Karamagi alipata wapi mamlaka ya kuelezea maana ya mabadiliko ya sheria? Wakati wao wabunge wana haki ya kutunga sheria, hawana haki ya kuelezea maana ya sheria hiyo au kama sheria hiyo inapingana na Katiba au ina utata. Chombo chenye mamlaka hiyo ni Mahakama.

  Sasa, kama Karamagi alijua kuwa kifungu kile cha sheria bado kipo na hakijaondolewa (kiliwekwa kwenye sheria ya Income Tax ya 1973 na bado kipo kwenye sheria ya Fedha ya 2002) ina maana kwa makusudi kabisa aliamua kulipotosha Bunge na Mudhihir Mudhihir na wenzake wakakubaliana na uongo huo. Hivyo, msingi wa kumfungia Zitto unaporomoka kwani Zitto alichosema ni kweli kuwa Waziri Karamagi hakusema kweli na ushahidi upo.
   
 15. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #15
  Oct 1, 2007
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hivi hakuna mahali ambapo Zitto aweza kata rufaa kupinga adhabu aliyo pewa na Bunge? make inaonekana Bunge halikumtendea haki hata kidogo!
   
 16. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #16
  Oct 1, 2007
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Field Marshal ES, Sunday Citizen wamefanya kazi nzuri sana. Tatizo gazeti hili halipo mtandaoni. Mimi naona nisiseme kwanza ili watu wachangie. Naomba uniulize swali lako specific kidogo maana sijakuelewa.

  Kimsingi hoja yangu stands kuwa Waziri Karamagi alilidanganya Bunge. Bahati mbaya Bunge halikujadili hili. Lakini ndio mwanzo wa harakati za kuimarisha demokrasia ya Bunge. Any development process is painful, tutafika tu.
   
 17. Gigo

  Gigo JF-Expert Member

  #17
  Oct 1, 2007
  Joined: Aug 6, 2006
  Messages: 455
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Kwahiyo Zitto Hana Mke?
   
 18. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #18
  Oct 1, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Gigo, kama lengo lako ni kuharibu mada utashindwa, muandikie PM na umuulize mambo binafsi ambayo ungependa kujua.
   
 19. Dua

  Dua JF-Expert Member

  #19
  Oct 1, 2007
  Joined: Nov 14, 2006
  Messages: 2,481
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Mtafutie basi? Tumuoze hapa JF. Teh Teh ...............
   
 20. K

  Koba JF-Expert Member

  #20
  Oct 1, 2007
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180

  ...unataka kuolewa na zitto nini? si umwambie tuu nini unazunguka zunguka lakini sijui kama anaweza kuoa dume
   
Loading...